Jose Mourinho alilia baada ya Sir Alex Ferguson kumkata bogi kwa kutomchagua kuwa Mrithi wake huko Manchester United.
Siri hii kubwa imetobolewa na Mwandishi
wa Habari wa Spain, Diego Torres, aliechapisha Kitabu kwamba Mourinho
alimwaga Machozi ilipotangazwa kuwa David Moyes ndie atakaekuwa Meneja
mpya wa Manchester United.
Kitabu hicho kiitwacho: "Prepare to lose: The Mourinho Era" [Jitayarishe Kushindwa-Zama za Mourinho] kimeanza kutolewa Makala zake spesho Magazetini hii leo.
Kwenye Sura ya Kwanza ya Kitabu hicho iitwayo Llorar, yaani kulia machozi,
Torres ameandika: “Mourinho, akipewa moyo na Wakala wake Jorge Mendes,
aliamini kabisa kuwa Ferguson ni mshirika wake, rafiki yake na Baba
Mlezi.”
“Mourinho aliamini kwamba alikuwa na
urafiki mkubwa wa kuaminiana na Ferguson. Aliamini na kudhani kuwa lundo
lake la Makombe, Ubingwa wa Ulaya mara 2, Ubingwa Ligi za Nchi mara 7
na Makombe mara 4 katika Nchi 4 tofauti, ni sifa na uzoefu mkubwa ambao
hakuna Mtu angekuwa navyo zaidi yake.”
“Alipofahamu kuwa Moyes ndie amechaguliwa, Mourinho hakuamini. Alipiga kelele: “Lakini hajashinda chochote!””
Kitabuni, Mwandishi Torres anaelezea
kuwa wakati huo ndio ulikuwa wakati wa fedheha kubwa kwa Mourinho kama
Meneja wa Real Madrid na anatoboa jinsi Kocha huyo Mreno alivyoshindwa
kupata usingizi kwa Siku kadhaa huku Simu ikiganda Sikioni.
Torres ameeleza kuwa kabla uteuzi wa
David Moyes, Wakala wa Mourinho, Jorge Mendes, alikuwa habanduki Old
Trafford akihaha kumganda Ferguson ili amrubuni amteue na kumpendekeza
Mourinho kama Mrithi wake na vitendo hivyo vilimpa imani kubwa Mourinho
kwamba yeye ndie atakuwa Meneja mpya Manchester United.
Imani hiyo na kuukosa Umeneja huo ndio kulimliza Mourinho kilio cha Mbwa.
HABARI KUTOKA:SOKAINBONGO
0 comments :
Post a Comment