Paide Linnameeskond inayojulikana kama Barcelona ya Estonia kutokana na rangi za jezi zao,wameichakaza klabu ya JK Raudteetoolised mabao 31-0 kwenye mechi ya kombe la Estonia iliyochezwa tarehe 30/06/2015.
Mchezaji wa Paide Sander Roivassepp alifunga magoli tisa huku nane akifunga kipindi cha kwanza, mchezaji mwenzake Sander Sinilaid akarudi nyavuni mara nane.
Hata hivyo matokeo hayo si makubwa kwenye kombe la Estonia kwa mwaka 2015.
Tallinna InfoNet iliichakaza klabu ya Virtsu Jalgpalliklubi magoli 36-0 katikati ya mwezi wa juni pia imewahi kutokea ushindi wa 20-0, 14-0, 12-1 na 10-1 katika mashindano hayo.
0 comments :
Post a Comment