Chile mabingwa wapya Copa America
Timu ya Chile imefanikiwa kutawazwa mabingwa wa Copa America baada ya kuifunga Argentina kwa penalti 4 - 1 katika ardhi ya nyumbani.
Matias Fernandez, Arturo Vidal, Charles Arangui na Alexis walifunga mikwaju yao ya penati kwa upande wa Chile huku Argentina wachezaji waliokosa penati ni Gonzalo Higuain ambaye alipaisha juu wakati golikipa wa Chile Claudio Bravo alipangua mkwaju wa penati uliopigwa na Ever Banega huku Messi akiwa ni mchezaji pekee aliyefunga penati ya Argentina.
0 comments :
Post a Comment