Zikiwa
zimebaki chini ya Siku 40 kabla Manchester United hawajaanza kucheza
Msimu mpya wa 2015/16, Wachezaji wa Timu ya Kwanza wameaanza kurejea
Kituo cha Mazoezi cha Carrington Jijini Manchester.
Timu hiyo itaruka hapo Julai 13 kwenda Marekani kwa ajili ya Ziara
kabla Msimu kuanza na kucheza Mechi na Club America, San Jose
Earthquakes, Barcelona na Paris Saint-Germain.
Man United watafungua Msimu wao mpya wa Ligi Kuu England hapo Agosti 8 Uwanjani Old Trafford kwa kucheza na Tottenham.
Benchi la Ufundi likiongozwa na Meneja Louis van Gaal, Msaidizi
wake Ryan Giggs na Wasaidizi wengine wameandaa programu kabambe
kuwatayarisha Wachezaji hao.
Safari hii Van Gaal ameandaa programu spesho ili kuepuka mwanzo
mbovu alioupata Msimu uliopita ambao ulikuwa Msimu wake wa kwanza ambapo
walifungwa Mechi ya kwanza na Swansea na kuambua Pointi 13 tu katika
Mechi zao 10 za kwanza.
Lakini si Wachezaji wote wamesharejea huko Carrington kwani Wayne
Rooney, Robin van Persie na Wawili ambao wapo na Argentina kwenye Copa
America, Angel Di Maria na Marcos Rojo, bado kujumuika na wao wamepewa
muda zaidi wa kupumzika kutokana na kuwa na Timu zao za Taifa.
Mchezaji mwingine ambae anategemewa kuwa kundini ni mpya Memphis Depay alienunuliwa toka Uholanzi Klabu ya PSV Eindhoven.
Wachezaji 9 ambao walikuwa nje kwa Mkopo Msimu uliopita nao
wamerejea na hao ni Sam Johnstone, Reece James, Guillermo Varela, Jesse
Lingard, Nani, Angelo Henriquez, Javier Hernandez na Will Keane.
Kitu cha kwanza kabisa hukabiliwa nacho Wachezaji hao baada kurudi
kazini ni kupimwa Afya zao na kisha kulivaa Jopo maalum la Wasaidizi wa
Van Gaal ambao ni Wataalam toka Idara ya Sayansi ya Michezo akiwepo Jos
van Dijk, ambae amekuwa na Van Gaal kwa Miaka 8 sasa, ambae jukumu lake
ni kumtayarishia kila Mchezaji Mazoezi maalum binafsi.
Akiongelea Ziara ya USA, Van Gaal ameeleza: "Katika Mechi 2 za
kwanza, nitachezesha Wachezaji wote kwa Dakika 45 ili wazoee hali mpya.
Wamekuwa vakesheni kwa Wiki 3 au zaidi na hiyo ni kuwapa nafasi kurejea
hali ya kawaida. Chipukizi wengi watapata fursa kucheza."
KIKOSI KAMILI:
MAKIPA: David De Gea, Sam Johnstone, Anders Lindegaard, Victor Valdes.
MABEKI: Tyler Blackett, Jonny Evans, Reece James, Phil Jones, Paddy
McNair, Rafael, Marcos Rojo, Luke Shaw, Chris Smalling, Antonio
Valencia, Guillermo Varela.
VIUNGO: Daley Blind, Michael Carrick, Memphis Depay, Angel Di
Maria, Marouane Fellaini, Ander Herrera, Adnan Januzaj, Jesse Lingard,
Juan Mata, Nani, Andreas Pereira, Nick Powell, Ashley Young.
MASTRAIKA: Angelo Henriquez, Javier Hernandez, Will Keane, Wayne Rooney, Robin van Persie, James Wilson.
MECHI ZA MAN UNITED:
-ZIARA USA:
18 Jul: Club America [Saa 12 Dak 10 Asubuhi]
22 Jul: San Jose Earthquakes [Saa 12 Dak 10 Asubuhi]
25 Jul: FC Barcelona [Saa 5 Dak 10 Usiku]
30 Jul: Paris Saint-Germain [Saa 10 Dak 10 Alfajiri]
LIGI KUU ENGLAND
Agosti 8 [Saa 1445]: Tottenham Hotspur [Old Trafford]
Agosti 14 [Saa 2145]: Aston Villa [Villa Park]
UCL
Agosti 18/19 [Saa 2145]: UEFA Championz Ligi-Mechi ya Kwanza Raundi ya Mchujo
LIGI KUU ENGLAND
Agosti 22 [Saa 1445]: Newcastle United [Old Trafford]
UCL
Agosti 25/26 [Saa 2145]: UEFA Championz Ligi-Mechi ya Marudiano Raundi ya Mchujo
LIGI KUU ENGLAND
Agosti 30 [Saa 1800]: Swansea City [Liberty Stadium]
0 comments :
Post a Comment