Kampuni ya Clouds media kupitia makampuni yake ya clouds fm na clouds Tv
wamebuni mbinu ya kuwaibia watanzania ambao wengi hawana uwelewa mkubwa
wa matumizi ya teknolojia ya mawasiliano kwani wanakutumia ujumbe mfupi
unaohusu shughuli za burudani wanazozifanya kisha wanakukata
hela,pasipo wewe mpokea ujumbe wa simu kujiunga na huduma hizo kiasi
wanachokata ni Tsh 150.Hili suala ni very sensitive kwani nimejaribu
kuwapigia simu watu wa huduma kwa wateja na kuwalalamikia wao wamesema
hawajui kitu zaidi ya kunishauri nitume neno STOP kwenda number 15556
Ili kusitisha ujumbe huo ambao unaiba pesa za watanzania,suala la
kujiuliza hapa ni kuwa mimi ni mwelewa wa mabo ya mawasiliano je kwa
mjomba wangu aliyepo kule kijijini Lukuredi kama atakuwa anatumiwa
ujumbe na hawa watu kila siku na anakatwa hela pasipo ridhaa yake hawa
watu watakuwa wanatengeneza mabilioni mangapi ya pesa?.Ufuatao ni copy
ya ujumbe mfupi ambao hii kampuni inautuma ovyo kwa watanzania na
kuwakata hela bila ridhaa yao
"CLOUDS TV:Angalia mkali wa ngolongolo Diamond Platnumz akiwasha moto
Fiesta 2012.Diamond amewakilisha Tabora, Dodoma.SIMU.TV;Bofya;
http://db.tt/CXiJhfHZ "
Nakala
i)Joseph Kusaga (Clouds media Group)
ii) Makamba J (Naibu waziri)
BUSTANI YA HABARI HATUHUSIKI NA HABARI HII
CHANZO NI
0 comments :
Post a Comment