Na Bakari Masasi (MUM)
Wafanyakazi wa kampuni ya Strabag, inayojenga barabara ya mabasi yaendayo kasi, wakimdhibiti kijana aliyetuhumiwa kuiba vifaa vya ujenzi wa miundombinu ya barabara na kukwamisha kwa muda maendeleo ya ujenzi huo katika eneo la Magomeni Kagera jijini Dar es salaam.
Hata hivyo, kundi la vijana wanaodhaniwa kuwa vibaka wenziye, walifanikiwa kumkomboa kijana huyo kabla ya kufikishwa kwenye mikono ya sheria, baada ya kutokea tafrani kubwa kati ya wahuni hao na wafanyakazi wa Strabag waliopewa dhamana ya ujenzi huo na serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, chini ya wizara ya ujenzi inayoongozwa na Mh. Magufuri.
Katika tukio hilo, mmoja wa wafanyakazi wa Strabag (aliyemshika kijana huyo, Pichani) alijeruhiwa vibaya kwa mawe kutoka kwa wahuni hao wakati wa harakati hizo za kumkomboa mwenzao ambaye walitokomea naye vichochoroni huku bado akiwa amefungwa kamba.
0 comments :
Post a Comment