-->

FIJI YAWEKA REKODI MPYA KATIKA SOKA,YASHINDA BAO 38 KWA BILA

Kwa mashabiki wengi wa kandanda ya kimataifa, timu ya taifa inaposhindwa japo kwa mabao 3-0 huwa ni uchungu mwingi sana kwa wananchi.

Lakini hebu tafakari kichapo cha mabao 30-0 ?

Haya basi, timu ya taifa ya visiwa vya Bahari ya Pacific, ya Micronesia ilichapwa 30-0 na Tahiti katika mechi ya kwanza ya kanda hiyo.

Masaibu yao hayakuishia hapo, siku ya jumapili, maji yalizidi unga ! Timu hiyo iliambulia mvua ya mabao 38 mikononi mwa Fiji!

Amini usiamini japo Micronesia hawakuwa na bahati ya kuweka rekodi kwa kutwaa kombe la mwaka wa 2015 ,lakini timu hiyo ina bahati kubwa kwani kichapo hicho huenda kikatokea kuwa kikubwa zaidi duniani.
Hata hivyo wanabahati sana, jina lao halitajumuishwa kwenye madaftari ya historia; Kisa na maana Micronesia si mwanachama wa FIFA.

Aidha, timu iliyocheza mechi hiyo ilikuwa ni ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 23.

Mechi hiyo ilikuwa mechi ya kufuzu michezo ya Olympiki.

Micronesia iliamua kumchezesha mchezaji wa kawaida kama mlinda lango baada ya mapumziko, ambapo tayari ilikuwa imefungwa mabao 21-0 na baadaye katika kipindi cha pili ikamiminiwa mabao mengine kumi na saba.

Antonia Tuvania alifunga mabao 10 huku mwenzake Christopher Wasasala akifunga 7 

Micronesia ilijikakamua na kutofungwa bao lolote kati ya dakika za 12 hadi 22.
http://ichef.bbci.co.uk/news/ws/624/amz/worldservice/live/assets/images/2015/02/03/150203170724_fiji_flag_512x288_getty_nocredit.jpgTimu hii itacheza mechi yake ya mwisho ya makundi dhidi ya visiwa vya Vanutu.

Vanutu ilitoka sare tasa na Fiji katika mechi yao ya awali.

Timu hiyo inawachezaji 18 pekee badala ya 23 inavyohitajika katika mashindano yenye hadhi kama hiyo.

Mechi inayoshikilia rekodi ya dunia kwa kuwa na matokeo ya juu zaidi ni ile kati ya Australia na Samoa.

Australia ilipoibwaga Samoa kwa mabao 31-0 katika mechi ya kufuzu kwa kwa kombe la dunia mwaka wa 2001.

MICRONESIA 
nullMicronesia ni muungano wa visiwa 600 vilivyoko Magharibi mwa bahari ya Pacific. 

Micronesia ni muungano wa visiwa 600 vilivyoko Magharibi mwa bahari ya Pacific.

Visiwa hivyo vimeunganishwa katika majimbo 4 Kosrae, Pohnpei, Chuuk na Yap.

Nchi hii iko katika eneo la bahari lenye ukubwa, mara tano wa nchi ya Ufaransa huku nchi yenyewe ikiwa na jumla ya watu 100,000 pekee.

Licha ya kuwa taifa huru kuanzia mwaka wa 1986,Micronesia ilitia sahihi mkataba wa kudumu wa usalama na Marekani ambao unaipa Marekani uhuru wa kukita kambi yake katika bahari ya Micronesia.

Katika mkataba huo Marekani itadumisha usalama wa nchi hiyo huku wakiwa huru kujenga kambi zao za kijeshi mahala popote katika jamhuri hiyo mbali na kufaidi maliasili yote ya Micronesia.
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment