BAADHI ya waliokuwa Madiwani wa CHADEMA katika Manispaa ya Kigoma Ujiji wamekihama chama hicho na kutimkia Chama cha ACT-Wazalendo, huku wakidai kwamba kwa muda mrefu wamekuwa wakishirikiana na ACT kuimarisha chama hicho ingawa walikuwa ndani ya CHADEMA wakiendelea kumalizia kipindi chao cha Udiwani.
Wakizungumza muda mfupi baada ya kutangazwa kujiunga na chama hicho, Madiwani hao Yunus Ruhomvya wa Kata ya Kibirizi na Adamu Shabani kutoka Kata ya Rubuga na Zubeda Nuhu, Tatu Amani Rajabu na Hawa Said, wote wa viti maalumu ambao walidai walishindwa kuhama mapema kutokana na utumishi wao ndani ya Halmashauri ya Manispaa Kigoma Ujiji.
Adam Shabani, aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Jimbo la Kigoma Mjini hadi alipoondolewa kwenye wadhifa huo mwaka uliopita (2014), alisema ameamua kuhamia ACT kwa vile ni chama kinachowajali Watu wa Kigoma, hivyo kinafaa kuungwa mkono wa kila mmoja.
“Nilikuwa CHADEMA lakini sasa nimehamia ACT. Nawaomba sana wale walioamua kubaki CHADEMA muache tabia ya kutukanana na kama mkiendelea kutoa matusi na sisi tutatoa matusi kwa vile kila mmoja ana mdomo, niwaombe tufanye siasa za kistaarabu ili tujenge Mji wetu wa Kigoma,”
alisema Shabani.
Kwa upande wake Yunus Ruhomvya, alisema amekuwa Naibu Meya wa Manispaa ya Kigoma Ujiji kuanzia 2010 hadi 2015 akifanya kazi ya usimamizi wa maendeleo ya Kigoma kwa mafanikio kwa vile kipindi kirefu cha uongozi wao Meya wa Manispaa hiyo, Bakari Beji alikuwa masomoni Chuo Kikuu cha Mzumbe.
Ruhomvya alisema kuwa:
Kwa upande wake Yunus Ruhomvya, alisema amekuwa Naibu Meya wa Manispaa ya Kigoma Ujiji kuanzia 2010 hadi 2015 akifanya kazi ya usimamizi wa maendeleo ya Kigoma kwa mafanikio kwa vile kipindi kirefu cha uongozi wao Meya wa Manispaa hiyo, Bakari Beji alikuwa masomoni Chuo Kikuu cha Mzumbe.
Ruhomvya alisema kuwa:
“Wakati chama cha ACT kinaanzishwa tulishindwa kwenda wote hivyo tukaamua kuwatanguliza Viongozi wetu wa Chadema waende kujenga ACT ili sisi Madiwani tutakapokamaliza muda wetu wa uongozi tukajiunge nao kama tulivyofanya sasa. Tumekuja na mapanga kufyeka msitu na tutahakikisha Chadema tunaimaliza.”Makamu Mwenyekiti wa ACT Taifa, Shabani Mambo alisema Madiwani hao ni wa mwanzo tu kujiunga na Chama hicho kinachojipambanua kunyakua Majimbo yote manane mkoani Kigoma.
- via Kigoma LIVE blog
0 comments :
Post a Comment