Shaffih Dauda ni moja miongoni mwa wachambuzi wakubwa wa mpira na wanaopendwa nchini Tanzania kama vile alivyopendwa Dr Leakey katika zama hapo nyuma.Shaffih Dauda kupitia mtandao wake aliandika habari ya kuhusu sakata la Okwi na huku akibainisha msimamo wake kwamba utata wa swala la Okwi umekwisha na FIFA ndio waliuomaliza utata huo.Hivyo kwa mujibu wa habari yake hiyo Shaffih Dauda haoni kama kuna hatari yoyote ya Emmanuel Okwi kuichezea klabu ya Yanga.
"Kuna baadhi ya watu wanaamini usajili wa Okwi bado unautata,binafsi siamini hilo.Utata wa Okwi ulimalizika pale FIFA ilipothibitisha uhalali wa Okwi kukipiga na mabingwa hao wa mitaa ya Twiga na Jangwani,full stop.FIFA wanatambua mgogoro kati ya Simba na Etoile Du Sahel unaohusu malipo,FIFA wanatambua mgororo wa Okwi na Etoile Du Sahel unaohusu madai ya Okwi ya fedha zake na yale ya Klabu kuhusu utovu wa nidhamu wa Okwi na kukiuka mkataba wake,FIFA inatambua kujiunga kwa Okwi Sc Villa,FIFA inatambua kama Okwi kauzwa Yanga,FIFA inajua kama TFF wamemzuia Okwi kucheza VPL na pia wanatambua kama CAF imemzuia kucheza michuano ya klabu bingwa Afrika.Leo hii wameridhia Okwi kucheza Yanga,utata unatoka wapi?"
Katika hali ya kushangaza Shaffih Dauda amekuwa kigeugeu baada ya kuandika post kwenye ukurasa wake wa facebook akiwapa tahadhari kuhusu kuchezeshwa Emmanuel Okwi katika mechi zozote kwani kwa mujibu wa matini ya ujumbe huo anamaanisha kuna hatari ambayo yeye anaiona katika swala la kuchezeshwa kwa mchezaji huyo.
"
"Jamani mimi sina uwezo wa kumzuia Okwi asichezee YANGA,vile vile sina uwezo wa kuzuia maamuzi ya FIFA,nimetoa tu angalizo huyo mchezaji akitumika basi maswala yake ya kimkataba na klabu ya Etoile du Sahel yawe cleared, Nimetoa maoni yangu kwa nia njema kabisa ili wahusika walifatilie hili jambo kwa umakini baada ya kugundua Etoile nao wanadai wanamiliki haki za huyo mchezaji."
huku rafiki yake kipenzi Edo Kumwembe nae aliweka post ya kuipongeza Yanga kwa kukamilisha zoezi zima la kumsajili Emmanuel Okwi na kuwasifu kwa utendaji wa mzuri wa kufanikisha swala hilo zito kama alivyonukuliwa.
"Mara chache Yanga kutaka jambo lao kwa upande ule halafu
wakashindwa. Okwi rasmi Yanga. Japo kwa sasa. Fifa hao. Dah dunia
yote imejaa fitna. Well done Yanga. Ngoja nimpigie mwanasiasa wa
upande wa pili aanze kunipa ngonjera zake . . "
Mwisho wa nukuu.
HEBU NA WEWE TUAMBIE NI SALAMA KWA OKWI KUWEZA KUCHEZESHWA BAADA YA RUHUSA YA FIFA AU LAA!!
0 comments :
Post a Comment