-->

KAPOMBE AGOMA KURUDI UFARANSA,KISA MSHAHARA WAKE WA MWEZI NOVEMBA


Shomari Kapombe akiwa naGallas
 Shomary Kapombe amegoma kurejea Ufaransa kwa madai
halipwi mishahara, lakini AS Cannes imeitaka Simba SC itoe Euro

33,000 sawa na Sh. Milioni 66 ili irejeshewe mchezaji wake huyo.
Ajabu sasa, mchezaji huyo anayeweza kucheza nafasi za ulinzi pia
pembeni na katikati, alitolewa bure kwenda AS Cannes katikati ya
mwaka jana akiwa bado ana Mkataba na klabu hiyo ya Msimbazi, unaomalizika Aprili mwaka huu. Hans pope alifunguka na kulizungumzia hili "“Mimi nilimuita
Kapombe Desemba (mwaka jana) ofisini kwangu tukazungumza
naye, akaniambia hataki kurudi Ufaransa kwa sababu wale jamaa
hawakumpa mshahara wa Novemba, nikamuambia nenda
watakupa kule, akagoma.Nikamuambia kama suala ni hilo, mimi
nakupa huo mshahara wako uende kule kama wale jamaa watanirudishia fedha zangu sawa, akakataa kupokea fedha. Pale
pale nikajua kuna kitu kingine,”alisema Hans Poppe. Poppe amesema anaamini kabisa Kapombe amerubuniwa na timu
moja ya nchini kati ya mbili, ili abaki hapa kujiunga nayo hivyo
anatoa visingizio visivyo na mantiki. Poppe amesema kwamba baada ya hapo, aliwasiliana na AS Cannes
kuomba mchezaji huyo arejeshwe Simba SC, lakini wakaambiwa
walipe Euro 33,000. “Hapa sasa ndio pagumu, sisi tulimtoa yule mchezaji bure kwa
makubaliano wakimuuza watupe asilimia 40, na kwa kweli Shomary
angeuzwa pale, maana ile klabu inauza sana wachezaji na sisi
tungenufaika kwa kupata fedha nyingi,”. “Na hili la sisi kulipa Euro 33,000 wakati pia mchezaji mwenyewe
anamaliza Mkataba mwezi wa nne, inakuwa ngumu. Tulikuwa tuna
sera nzuri sana kwa ajili ya kuwasaidia wachezaji, ila mambo
yenyewe kama ndio hivi hatuwezi kufanya hivi siku
nyingine,”alisema Poppe. Aidha, Kapteni huyo wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania
(JWTZ) amesema wameona bora waiache klabu hiyo ya Cannes
imuuze Kapombe ili wao wapate asilimia yao 40 ya mauzo na dau
wanalotaka ni Euro 70,000 sawa na Sh. Milioni 140,000 ambapo
Simba itapata Euro 28,000 sawa na Sh. Milioni 56. Poppe amesema kwamba kwa kuwa Kapombe ana Mkataba na AS
Cannes, basi klabu hiyo ndiyo itakayomuuza na anaamini watapata
fungu lao.

Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment