HOTUBA YA
MHESHIMIWA DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA
TANZANIA WAKATI WA KUVUNJA BUNGE LA KUMI NA KUAGANA NA WABUNGE, UKUMBI
WA BUNGE, DODOMA 9 JULAI, 2015
Mheshimiwa Spika;
Tunayo
kila sababu ya kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehma kwa kutujalia
uzima na kutuwezesha kuishuhudia siku hii adhimu katika historia ya
Bunge letu na nchi yetu. Hatimaye siku ya kulivunja Bunge la Kumi
imewadia ili kuwezesha hatua husika za mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa
mwaka 2015 ziweze kutekelezwa.
Nakushukuru
sana Mheshimiwa Spika kwa kunipatia nafasi hii ya kulihutubia Bunge
lako tukufu ili niweze kutimiza wajibu wangu huo wa msingi Kikatiba.
Lakini, shukrani zangu kubwa ni kwa uongozi wako mahiri na shupavu.
Umeliongoza Bunge vizuri. Najua haikuwa kazi rahisi. Penye wengi pana
mengi. Lakini kwa uhodari mkubwa umeweza kulifikisha jahazi bandarini
salama salmini. Hakika wewe ni nahodha makini na jemedari hodari,
uliyethibitisha uhodari na umakini wako katika uwanja wa medani. Wewe
ndiwe mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huu wa juu kabisa katika
mhimili huu wa kutunga sheria na umeidhihirishia dunia kuwa wanawake
wakipewa nafasi wanaweza.
Mheshimiwa Spika;
Niruhusu
pia nitoe shukrani na pongezi zangu za dhati kwa Waheshimiwa Wabunge kwa
kazi kubwa na nzuri waliyoifanya. Wametimiza ipasavyo wajibu wao wa
Kikatiba wa Kutunga Sheria na kusimamia Serikali. Nawashukuru kwa
ushirikiano wenu na msaada wenu. Ni ukweli ulio wazi kuwa bila ya ninyi
Wabunge wetu na Bunge hili, tusingeweza kupata mafaniko na maendeleo
tuliyoyapata. Mmejijengea, nyinyi wenyewe na Bunge letu heshima kubwa
mbele ya wananchi. Mmeitendea haki demokrasia ya Tanzania na kuliletea
heshima kubwa Bunge letu nchini, kikanda na kimataifa.
Mheshimiwa Spika;
Tarehe 30
Desemba 2005 nilipozindua Bunge la Tisa nilielezea mtazamo wangu kuhusu
nchi yetu na kutaja majukumu ya msingi na vipaumbele vya Serikali ya
Awamu ya Nne. Nilisema tutatekeleza wajibu wetu na vipaumbele hivyo kwa
ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya. Tarehe 16 Julai, 2010 wakati wa
kuvunja Bunge hilo nilielezea mafanikio tuliyopata na changamoto
zilizotukabili katika kipindi hicho. Tarehe 28 Novemba, 2010 wakati wa
kuzindua Bunge hili la Kumi niliainisha vipaumbele vya Serikali ya Chama
cha Mapinduzi katika kipindi changu cha pili cha uongozi wa nchi yetu
na kuahidi kuvitekeleza kwa ari zaidi, nguvu zaidi na kasi zaidi. Kama
ilivyo ada, leo tunafikia mwisho wa uhai wa Bunge la Kumi, naomba
kutumia fursa hii kutoa mrejesho wa utekelezaji wa Leo tunapoagana,
ninyi na mimi, ni mashuhuda kuwa Tanzania na Watanzania tumebakia kuwa
wamoja. Hata hivyo, katika kipindi hiki kumekuwepo na matukio ya hapa na
pale madogo na makubwa, yaliyotishia umoja wa nchi yetu na watu wake.
Yapo mambo yaliyopandikizwa kuleta chuki baina ya Tanzania Bara na
Zanzibar, baina ya Wakristo na Waislamu na baina ya maeneo fulani ya
nchi na wengine.
Bahati
nzuri, msimamo thabiti wa viongozi wakuu wa Serikali zetu mbili
wakisaidiwa na viongozi wengine pamoja na ushirikiano na viongozi wa
dini na wa jamii na uelewa wa wananchi, vimeliwezesha taifa letu
kushinda changamoto hizo na matishio yote hayo. Changamoto hizi
zimethibitisha ubora wa mazungumzo. Ni kweli kabisa kwamba wanaozungumza
hawagombani na wanaozungumza humaliza tofauti zao bila kugombana.
Mheshimiwa Spika;
Niruhusuni,
nitumie nafasi hii kuwashukuru kwa mara nyingine viongozi wakuu
wenzangu, viongozi wa dini, viongozi wa jamii na wananchi wote kwa
nafanikio tuliyoyapata katika kudumisha umoja wetu. Hata hivyo,
tahadhari kubwa lazima iendelee kuchukuliwa kwani watu wenye nia mbaya
kwa nchi yetu au na umoja wetu hawajaisha na hawajafurahi kwamba
hawajafaulu. Huenda wakajaribu tena. Tunachotakiwa kufanya ni kuendelea
kushikamana ili hata wakijaribu tena washindwe.
Muungano Wetu Umeimarika Zaidi
Mheshimiwa Spika;
Nafurahi
kwamba namaliza kipindi changu cha uongozi tukiwa tumeweza kudumisha na
kuuimarisha Muungano wetu adhimu na adimu Barani Afrika. Mtakumbuka kuwa
katika hotuba yangu ya kufungua Bunge la Tisa nilisisitiza umuhimu wa
viongozi wa pande zetu mbili kukutana mara kwa mara kuzungumzia ustawi
wa Muungano wetu. Nafurahi kwamba jambo hili limefanyika chini ya
uenyekiti wa Makamu wa Rais, akisaidiwa na Waziri Mkuu kwa upande wa
Tanzania Bara na kwa upande wa Zanzibar, Waziri Kiongozi katika awamu
yangu ya kwanza na Makamu wa Pili wa Rais katika awamu hii. Majukumu ya
Serikali na yale mambo ambayo tuliahidi na kupanga kufanya.
Umoja, Amani na Usalama
Mheshimiwa Spika;
Niliahidi
kuwa katika kipindi cha uongozi wangu nitafanya kila niwezalo
kuhakikisha kuwa Tanzania inaendelea kuwa nchi moja na watu wake
wanaendelea kuwa wamoja, wanaopendana na kushirikiana licha ya tofauti
zao za rangi, dini, makabila, mahali watokako, na ufuasi wa vyama vya
siasa. Pia, kwamba nchi yetu inaendelea kuwa yenye amani, usalama na
utulivu.
Leo
tunapoagana, ninyi na mimi, ni mashuhuda kuwa Tanzania na Watanzania
tumebakia kuwa wamoja. Hata hivyo, katika kipindi hiki kumekuwepo na
matukio ya hapa na pale madogo na makubwa, yaliyotishia umoja wa nchi
yetu na watu wake. Yapo mambo yaliyopandikizwa kuleta chuki baina ya
Tanzania Bara na Zanzibar, baina ya Wakristo na Waislamu na baina ya
maeneo fulani ya nchi na wengine.
Bahati
nzuri, msimamo thabiti wa viongozi wakuu wa Serikali zetu mbili
wakisaidiwa na viongozi wengine pamoja na ushirikiano na viongozi wa
dini na wa jamii na uelewa wa wananchi, vimeliwezesha taifa letu
kushinda changamoto hizo na matishio yote hayo. Changamoto hizi
zimethibitisha ubora wa mazungumzo. Ni kweli kabisa kwamba wanaozungumza
hawagombani na wanaozungumza humaliza tofauti zao bila kugombana.
Mheshimiwa Spika;
Niruhusuni,
nitumie nafasi hii kuwashukuru kwa mara nyingine viongozi wakuu
wenzangu, viongozi wa dini, viongozi wa jamii na wananchi wote kwa
nafanikio tuliyoyapata katika kudumisha umoja wetu. Hata hivyo,
tahadhari kubwa lazima iendelee kuchukuliwa kwani watu wenye nia mbaya
kwa nchi yetu au na umoja wetu hawajaisha na hawajafurahi kwamba
hawajafaulu. Huenda wakajaribu tena. Tunachotakiwa kufanya ni kuendelea
kushikamana ili hata wakijaribu tena washindwe.
Muungano Wetu Umeimarika Zaidi
Mheshimiwa Spika;
Nafurahi
kwamba namaliza kipindi changu cha uongozi tukiwa tumeweza kudumisha na
kuuimarisha Muungano wetu adhimu na adimu Barani Afrika. Mtakumbuka kuwa
katika hotuba yangu ya kufungua Bunge la Tisa nilisisitiza umuhimu wa
viongozi wa pande zetu mbili kukutana mara kwa mara kuzungumzia ustawi
wa Muungano wetu. Nafurahi kwamba jambo hili limefanyika chini ya
uenyekiti wa Makamu wa Rais, akisaidiwa na Waziri Mkuu kwa upande wa
Tanzania Bara na kwa upande wa Zanzibar, Waziri Kiongozi katika awamu
yangu ya kwanza na Makamu wa Pili wa Rais katika awamu hii.
Mafanikio
yaliyopatikana ni makubwa. Masuala mbalimbali ya zamani na mapya
yameshughulikiwa na kupatiwa ufumbuzi. Kwa mfano, hadi mwaka 2005
zilikuwa zimebakia kero 13 za Muungano zilizoainishwa na Tume ya
Shelukindo, hivi sasa zimebaki kero nne. Tayari ufumbuzi wa kero moja
unakamilishwa kiutawala na tatu zimeshughulikiwa katika Katiba
Inayopendekezwa. Kama kura ya maoni ingekuwa imefanyika na Katiba hiyo
kupitishwa kungekuwa hakuna kiporo cha kero za Tume ya Shelukindo.
Lakini kwa vile kura ya maoni haijafanyika ndiyo maana tunaendelea
kuzitaja. Hata hivyo, Serikali zetu mbili zimezungumza na kukubaliana
tutafute njia ya kumaliza suala la rasilimali ya mafuta na gesi. Ndiyo
maana katika Muswada wa Petroli hoja ya Zanzibar kuwa na mamlaka kamili
ya kusimamia uchimbaji wa mafuta na kumiliki mapato yake ilijumuishwa.
Natoa shukrani nyingi kwa Bunge lako tukufu kwa kupitisha Muswada huo.
Moja ya kero kubwa katika Muungano tumeimaliza.
Mpasuko wa Kisiasa Zanzibar
Mheshimiwa Spika;
Mtakumbuka
kuwa nilizungumzia kusononeshwa kwangu na mpasuko wa kisiasa uliokuwepo
Zanzibar wakati ule na kuelezea utayari wangu wa kusaidia kuuondoa.
Kama mjuavyo mazungumzo yalifanyika ndani ya CCM na CUF na baina ya
vyama hivyo na muafaka ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa
ikaundwa na mpasuko wa kisiasa ukawa umepatiwa tiba. Matokeo ya yote
hayo ni kuwa mazingira ya kisiasa na kijamii yamekuwa bora zaidi siku
hizi kuliko ilivyokuwa kabla ya hapo.
Ni
matumaini yangu kuwa ndugu zetu wa Zanzibar watayadumisha mafanikio haya
ili waendelee kuishi kwa amani, upendo na udugu. Natambua kuwepo kwa
changamoto za hapa na pale katika uendeshaji wa Serikali hiyo. Jambo
linalonipa faraja ni kuwa matatizo yenyewe hayahusu muundo wa Serikali
bali yanaletwa na watu kupishana kauli au kutofautiana katika uendeshaji
wa baadhi ya mambo. Mimi naamini hayo ni mambo yanayoweza kumalizwa kwa
wadau kukaa kitako na kuzungumza kama ilivyokuwa kabla ya muafaka.
Amani na Usalama
Mheshimiwa Spika;
Jeshi la
Ulinzi la Wananchi wa Tanzania limeendelea kutimiza ipasavyo jukumu lake
la kulinda uhuru na mipaka ya nchi yetu. Nchi iko salama. Katika
kipindi hiki tumewekeza sana katika kuliimarisha Jeshi letu kwa vifaa na
zana za kisasa za kivita na mafunzo. Tumeimarisha Kamandi za Nchi Kavu,
Anga na Majini. Utayari wa jeshi letu kivita ni mzuri tena wa hali ya
juu. Weledi na nidhamu ya Wanajeshi wetu ni ya hali ya juu. Tumeboresha
maslahi na makazi ya wanajeshi kwa kujenga nyumba mpya za kuishi.
Utekelezaji wa mpango wa kuwajengea nyumba 10,000 unaendelea vizuri.
Hadi hivi sasa nyumba 6,064 zinaendelea kujengwa nchi nzima na kati yake
nyumba 3,096 zimekamilika. Namaliza kipindi changu cha kuwa Amiri Jeshi
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama kwa kujiamini kwamba “Tupo
vizuri”. Pamoja na hayo kazi ya utekelezaji wa Mpango wa Miaka 15 wa
kuimarisha JWTZ lazima iendelezwe ili kulifikisha Jeshi letu pale
tulipopakusudia.
Mheshimiwa Spika;
Katika
miaka 10 hii tumefanya jitihada kubwa ya kupambana na uhalifu ili
kulinda usalama wa maisha na mali za watu waishio Tanzania. Mtakumbuka
kuwa mwaka 2005 na mwanzoni mwa 2006 kulikuwa na matukio mengi ya
ujambazi. Niliahidi wakati wa kampeni na katika hotuba yangu Bungeni
kwamba hatutawaacha majambazi waendelee kutamba. Hali ile imedhibitiwa.
Ingawaje matukio ya ujambazi hayajaisha, lakini hayako kama ilivyokuwa
wakati ule.
Hali
kadhalika, matukio ya uhalifu wa kuwania mali yamepungua kutoka 53,268
mwaka 2005 hadi 43,808 mwaka 2014. Natoa pongezi nyingi kwa Jeshi la
Polisi kwa kazi kubwa na nzuri waliyoifanya na wanayoendelea kufanya.
Jambo ambalo bado hatujafanikiwa vya kutosha ni ajali za barabarani.
Lazima tuendelee kuzitafutia muarobaini wake. Niruhusuni niwatambue na
kuwashukuru Inspekta Jenerali (mstaafu) Omari Mahita, Inspekta Jenerali
(mstaafu) Said Mwema na Inspekta Jenerali Ernest Mangu aliyepo sasa kwa
uongozi wao mzuri.
Mafanikio
haya ni matokeo ya uwekezaji wa Serikali katika utakelezaji wa mpango
wa maboresho ya Jeshi la Polisi uliobuniwa wakati wa uongozi wa Ndugu
Saidi Mwema, IGP mstaafu. Jeshi la Polisi linaendelea kuwezeshwa kwa
zana, vifaa na mafunzo. Taratibu zimekamilika za kulipatia Jeshi hilo
magari ya kutosha ili kuongeza ufanisi.
Pia,
tumeendelea kuboresha maslahi na mazingira ya kuishi Maafisa na Askari.
Kwa ajili hiyo tumekarabati baadhi ya nyumba zilizopo, tumejenga nyumba
kadhaa mpya za ghorofa, za kawaida na mabweni. Mipango imekamilika ya
kupata mkopo wa kugharamia ujenzi wa nyumba 10,000 ambazo zitapunguza
kwa kiasi kikubwa tatizo la uhaba wa nyumba za kuishi katika Jeshi la
Polisi.
Mheshimiwa Spika;
Jeshi
letu la Magereza nalo limeendelea kutekeleza vizuri majukumu yake ya
kulinda wafungwa na kurekebisha tabia zao. Aidha, huduma za malazi,
mavazi, chakula na usafiri kwa wafungwa zimeendelea kuboreshwa.
Changamoto kubwa ni msongamano wa wafungwa Magerezani. Naamini mipango
ya kujenga magereza mapya na kupanua yaliyopo ikitekelezwa tatizo
litaisha. Aidha, mpango wa maboresho ya Jeshi la Magereza ukikamilika na
kutekelezwa, utaboresha mazingira ya kufanyia kazi na kuishi maafisa na
askari, hivyo kupandisha morali wao na kuongeza ufanisi.
Jeshi la Kujenga Taifa
Mheshimiwa Spika;
Ahadi
yangu ya kuanzisha upya utaratibu wa kuchukua vijana wa mujibu wa Sheria
katika Jeshi la Kujenga Taifa imetimia. Mpaka hivi sasa vijana 38,200
wamekwisha hitimu mafunzo hayo wakiwemo Waheshimiwa Wabunge. Nawapongeza
sana Waheshimiwa Wabunge walioshiriki kwa kuongoza kwa mfano. Imesaidia
sana utaratibu huo kuanza upya bila vipingamizi. Ni matumaini yangu
kuwa Wizara ya Fedha, Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa watakaa
pamoja kujadili namna ya kutafuta ufumbuzi kwa changamoto zilizopo.
Naamini zinaweza kumalizwa, vijana wetu wakashiriki mafunzo bila
matatizo yoyote.
Utawala Bora
Mheshimiwa Spika;
Katika
kipindi cha miaka kumi hii tumetekeleza dhamira yetu ya kujenga na
kuimarisha utawala bora kwa sera, sheria, mifumo, taasisi na kwa
rasilimali watu. Tumefanya hivyo katika maeneo yote muhimu yakiwemo yale
yahusuyo haki za binadamu, demokrasia, mapambano dhidi ya rushwa,
maadili ya viongozi, ukusanyaji wa mapato na nidhamu ya matumizi ya
fedha za umma na mgawano wa madaraka hati ya mihimili.
Bunge la Jamhuri ya Muungano
Mheshimiwa Spika;
Serikali
imetimiza ipasavyo wajibu wake kwa mhimili mkuu wa dola wa Kutunga
Sheria. Tulianzisha Mfuko wa Bunge na kuongeza fedha katika bajeti ya
Bunge toka shilingi bilioni 30.58 mwaka 2005/06 hadi shilingi bilioni
173.76 mwaka 2015/16. Pia tumeanzisha Mfuko wa Jimbo ili kuwawezesheni
Wabunge kuchangia katika kutatua changamoto za maendeleo zinazowakabili
wananchi wa majimbo yao. Bunge letu limetekeleza ipasavyo majukumu yake
kupitia Kamati zake za kudumu na pale ilipolazimu Kamati teule
zilizoundwa.
Katika
kipindi hiki miswada 163 imepitishwa, maswali ya msingi 7,544 na ya
nyongeza 22,632 yameulizwa na kujibiwa. Kamati teule 2 ziliundwa. Haya
ni mafanikio makubwa kwa Bunge letu. Bunge hili limefanya kazi kubwa na
kazi ya kutukuka. Michango na ushauri wake umekuwa chachu ya baadhi ya
hatua na mabadiliko ya kisera, kisheria na kiutendaji yaliyofanywa na
Serikali. Kwa kweli mnastahili pongezi nyingi. Huwezi kutaja mafanikio
ya Serikali ya Awamu ya Nne bila kutambua mchango wa Bunge hili.
Mchakato wa Katiba
Mheshimiwa Spika;
Kama sote
tujuavyo, kupitia Sheria iliyotungwa na Bunge hili, mwaka 2013
tulianzisha mchakato wa Mabadiliko ya Katiba kwa lengo la kuipatia nchi
yetu Katiba mpya iliyo bora zaidi kuliko iliyopo sasa. Nafurahi kwamba
mchakato huo ulituwezesha kupata Katiba Inayopendekezwa ambayo imekidhi
matarajio hayo. Narudia kutoa pongezi za dhati kwa Tume ya Mabadiliko ya
Katiba na Bunge Maalum la Katiba kwa kazi kubwa na nzuri waliyofanya.
Hatua iliyobaki ni Kura ya Maoni ambapo sote tunasubiri maelekezo ya
Tume ya Uchaguzi. Mimi naamini iwapo itapitishwa, Katiba Inayopendekezwa
itaimarisha zaidi taifa letu.
Vyama vya Siasa
Mheshimiwa Spika;
Katika
kipindi hiki tumeshuhudia vyama vya siasa vikiendelea kuimarika na
kujijenga nchini. Idadi ya vyama vya siasa imeongezeka kutoka 18 hadi
24. Vyama vya siasa vimefanya shughuli zake kwa uhuru. Viongozi na
wanachama wao wamefanya mikutano mingi na hata maandamano kote nchini.
Baraza la Vyama vya Siasa na TCD vimekuwa vyombo muhimu vilivyofanya
kazi nzuri ya kujenga ushirikiano miongoni mwa vyama vya siasa. Yamekuwa
majukwaa muhimu ya mashauriano baina ya vyama vya siasa kwa masuala
mbalimbali. Matatizo na changamoto nyingi zimeweza kupatiwa ufumbuzi. Ni
matumaini yangu kuwa vyombo hivi viwili vitaendelezwa na kuimarishwa
miaka ijayo.
Huu ni
mwaka wa Uchaguzi, na vyama vya siasa ndiyo wahusika wakuu. Ni matumaini
yangu kuwa vyama vya siasa vitaheshimu na kuzingatia maadili ya
uchaguzi. Hii itasaidia kuwepo kwa utulivu na amani katika mchakato wa
uchaguzi.
Uchaguzi Mkuu
Mheshimiwa Spika;
Habari
kubwa hapa nchini sasa ni uchaguzi mkuu. Tayari Tume ya Uchaguzi ya
Taifa (NEC) na ile ya Zanzibar (ZEC) zimekwisha tangaza tarehe 25
Oktoba, 2015 kuwa ni siku ya kufanyika uchaguzi mkuu. Maandalizi ya
uchaguzi huo yanaendelea vizuri. Tume ya Taifa ya Uchaguzi inaendelea na
zoezi la uandikishaji wa wapiga kura kwa mfumo mpya wa teknolojia ya
Biometric Voters Register (BVR). Hadi sasa zoezi la uandikishaji
limekamilika katika mikoa 13 na linaendelea katika mikoa 11 na katika
mkoa wa Dar es Salaam na Zanzibar uandikishaji unategemea kuanza mwezi
huu. Kwa taarifa za Tume ya Uchaguzi, tayari wamekwisha andikisha hadi
sasa wapiga kura milioni 11 kati ya lengo la kuandikisha wapiga kura
kati ya milioni 21 hadi 23.
Sisi
katika Serikali tutaendelea kutimiza wajibu wetu wa kuiwezesha Tume
kutimiza wajibu wake. Napenda kuwahakikishia kuwa kila Mtanzania mwenye
haki ya kupiga kura atapata fursa ya kuandikishwa. Shime tuhimize watu
wajitokeze kujiandikisha ili wasikose haki yao hiyo.
Uhuru wa Habari
Mheshimiwa Spika;
Mtakubaliana
nami kuwa katika kipindi hiki uhuru wa habari na uhuru wa watu kutoa
maoni yao umepanuka sana. Tanzania kuna magazeti ya kila siku 16 na kati
ya hayo ya Serikali ni 2 (Daily News, Habari Leo). Pia magazeti ya kila
wiki yapo 62. Aidha, kuna vituo vya redio kutoka 115 na vya televisheni
29. Serikali haifanyi uhakiki wa habari kabla ya kuchapishwa au
kuandikwa. Tumeamua hivyo kwa imani yangu kwamba ustawi wa demokrasia
hutegemea sana uhuru wa vyombo vya habari. Pili, kwa vile tunatambua
manufaa ya vyombo vya habari kuelimisha jamii, kupambana na maovu na
kuhimiza uwajibikaji.
Pamoja na
hayo, hatukusita wala kuchelea kuchukua hatua pale uhuru huo
ulipotumiwa vibaya na kutishia kuvuruga amani, umoja na usalama wa jamii
au taifa. Au, pale ambapo Sheria za nchi zimekiukwa. Huo ni wajibu wetu
wa kikatiba ambao mimi na wenzangu tuliapa kuutimiza.
Mheshimiwa Spika;
Serikali
ina kituo kimoja cha redio na kimoja cha televisheni. Katika kuongeza
uwazi na mawasiliano na wananchi mwaka 2007 tulianzisha tovuti ya
wananchi. Tovuti hiyo imeshapokea hoja 117,243 na kati ya hizo
zilizohusu Serikali zilikuwa 78,258 na zote zimeshughulikiwa.
Katika
kuboresha mfumo wa mawasiliano, Tanzania imeshahama kutoka mfumo wa
analogia na kuingia kwenye mfumo wa digitali. Hii ni hatua kubwa muhimu
kwa maendeleo ya tasnia ya habari nchini. Jambo ambalo nasikitika kuwa
hatukuweza kulikamilisha ni utungaji wa Sheria ya Haki ya Upatikanaji wa
Habari na Sheria ya Vyombo vya Habari. Miswada imekamilika na kusomwa
mara ya kwanza hapa Bungeni lakini mchakato wake haukuweza kufika
mwisho. Tunawaachia wenzetu wajao washughulike nayo katika Bunge la 11.
Vita dhidi ya Rushwa
Mheshimiwa Spika;
Vita
dhidi ya rushwa ni eneo jingine ambalo tulilivalia njuga katika Awamu ya
Nne. Tumepata mafanikio ya kutia moyo katika mapambano dhidi ya rushwa
ingawaje kazi bado ni kubwa. Tumefanya mambo matatu. Kwanza, tumetunga
Sheria Na. 11 ya mwaka 2007 ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ambayo
imeongeza nguvu ya mapambano dhidi ya uovu huu. Idadi ya makosa ya
rushwa iliongezwa kutoka 4 mpaka 24 na wigo wa wakosaji pia, kwa
kuhusisha watu katika sekta binafsi. Mifumo ya upelelezi na uendeshaji
mashitaka nayo imeimarishwa.
Tumeunda
chombo kipya TAKUKURU badala ya TAKURU ambacho kimepewa majukumu ya
kuzuia na kupambana na rushwa badala ya kuzuia peke yake. TAKUKURU
imepewa mamlaka zaidi katika kuongoza mapambano haya. Taasisi imeendelea
kuimarishwa kwa kuipatia zana na vifaa vya kufanyia kazi pamoja na
rasilimali watu na mahitaji mengine. Tumeiwezesha TAKUKURU kufungua
ofisi katika Mikoa na Wilaya zote.
Mheshimiwa Spika;
Maboresho
haya yamewezesha idadi ya kesi za tuhuma za rushwa zinazofikishwa
mahakamani kuongezeka kutoka kesi 50 mwaka 2005 hadi 1,900 mwaka 2014.
Jumla ya shilingi bilioni 87.8 ziliokolewa. Watumishi wa Serikali 97
wameachishwa kazi kwa tuhuma za rushwa na matumizi mabaya ya ofisi zao
baada ya ushahidi wa kijinai kukosekana. Kwa upande wa kupambana na
rushwa kwenye shughuli za uchaguzi, tumetunga Sheria ya Kudhibiti
Gharama za Uchaguzi Na. 6 ya mwaka 2010 ili kutoa majibu ya kilio cha
siku nyingi dhidi ya watu wanaotumia fedha kununua kura.
Mapato na Matumizi ya Fedha na Mali za Serikali
Mheshimiwa Spika;
Nilieleza
katika hotuba yangu ya Kuzindua Bunge la Tisa tarehe 30 Desemba, 2005
kuwa tutatoa kipaumbele cha juu kwa ukusanyaji wa mapato ya Serikali na
nidhamu ya matumizi ya Serikali. Leo miaka kumi baadae ninaona fahari
tumepata mafanikio makubwa. Mapato ya Serikali yameongezeka kutoka
shilingi bilioni 177.1 mwaka 2005 kwa mwezi hadi takriban shilingi
bilioni 850. Hii imewezesha bajeti ya Serikali kukua kutoka trilioni
4.13 mwaka 2005/2006 hadi trilioni 22.49 mwaka 2015/2016. Isitoshe
imetuwezesha kupunguza misaada na mikopo ya washirika wa maendeleo
kutoka asilimia 42 ya Bajeti ya Serikali mwaka 2005 hadi asilimia 15
mwaka 2014/2015 na tumejipa lengo la kushusha zaidi hadi asilimia 8
mwaka huu wa fedha wa 2015/2016.
Mheshimiwa Spika;
Mafanikio
haya yametokana hasa na kazi kubwa tuliyoifanya ya kuimarisha Mamlaka
ya Mapato ambao wanastahili pongezi zetu nyingi. Bado naamini tunaweza
kufanya vizuri zaidi ya hivi, kama tukiongeza udhibiti kwa mianya ya
kupoteza mapato na kuimarisha zaidi TRA na mamlaka nyingine za
ukusanyaji mapato ya Serikali. Bado ukusanyaji wa mapato yasiyokuwa ya
kodi katika Halmashauri za Wilaya na Miji na katika Wizara, Idara
zinazojitegemea na Wakala wa Serikali uko chini ya lengo. Huku kuendelee
kufanyiwa kazi.
Mheshimiwa Spika;
Kwa
upande wa nidhamu ya matumizi ya fedha na mali za Serikali tulielekeza
nguvu zetu katika kuimarisha utaratibu wa manunuzi Serikalini na ukaguzi
wa hesabu za Serikali. Kwa upande wa ununuzi wa bidhaa na huduma,
tumeendelea kuimarisha Sheria na Mamlaka ya Ununuzi wa Umma ili iweze
kuhakikisha kuwa kuna usimamizi thabiti wa sheria hiyo na kanuni zake.
Kama mjuavyo sehemu, kubwa ya fedha za Serikali hutumiwa katika ununuzi
wa bidhaa na huduma, hivyo kuwepo usimamizi mzuri ni jambo jema.
Ukikosekana, wizi na rushwa hutawala.
Mheshimiwa Spika;
Kwa
upande wa ukaguzi wa hesabu za Serikali, tumechukua hatua za makusudi za
kuimarisha Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.
Tumetunga Sheria mpya inayoipa nguvu na uhuru zaidi Ofisi hiyo. Aidha,
tumewaongezea bajeti, vitendea kazi na rasilimali watu. Ofisi 8 za Mikoa
zimejengwa na 2 zinaendelea kujengwa.
Nafurahi
kwamba maagizo yangu kwa viongozi na watendaji katika Serikali Kuu na
Serikali za Mitaa kuhusu Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu
za Serikali kupewa uzito linazingatiwa. Taarifa hizo sasa zinasomwa,
zinajadiliwa na hatua kuchukuliwa kwa kasoro zilizoonekana. Wezi na
wabadhirifu wanaobainika kuchukuliwa hatua za kisheria mara makosa
yanapogundulika. Kitaifa taarifa hiyo hujadiliwa Bungeni kwa muda wa
kutosha.
Mheshimiwa Spika;
Niliamua
pia kuanzisha Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali na kuwaweka
Wakaguzi wa Ndani wote wa Serikali Kuu na Serikali za Mitaa chini ya
Mamlaka yake na kuwajibika kwake. Ofisi hii imesaidia kuhakikisha sheria
na kanuni za matumizi ya fedha na mali ya umma zinaheshimiwa. Pia,
katika ufuatiliaji na utekelezaji wa mapendekezo ya CAG. Uimarishaji wa
ukaguzi wa ndani na ule wa CAG umesaidia kuboresha hesabu za Serikali
kuwa nzuri zaidi siku hizi. Hati safi zimeongezeka na hati chafu
zinazidi kupungua Serikalini. Kwa mfano katika Halmashauri za Wilaya na
Miji, hati safi zimeongezeka kutoka 56 mwaka 2006 hadi 150 mwaka 2014.
Hati zenye mashaka ni 13 na hakuna Hati isiyoridhisha. Kazi ya
kuimarisha ukaguzi na nidhamu ya matumizi lazima iendelezwe.
Maadili ya Viongozi wa Umma
Mheshimiwa Spika;
Katika
miaka 10 hii tumeimarisha mfumo wa kusimamia maadili ya viongozi.
Tumefanya hivyo kwa kutambua kuwa maadili mema ni sifa ya msingi ya
kiongozi na huiletea heshima Serikali. Tumeendeleza Kamati ya Maadili na
kuunda Baraza la Maadili kwa mujibu wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa
Umma namba 13 ya 1995. Tumepanua wigo na kwamba sasa mali za viongozi
na familia zao hutolewa taarifa na kiongozi katika Tamko la Mali la kila
mwaka. Hii inasaidia kuondoa uwezekano wa kiongozi kuficha mali kwa
mgongo wa mwenza wake au mtoto.
Mheshimiwa Spika;
Kamati ya
Maadili sasa si tu inapokea fomu na kuzihifadhi, bali inafanya ukaguzi
wa mali za viongozi na kuzifuatilia. Kikwazo chao ni kupata rasilimali
fedha. Hili litazamwe zaidi. Pale inapoonekana kuna makosa ya kimaadili
wahusika hufikishwa kwenye Baraza la Maadili. Sote tumeshuhudia kazi
nzuri iliyofanywa na Baraza hilo wakati wa sakata la Escrow. Bado kazi
ya kuimarisha Kamati ya Maadili kwa rasilimali fedha, vitendea kazi,
majengo ya ofisi na rasilimali watu haina budi kuendelezwa.
Muhimili wa Mahakama
Mheshimiwa Spika;
Katika
kipindi cha miaka 10 hii tumefanya jitihada kubwa za kuimarisha mhimili
wa Mahakama. Miongoni mwa mambo mengine tumefanya mambo muhimu kwa
madhumuni ya kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa jukumu lake la
msingi la utoaji haki.
Kwanza,
tumetenganisha shughuli za kutoa haki na za utawala. Tumeunda Ofisi ya
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya kushughulikia mambo ya fedha na utawala.
Hivyo basi, Wasajili wa Mahakama wanabaki na jukumu la kutoa haki. Mpaka
sasa mabadiliko haya yamekuwa ya manufaa makubwa kwa Mahakama kwani
yameboresha utekelezaji wa majukumu katika Mahakama. Pili, tumeanzisha
Mfuko wa Mahakama ambao unaipa Mahakama uhuru katika kuendesha shughuli
zake. Sambamba na hilo tumeongeza bajeti ya Mahakama kutoka shilingi
bilioni 36.6 mwaka 2006/07 hadi shilingi bilioni 87.6 mwaka 2014/15.
Jambo linalohitaji kuboreshwa ni Hazina kutoa fedha kwa wakati ili
shughuli zifanyike kama ilivyopangwa.
Mheshimiwa Spika;
Jambo la
tatu, ni kwamba tumeongeza idadi ya Majaji wa Rufani, Majaji wa Mahakama
Kuu, Mahakimu Wakazi na Mahakimu wa Mahakama za Mwanzo. Lengo letu ni
kuongeza nguvukazi ya kusikiliza na kuamua mashauri. Kwa upande wa
Mahakimu wa Mahakama za Mwanzo wameanza kuteuliwa watu wenye Shahada ya
Sheria. Hivi sasa itawawezesha watu wenye mashauri katika Mahakama hizo
kupata utetezi wa Mawakili. Kati ya mwaka 2005 na 2015 tumeongeza Majaji
wa Rufani kutoka 8 mwaka 2005 hadi 16, na Majaji wa Mahakama Kuu kutoka
37 hadi 81 katika kipindi hicho. Hali kadhalika, tumeongeza idadi ya
Majaji wanawake. Katika Mahakama ya Rufani wapo 5 na katika Mahakama Kuu
wapo 32 na kufanya jumla yao kuwa 37. Hivi sasa tunao jumla ya Mahakimu
Wakazi 1,266 katika ngazi zote za Mahakama. Kati ya hao 534 sawa na
asilimia 35 ni wanawake. Idadi ya Majaji na Mahakimu wanawake hivi sasa
ni kubwa kuliko wakati wowote uliopita.
Mheshimiwa Spika;
Kutokana
na mipango mizuri iliyowekwa na Jaji Mkuu Mohamed Chande Othman Mahakama
zimepiga hatua kubwa katika kupunguza mlundikano wa kesi Mahakamani.
Majaji wamejiwekea malengo kwa kila Jaji asikilize na kuamua mashauri
yasiyopungua 220 kwa mwaka na kila Hakimu Mkazi mashauri 250 na wale wa
Mahakama ya Mwanzo mashauri 260 kwa mwaka. Kwa sababu hiyo, kuanzia
Julai, 2014 hadi kufikia mwezi Machi mwaka 2015 yalifunguliwa mashauri
177,586 na Mahakama ilisikiliza na kuamua mashauri 179,962. Maana yake
ni kuwa zimesikilizwa zote na nyingine zilizobakia miaka ya nyuma. Bila
shaka kwa kasi hii sasa mrundikano wa kesi utabakia kuwa historia katika
kipindi kifupi kijacho. Nawapongeza sana Majaji na Mahakimu kwa kazi
nzuri waifanyayo.
Kwa
upande wa ujenzi wa majengo ya Mahakama Kuu, wamekamilisha ujenzi wa
jengo la Mahakama Kuu za Divisheni ya Kazi pamoja na majengo ya Mahakama
Kuu Mikoa ya Shinyanga na Kagera. Aidha, majengo mawili ya Mahakama za
Wilaya na 12 ya Mahakama za Mwanzo nayo yamekamilika. Hivi sasa, ujenzi
unaendelea wa majengo ya Mahakama Kuu 9 za mikoa iliyosalia, Mahakama za
Wilaya 9 na za mwanzo 25.
Maboresho ya Mfumo wa Utoaji Haki
Mheshimiwa Spika;
Jambo
lingine ambalo tumefanya katika nia ya kuongeza uwajibikaji, ufanisi, na
kupunguza malalamiko ya wananchi na ucheleweshaji wa mashauri ni
kutenganisha kazi ya upelelezi wa makosa ya jinai na uendeshaji wa
mashtaka hayo Mahakamani. Polisi waliokuwa wanafanya yote sasa
watashughulikia upelelezi na ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ndiyo
inayoendesha mashauri. Tayari Ofisi za Mkurugenzi wa Mashtaka
zimekwishafunguliwa katika kila Mkoa na sasa tunaenda wilayani. Aidha,
tumeboresha Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa rasilimali watu,
vitendea kazi na fedha ili kuongeza ufanisi katika utendaji wa ofisi
hiyo muhimu sana. Kuna haja ya kuendelea kuongezea rasilimali fedha na
vitendea kazi ili ufanisi uongezeke zaidi.
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora
Mheshimiwa Spika;
Katika
kipindi hiki, tumeimarisha Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kwa
kuiwezesha kwa nyenzo, rasilimali fedha na watu. Tume sasa inafanya kazi
katika eneo lote la Jamhuri ya Muungano. Aidha, kutokana na utumiaji wa
mfumo wa elektroniki malalamiko ya wananchi mengi zaidi yanafikishwa
kwenye Tume na mengi yanapatiwa ufumbuzi. Kwa mfano, idadi ya malalamiko
yaliyowasilishwa Tume yameongezeka kutoka 9,455 mwaka 2006 hadi 25,921
mwaka 2014 na uwezo wa Tume kushughulikia malalamiko kwa mwaka
umeongezeka kutoka malalamiko 3,021 mwaka 2005 hadi malalamiko 18,501
mwaka 2014.
Utendaji Serikalini
Maeneo ya Utawala
Mheshimiwa Spika;
Kwa nia
ya kusogeza huduma, mwaka 2010 tulianzisha mikoa mipya 4 ya Geita,
Simiyu, Njombe na Katavi na wilaya mpya 19. Pia, tulianzisha Halmashauri
45, kata 1,432, vijiji 1,949, Mitaa 1,379 na vitongoji 8,777. Nimeamua
kuanzisha mkoa mpya wa Songwe kutoka mkoa wa Mbeya na Wilaya sita kama
ifuatavyo: Tanganyika mkoani Katavi, Kigamboni na Ubungo mkoani Dar es
Salaam, Songwe mkoani Mbeya, Kibiti mkoani Pwani na Malinyi mkoani
Morogoro. Najua tulikuwa na maombi mengi lakini kwa sasa tufanye haya.
Maslahi ya Wafanyakazi
Mheshimiwa Spika;
Serikali
ya Awamu ya Nne imelipa umuhimu wa juu suala la kuboresha maslahi ya
watumishi wa Serikali. Karibu kila mwaka tumekuwa tunaongeza kima cha
chini cha mshahara. Kwa sababu hiyo, kima cha chini cha mshahara
kimeongezeka kutoka shilingi 65,000 mwaka 2005 hadi shilingi 265,000
mwaka wa jana. Mwaka huu tumefikia shilingi 300,000. Najua bado
hakikidhi mahitaji lakini ukilinganisha na tulikokuwa kipindi hiki
tumeongeza sana mishahara ya wafanyakazi. Vile vile, tumeendelea
kupunguza kodi ya mapato kwa mfululizo kutoka asilimia 18 mwaka 2005
hadi asilimia 11 mwaka huu. Dhamira yetu ni kutaka kutoa nafuu zaidi kwa
wafanyakazi. Vile vile, tumewapandisha vyeo watumishi 233,876 na kulipa
malimbikizo ya watumishi 422,348 ya kiasi cha shilingi bilioni 384.8.
Mheshimiwa Spika;
Tumetekeleza
sera ya ugatuaji wa madaraka kwa wilaya jambo ambalo limelazimu
kuongeza rasilimali fedha na watu kwa Halmashauri za Wilaya na Miji. Kwa
ajili hiyo ruzuku kwa Halmashauri zetu imeongezeka kutoka shilingi
bilioni 780 mwaka 2005/2006 hadi shillingi trilioni 4.69 mwaka
2015/2016. Aidha, tumeimarisha utumishi katika Halmashauri kwa kuajiri
watumishi wengi wa kada mbalimbali.
Usawa wa kijinsia
Mheshimiwa Spika;
Mwaka
2005 niliahidi wakati wa kampeni na wakati wa kuzindua Bunge la Tisa,
kuwa tutaongeza ushiriki wa wanawake katika shughuli na nyanja
mbalimbali za maisha ya watu wa nchi yetu ikiwemo nafasi za maamuzi.
Ninyi na mimi ni mashahidi kwamba tumetimiza ahadi hiyo. Idadi ya
Wabunge wanawake imeongezeka kutoka 62 mwaka 2005 hadi 127. Hivi sasa
hamsini kwa hamsini ni rasmi katika Katiba Inayopendekezwa. Kwa mara ya
kwanza katika historia ya nchi yetu na Bunge letu tumepata Spika
mwanamke Mheshimiwa Anne Semamba Makinda.
Wanawake
wameongezeka katika ngazi zote kuu za uamuzi. Kwa mfano, tunao Mawaziri
wanawake 10, Naibu Mawaziri wanawake 5, Majaji wanawake 37 na Wakuu wa
Wilaya wanawake wako 53. Kwa upande wa Makatibu Wakuu, Naibu Makatibu
Wakuu, Wakuu wa Mikoa, Wakurugenzi Watendaji n.k. pia wameongezeka.
Katika elimu nako tuna usawa wa kijinsia kwa upande wa idadi ya
wanafunzi wa kike na wa kiume katika shule za msingi na sekondari.
Katika vyuo vya elimu ya juu, idadi ya wanafunzi wa kike imeongezeka kwa
kasi kutoka 10,039 mwaka 2005 hadi 78,800 mwaka 2014.
Hali ya Uchumi
Mheshimiwa Spika;
Wakati
ninaingia madarakani mwaka 2005 niliwaahidi Watanzania wenzangu kuwa
tutafanya kila tuwezalo kujenga uchumi ulio imara na shirikishi.
Hususan, nilisema nitaendeleza sera za mageuzi ya kiuchumi na kuweka
misingi madhubuti ya kukuza uchumi, kuongeza ajira, kuongeza Pato la
Taifa na kupunguza umaskini. Katika miaka kumi iliyopita tumeendelea
kusimamia kwa kiwango kizuri sera za uchumi jumla na sera za uchumi
katika ngazi ya chini zinazogusa wananchi wa kawaida.
Jitihada
zetu hizo zimezaa matunda ya kutia moyo. Katika kipindi hiki, Pato la
Taifa lilikua kwa wastani wa takriban asilimia 7. Nchi yetu ni miongoni
mwa mataifa 10 ya Afrika na 20 duniani ambayo uchumi wake unakua kwa
kasi kubwa. Pato ghafi la Taifa limeongezeka zaidi ya mara tatu kutoka
shilingi trilioni 14.1 mwaka 2005 hadi kufikia trilioni 79.4 mwaka 2014.
Hivyo basi, pato la wastani la Mtanzania nalo limeongezeka kutoka
shilingi 441,030 mwaka 2005 hadi shilingi 1,724,416 mwaka 2014.
Mauzo
yetu ya nje yameongezeka kutoka Dola za Marekani bilioni 1.67 mwaka 2005
hadi Dola za Marekani bilioni 8.76 mwaka 2014 na kutunisha akiba yetu
ya fedha za kigeni na kutuwezesha kuagiza bidhaa na mahitaji ya nchi
kutoka nje kwa kipindi cha miezi 4.1 kama tulivyopanga. Mfumuko wa bei
ni asilimia 4.5.
Mheshimiwa Spika;
Kama
mjuavyo, mwaka 2000 nchi yetu ilijiwekea Dira ya Taifa ya Maendeleo ya
hadi mwaka 2025. Mwaka 2010 tulitengeneza Mpango wa Muda Mrefu (Long
Term Perspective Plan) wa (2010 – 2025) wa kuongoza utekelezaji wa Dira
kwa miaka 15 iliyobaki. Tuligawa utekelezaji wake katika Mipango mitatu
ya Maendeleo ya Miaka Mitano kila mmoja. Tuko katika hatua za mwisho za
utekelezaji wa Mpango wa Kwanza, (2011/12 – 2015/16) na kuandaa mpango
wa pili (2016/17 – 2021/22).
Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa
Mheshimiwa Spika;
Kwa
madhumuni ya kuboresha utendaji wa Serikali nilianzisha Mpango wa
Matokeo Makubwa Sasa (BRN). Huu ni mfumo mpya wa kupanga, kufuatilia na
kusimamia utekelezaji wa malengo na shughuli za Serikali kwa nia ya
kuhakikisha kuwa kilichokusudiwa kinafanyika, tena kwa wakati. Tuliamua
kuanza na sekta sita za Elimu, Nishati, Kilimo, Uchukuzi, Maji na Mapato
ya Serikali. Baadae sekta ya afya na uboreshaji mazingira ya uwekezaji
ziliongezwa.
Katika
kipindi hiki kifupi Mpango umethibitisha kuwa wenye manufaa. Mambo
katika sekta zilizojumuishwa katika BRN yameanza kwenda vizuri.
Changamoto yetu kubwa imekuwa ni upatikanaji wa fedha zinazohitajika kwa
wakati kutoka Hazina. Kama changamoto hiyo isingekuwepo mambo yangekuwa
mazuri zaidi.
Uboreshaji wa Mazingira ya Biashara na Uwekezaji
Mheshimiwa Spika;
Kwa
kutambua umuhimu wa uwekezaji katika kukuza uchumi, kuzalisha ajira,
kuongeza mapato na kupunguza umaskini, Serikali yetu imekuwa inachukua
hatua thabiti za kutengeneza mazingira mazuri ya kuwavutia wawekezaji wa
ndani na nje kuchagua Tanzania kuwa nchi inayofaa kuwekeza.
Mwaka
2010 tumetengeneza Sera na kutunga Sheria ya Ubia baina ya Sekta ya Umma
na Sekta Binafsi (Public Private Partnership—PPP). Lengo letu ni kuweka
mazingira mazuri kwa sekta binafsi kuvutika kushirikiana na Serikali
katika shughuli za kiuchumi na maendeleo. Faida kubwa ya utaratibu huu
ni kuipunguzia Serikali mzigo wa kuwekeza katika baadhi ya shughuli
ambazo sekta binafsi inaweza kubeba sehemu ya gharama. Hii siyo tu
inaongeza kasi ya maendeleo, bali kuiwezesha Serikali kuokoa fedha
ambazo inaweza kuzitumia kwa shughuli nyingine.
Juhudi
zetu za kuboresha mazingira ya uwekezaji zinaendelea kuzaa matunda mema.
Kati ya 2005 na 2014, Kituo chetu cha Uwekezaji (TIC) kimesajili miradi
7,159 yenye thamani ya Dola za Marekani bilioni 154.274. Kati ya miradi
hiyo asilimia 49.38 ni ya wawekezaji wa ndani, asilimia 23.41 ni
wawekezaji wa kutoka nje na asilimia 27.18 ni miradi ya ubia baina ya
Watanzania na wawekezaji wa kigeni. Ajira 16,000 zilipatikana. Ukuaji
huu wa uwekezaji umeongeza mapato ya Serikali.
Kwa
mujibu wa taarifa ya uwekezaji iliyotolewa na Shirika la Umoja wa
Mataifa la Viwanda na Biashara Duniani (UNCTAD) ya mwaka 2015, Tanzania
inaongoza Afrika Mashariki kwa kuvutia uwekezaji. Ilipata Dola za
Marekani bilioni 2.142 sawa na asilimia 31.5 ya uwekezaji wote katika
Jumuiya yetu.
Sekta za Uzalishaji
Sekta ya Kilimo
Mheshimiwa Spika;
Kuendeleza
kilimo ilikuwa ni moja ya mambo tuliyoyapa kipaumbele cha juu. Shabaha
yetu kuu ni kutaka kuongeza tija ili uzalishaji uongezeke, wakulima
wapate mavuno mengi, masoko ya uhakika yawepo na bei iwe nzuri ili
mapato yao yaongezeke na umasikini uwapungukie. Vile vile wao na taifa
lijitosheleze kwa chakula.
Kwa ajili
hiyo mwaka 2006 tuliasisi Programu ya miaka 7 ya Maendeleo ya Sekta ya
Kilimo (Agricultural Sector Development Programme—ASDP). Katika Programu
hiyo, matatizo yanayofanya tija na uzalishaji katika kilimo kuwa mdogo
yalitambuliwa na kutengenezewa mpango wa kuyatatua. Serikali pia
ilianzisha mikakati, programu na mipango mingine ya kuongeza msukumo
katika kuleta mageuzi ya kilimo. Miongoni mwa hiyo ni mkakati wa Kilimo
Kwanza, Mpango wa Kuendeleza Kilimo katika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania
(SAGCOT), Mpango wa Uwekezaji katika Sekta ya Kilimo (TAFSIP), Sera ya
Umwagiliaji tuliyoitunga mwaka 2010 na Programu ya Mageuzi na
Modenaizesheni ya Ushirika.
Mheshimiwa Spika;
Pamoja na
hayo, tumeongeza pia bajeti ya sekta ya kilimo kutoka shilingi bilioni
233.3 mwaka 2005/06 hadi shilingi bilioni 1,084.7 mwaka 2014/15.
Kuongezwa kwa bajeti kumewezesha fedha za ruzuku ya mbolea na pembejeo
kuongezeka kutoka shilingi bilioni 7.5 mwaka 2005/06 hadi shilingi
bilioni 299.3 mwaka 2013/14. Matrekta makubwa na madogo yameongezeka
kutoka 7,491 mwaka 2005 hadi 16,412 mwaka 2014. Kwa sababu hiyo matumizi
ya jembe la mkono yamepungua kutoka asilimia 70 hadi asilimia 62.
Tumeongeza maafisa ugani kutoka 3,379 mwaka 2005 hadi 7,974 mwaka 2014.
Vituo vya
utafiti wa kilimo tumeviongezea rasilimali fedha, watu na vitendea
kazi. Aidha, tumeanza safari ya kufufua mashamba ya mbegu ya Serikali na
kuhusisha sekta binafsi, Jeshi la Magereza na Jeshi la Kujenga Taifa
katika kuzalisha mbegu. Aidha, tumeimarisha Wakala wa Mbegu
(Agricultural Seed Agency – ASA) na kuongeza uzalishaji wa mbegu bora
kutoka tani 10,477.17 mwaka 2005 hadi tani 32,340 mwaka 2014.
Mheshimiwa Spika;
Juhudi za
Serikali kuendeleza kilimo zimezaa matunda mazuri. Tija katika
uzalishaji wa mazao ya biashara na chakula imeongezeka. Kwa upande wa
mazao ya chakula uzalishaji umeongezeka kutoka tani milioni 9.66 mwaka
2005 hadi tani milioni 16.01 mwaka 2014. Ongezeko hili limeliwezesha
taifa letu kujitosheleza kwa chakula kwa asilimia 125 mwaka 2014
ikilinganishwa na asilimia 95 mwaka 2005. Uzalishaji wa mazao ya asili
ya biashara umeongezeka toka tani 427,738 mwaka 2005 hadi tani 569,054
mwaka 2014 na uzalishaji wa mbegu za mafuta umeongezeka karibu ya mara 4
toka tani 1,389.9 mwaka 2005 hadi tani 5,545.6 mwaka 2014. Aidha,
uzalishaji wa matunda nao umeongezeka toka tani milioni 1.2 mwaka 2005
hadi tani milioni 4.4 mwaka 2014 na maua toka tani 5,862 hadi tani
10,790.
Mheshimiwa Spika;
Upatikanaji
wa masoko ya uhakika na bei nzuri kwa mazao ya wakulima bado ni
changamoto. Pia kuna tatizo la upungufu wa maghala ya kuhifadhi mazao.
Jitihada zinaendelea kupata mkopo au wabia wa kujenga maghala ya kisasa
nchi nzima. Programu ya Mageuzi na Modenaizesheni ya Ushiriki
ilianzishwa ili kutatua tatizo la masoko. Aidha, tumeanza maandalizi ya
kuanzisha soko la bidhaa (Commodity Market Exchange) kwa nia hiyo hiyo.
Naamini misingi mizuri tuliyoijenga pamoja na kuenea kwa SACCOS na
kuanza kwa Benki ya Kilimo ikiendelezwa itatoa mchango mkubwa katika
kuongeza kasi ya mapinduzi ya kilimo.
Mifugo
Mheshimiwa Spika;
Kwa
upande wa mifugo, dhamira yetu ilikuwa kuanza safari ya kuleta mageuzi
katika sekta hii. Safari hiyo tumeianza kupitia Programu ya Kuendeleza
Sekta ya Mifugo. Changamoto zinazochangia maendeleo duni ya sekta hii
zimeainishwa na kutengenezewa mkakati wa utekelezaji. Katika kipindi
hiki malambo 1,008, majosho 2,364 na maabara 104 za mifugo zimejengwa.
Visima virefu 101 vimechimbwa, malambo 370 na majosho 499 yamekarabatiwa
katika kipindi hiki cha miaka 10.
Ukarabati
na ujenzi wa majosho umeongeza idadi kutoka 2,177 mwaka 2006 hadi 3,637
mwaka 2015. Tumeongeza Maofisa Ugani kutoka 2,270 mwaka 2005 hadi 6,041
mwaka 2014. Kuhusu uhamilishaji, tumeongeza vituo kutoka kituo 1 mwaka
2005 hadi vituo 8 mwaka 2015 na kuwezesha ng’ombe 955,360 kuhamilishwa
katika miaka 10 hii.
Mheshimiwa Spika;
Mazingira
mazuri ya uwekezaji kwa sekta binafsi tuliyoyajenga yamewezesha viwanda
vya kusindika nyama, maziwa na vyakula vya mifugo kuongezeka. Viwanda
vya kusindika maziwa vimeongezeka kutoka 22 mwaka 2005 hadi 74 mwaka
2015. Viwanda vya kuzalisha vyakula vya mifugo vimeongezeka kutoka
viwanda 6 mwaka 2005 hadi 80 mwaka 2015 vikiwa na uwezo wa kusindika
tani milioni 1.4 za vyakula hivyo kwa mwaka. Aidha viwanda na machinjio
ya kisasa 9 vimejengwa katika kipindi hiki. Usindikaji wa ngozi pia
umeongezeka kutoka vipande 790,000 mwaka 2005 hadi vipande milioni 3.78
mwaka 2014. Hivi sasa kwa mfano, uzalishaji wa malisho ya mifugo (hei)
umefikia marobota 957,860 ikilinganishwa na marobota 178,100 mwaka 2005.
Safari
yetu ya kuanza kuondoka kwenye uchungaji kwenda kwenye ufugaji imeanza.
Vijiji vingi vimeandaa mipango ya matumizi bora ya ardhi na hivyo
vimetenga maeneo ya kilimo na ya ufugaji. Tuendelee kuhimiza vijiji
vyetu kutekeleza mipango hiyo ili wafugaji wapate maeneo ya malisho
mbali na mazao ya wakulima. Pia, tutimize uhamilishaji kama mlango wa
kuingilia kwenye kuboresha kosafu za mifugo yetu.
Uvuvi
Mheshimiwa Spika;
Wakati
nazindua Bunge la Tisa tarehe 30 Desemba 2005 nilisema kuwa Serikali ya
Awamu ya Nne itatoa kipaumbele kwenye kuendeleza sekta ya uvuvi. Katika
kutekeleza hayo tumefanya yafuatayo. Kwanza, nimeunda Wizara mpya ya
Mifugo na Uvuvi. Pili, tulifuta kodi ya zana za uvuvi ili kuwawezesha
wavuvi kupata zana bora na za kisasa kwa bei nafuu zaidi. Tatu,
tumeimarisha vyuo vya uvuvi na hivi sasa vina uwezo wa kudahili
wanafunzi 1,215 ikilinganishwa na wanafunzi 127 mwaka 2005. Hii
imetuwezesha kuongeza wagani wa uvuvi kutoka 103 mwaka 2005 hadi 540
mwaka 2014. Nne, tumeongeza sana juhudi za kupambana na uvuvi haramu ili
kutunza mazingira, mazalia ya samaki na kuzuia kuvuliwa au kuuawa kwa
samaki wadogo.
Tumeimarisha
maabara ya Taifa ya Samaki pale Nyegezi kwa vifaa vya kisasa na
wataalamu ili iende na wakati. Tano, tumeongeza msukumo wa kuhimiza
ufugaji wa samaki na kuwezesha mashamba ya samaki kuongezeka kutoka 13,
011 mwaka 2005 hadi 20, 325 mwaka 2014.
Uvuvi
haramu unapungua. Mapato ya sekta ya uvuvi yameongezeka kutoka shilingi
bilioni 351.6 mwaka 2005 hadi shilingi trilioni 1.8 mwaka 2013. Bado
tuna kazi kubwa ya kufanya katika sekta hii ili kuongeza tija na mapato
ya wavuvi na taifa.
Utalii
Mheshimiwa Spika;
Kwa
upande wa utalii, tumeendelea na jitihada za kuiendeleza sekta hii
muhimu. Tumeongeza kutangaza vivutio vya utalii vya nchi yetu katika
masoko makubwa duniani. Sekta ya utalii imekua kwa wastani wa asilimia
7.1 na imechangia asilimia 25 ya mapato ya fedha za kigeni. Idadi ya
watalii imeongezeka kutoka watalii 612, 754 mwaka 2005 hadi watalii
1,140,156 mwaka 2014. Idadi ya vitanda katika mahoteli imeongezeka
kutoka 15,828 hadi 21,929. Mapato pia yameongezeka kutoka Dola za
Marekani milioni 823.05 mwaka 2005 hadi Dola za Marekani bilioni 2 mwaka
2014. Ajira za moja kwa moja zimeongezeka kutoka 32,673 hadi 686,130 na
zisizokuwa za moja kwa moja kutoka 165,883 hadi 1,318,109. Haya ni
mafanikio makubwa na ya kujivunia.
Mheshimiwa Spika;
Katika
kipindi hiki tumekabiliana na tukio kubwa la ujangili wa wanyamapori
hasa wa ndovu kutokana na kushamiri kwa biashara ya meno ya ndovu na bei
kuwa kubwa katika nchi za Mashariki ya Mbali. Vuguvugu la ujangili
lilifikia kiwango cha kutishia kumaliza ndovu nchini na dunia nzima.
Tukaamua kuchukua hatua za kuidhibiti hali hiyo. Tumefanya operesheni
tatu kukabiliana na tishio hili. Ya kwanza, iliendeshwa na Idara ya
Wanyamapori na Misitu wakishirikiana na TANAPA na Ngorongoro
Conservation Area. Hii hasa ilihusu kupambana na ujangili katika hifadhi
na mapori ya Kaskazini mwa Tanzania. Mafanikio makubwa yalipatikana.
Mheshimiwa Spika;
Operesheni
ya pili ni ile iliyohusisha Jeshi la Polisi katika hifadhi na sehemu
nyingine za Tanzania. Operesheni Kipepeo kama ilivyoitwa nayo ilipata
mafanikio. Na ya tatu, Operesheni Tokomeza iliyohusisha vyombo vyote vya
ulinzi na usalama. Pamoja na changamoto zake operesheni hizi zimesaidia
sana kupunguza kasi ya ujangili nchini. Matokeo yake katika sensa ya
ndovu iliyofanyika mara ya mwisho, ukiacha Ruaha, hali katika hifadhi na
mapori mengine ina muelekeo mzuri.
Kuundwa
kwa Mamlaka ya Wanyamapori (TAWA) yenye mamlaka makubwa zaidi ya
kusimamia sekta ya wanyamapori nako kutaimarisha uhifadhi na mapambano
ya ujangili. Kwa mipango na program zilizopo Wizarani, naamini mambo
yatakuwa mazuri zaidi muda si mrefu.
Viwanda
Mheshimiwa Spika;
Katika
miaka kumi hii, sekta ya viwanda imeendelea kukua kwa kasi nzuri ya
kutia moyo. Viwanda vikubwa, vya kati na vidogo vimeongezeka kutoka 11,
544 mwaka 2005 hadi viwanda 51,224 mwaka 2015. Kati ya mwaka 2005 na
2014 na miradi 751 imepewa leseni za kudumu na BRELA ya kuanzisha
viwanda. Mchango wa sekta ya viwanda katika Pato la Taifa umefikia
asilimia 7.3 mwaka 2014 kutoka asilimia 6.8 mwaka 2005. Mchango wa
viwanda kwenye mauzo ya nje umeongezeka kutoka asilimia 9.3 mwaka 2005
hadi asilimia 23.3 mwaka 2014.
Tunategemea
ukuaji mkubwa wa viwanda katika Mpango wa Pili wa maendeleo wa miaka 5
kutokana na misingi imara tuliyoijenga katika Mpango wa Kwanza. Ujenzi
wa kiwanda cha chuma kule Liganga unatarajiwa kuanza mwaka huu na
kiwanda cha kuchakata gesi pale Lindi unatarajiwa kuanza baada ya
taratibu za kuwapatia ardhi zitakapokamilika. Hivi ni viwanda vya msingi
na mama ambavyo vitachochea kasi ya ukuaji wa viwanda nchini na uchumi
kwa jumla.
Madini
Mheshimiwa Spika;
Sekta ya
Madini ndiyo ya pili baada ya utalii kwa kuingiza fedha nyingi za
kigeni. Kama nilivyoahidi, tulipitia upya sera, sheria na mikataba ya
madini iliyokuwepo na kutengeneza sera na sheria mpya. Halikadhalika,
tulianzisha mazungumzo na baadhi ya makampuni ambayo hatimaye yalizaa
marekebisho ya mikataba yao na hivyo kuboresha maslahi ya taifa.
Kufuatia
marekebisho hayo, makampuni husika ya madini yanalipa kodi ya mapato.
Bila ya hivyo huenda mpaka leo yangekuwa hayajaanza kulipa kodi.
Kutumika kwa Sheria mpya ya Madini, viwango vipya vya mrahaba na
kupunguzwa kwa misamaha ya kodi vimeongeza mapato ya Serikali. Aidha,
tuliunda Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) ambao umewezesha
kukagua mahesabu ya migodi kuhusu uwekezaji na mauzo ya madini na
kuwawezesha TRA kutoza kodi stahiki kutoka kwa makampuni hayo.
Mheshimiwa Spika;
Mabadiliko
haya pamoja na kuongezeka kwa uwekezaji katika sekta hii yamewezesha
mchango wa sekta ya madini katika Pato la Taifa kuongezeka kutoka
asilimia 2.9 mwaka 2005 hadi kufikia asilimia 3.5 mwaka 2014. Thamani ya
mauzo ya madini nje ya nchi pia imeongezeka kutoka Dola za Marekani
milioni 655.5 mwaka 2005 hadi kufikia Dola za Marekani bilioni 1.794
mwezi Desemba 2014. Mambo yangekuwa mazuri zaidi kama bei ya dhahabu
isingeshuka katika kipindi hiki.
Mheshimiwa Spika;
Serikali
ilifanya uamuzi wa kulifufua na kuliwezesha Shirika letu la Madini
(STAMICO) kuanza tena kazi ya utafutaji na uchimbaji wa madini kupitia
kampuni zake tanzu. STAMICO kwa kupitia kampuni yake ya STAMIGOLD
imeanza kuzalisha dhahabu na kuuza nje. Vilevile, tumejiunga na Mpango
wa Uwazi wa Uvunaji wa Maliasili (EITI) ambao umesaidia sana katika
kuongeza uwazi katika biashara ya madini na kusaidia katika ukusanyaji
wa mapato kutoka kwenye makampuni ya madini.
Katika
kipindi hiki, migodi mitatu mipya ilianzishwa nayo ni Migodi ya dhahabu
wa Buzwagi (Shinyanga) na New Luika (Mbeya) na mgodi wa makaa ya mawe wa
Ngaka (Ruvuma). Aidha, miradi mikubwa mingine 8 imeendelezwa na kufikia
hatua ya kuanzisha mgodi ukiwemo Mradi wa Urani wa Mkuju (Ruvuma),
Mradi wa Chuma Liganga na Mradi wa Makaa ya Mawe wa Mchuchuma (Njombe).
Pia, ajira rasmi kwenye migodi mikubwa nchini imeongezeka kutoka
waajiriwa 3,517 mwaka 2005 hadi waajiriwa 15,000 mwaka 2014. Hali
kadhalika, makampuni ya madini yameongeza unununzi wa bidhaa na huduma
hapa nchini (local procurement) kutoka Dola za Marekani milioni 230.41
mwaka 2005 hadi Dola za Marekani milioni 536.56 mwaka 2014.
Mheshimiwa Spika;
Katika
kipindi hiki pia, tumetenga maeneo 8 kwa ajili ya wachimbaji
wadogowadogo. Maeneo haya yamewezesha wachimbaji wadogo kuchimba madini
bila bughudha. Aidha, Wizara imenunua mitambo miwili kwa ajili ya
uchorongaji wa miamba kusaidia utafiti wa madini kwa ajili ya wachimbaji
wadogo. Tumeanzisha mfuko wa kuwakopesha wachimbaji wadogo pale
Wizarani ili kutoa fursa kwa wachimbaji wadogo kupata mikopo ya
kuendeleza shughuli zao.
Miundombinu
Nishati
Mheshimiwa Spika;
Wakati
naanza kazi ya uongozi wa nchi yetu, Tanzania ilikuwa inakabiliwa na
ukame mkubwa uliosababisha upungufu mkubwa wa chakula. Pia kulikuwa na
upungufu mkubwa wa umeme kwa sababu ya mabwawa ya kuzalisha umeme kukosa
maji ya kutosha. Serikali ililazimika kulisha watu zaidi ya milioni
3,776,000 na kukodisha mitambo ya kuzalisha umeme. Kwa siku za usoni
tuliamua kuchukua hatua thabiti ya kuongeza uzalishaji wa umeme kwa
kutumia gesi asilia na vyanzo vingine kama vile makaa ya mawe, mionzi ya
jua na upepo.
Ujenzi
umekamilika wa bomba la kusafirisha gesi kutoka Mtwara na Songo Songo
litakaloongeza kiasi cha gesi kuja Dar es Salaam na kuwezesha uzalishaji
wa megawati 3000 za umeme. Wakati huo huo kazi ya kujenga vituo vya
kufua umeme inaendelea pale Kinyerezi, Dar es Salaam. Umeme huo utakidhi
mahitaji ya umeme sasa na miaka kadhaa ijayo.
Mheshimiwa Spika;
Katika
kipindi hiki tuliunda Wakala wa Umeme Vijijini (REA) ambao wamefanya
kazi kubwa na nzuri ya kusambaza umeme kwa vijiji 5,336 kati ya vijiji
12,423 nchini. Kazi kubwa iliyofanyika vijijini inapochanganywa na ile
ya mijini imeongeza idadi ya Watanzania wanaopata umeme kutoka asilimia
10 hadi asilimia 40 mwaka 2015. Uamuzi uliofanywa katika Bajeti ya mwaka
huu wa kukusanya fedha kwa ajili ya umeme vijijini kupitia mafuta ya
petroli, utasaidia sana kuongeza kasi ya kusambaza umeme vijijini.
Gesi Asilia
Mheshimiwa Spika;
Tumepata
mafanikio katika utafutaji wa mafuta na gesi asilia. Kuanzia mwaka 2010
nchi yetu imepata bahati ya ugunduzi wa kiasi kikubwa cha gesi bahari
kuu. Mpaka sasa zimegundulika futi za ujazo trilioni 47.08. Ukijumlisha
na futi za ujazo trilioni 8 zilizogunduliwa takriban miaka 40 iliyopita
kule Songo Songo na Msimbati jumla ya rasilimali ya gesi asilia nchini
ni futi za ujazo trilioni 55.08. Kazi ya utafutaji inaendelea na
wataalamu wanasema kuwa Tanzania inaweza kuwa na akiba ya futi za ujazo
trilioni 200. Kiasi cha gesi kilichogunduliwa mpaka sasa ni kikubwa na
kufanya Tanzania kuwa mahala papya pa kuipatia dunia nishati hii.
Gesi
asilia tuliyonayo ikisimamiwa na kutumiwa vizuri itaiwezesha nchi yetu
na watu wake kupata maendeleo makubwa na kuondokana na umaskini. Ni
fursa ya aina yake ya kuipatia Serikali mapato makubwa na kuiwezesha
kutimiza kwa uhakika majukumu yake na mipango yake. Lakini, ili hayo
yaweze kufanyika hapana budi pawepo usimamizi mzuri wa hatua zote muhimu
za mnyororo wa thamani: yaani utafutaji, uchimbaji, usafirishaji,
uuzaji wa gesi asilia na matumizi yake nchini kama nishati na mali ghafi
ya viwanda upande mmoja. Upande mwingine inategemea sana matumizi
mazuri ya mapato yatokanayo na rasilimali hiyo.
Mheshimiwa Spika;
Ni
kutokana na kutaka kuhakikisha kwamba mambo yanakuwa hivyo ndiyo maana
tumetunga Sera ya Gesi Asilia na kuwasilisha katika Bunge hili ile
Miswada miwili yaani wa Sheria ya Petroli na ule wa Matumizi ya Mapato
ya Mafuta na Gesi. Nawashukuru Waheshimiwa Wabunge kwa kuipitisha
Miswada hii nami nitaitia saini mara nitakapoletewa.
Usafirishaji na Uchukuzi
Barabara
Mheshimiwa Spika;
Serikali
ya Awamu ya Nne, imetoa kipaumbele cha juu kwa uendelezaji wa
miundombinu ya usafirishaji na uchukuzi nchini. Hii ni pamoja na
barabara, reli, bandari, usafiri wa majini na usafiri wa angani.
Tumeendeleza kazi ya kuongeza mtandao wa barabara za lami nchini kwa
mafanikio makubwa. Karibu barabara kuu zote nchini na zile
zinazounganisha mikoa zimekamilika kujengwa au kazi ya ujenzi
inaendelea. Kwa sababu hiyo hivi leo kutokea po pote nchini kwenda Dar
es salaam unafika siku hiyo hiyo, tofauti na ilivyokuwa zamani watu
walichukua zaidi ya siku moja. Adha ya kupita Kenya na Uganda kwa watu
wa Mikoa ya Ziwa tumeimaliza.
Katika
mkakati wetu wa kupanua mtandao wa barabara za lami nchini, tulitambua
barabara za urefu wa kilomita 11,474 za kujengwa kwa kiwango cha lami.
Baadae tuliongeza barabara nyingine na kufikisha kilomita 17,742 katika
mpango huo. Utekelezaji wake upo katika hatua mbalimbali. Tayari ujenzi
wa kilomita 5,568 kwa upande wa barabara kuu na kilomita 535 kwa
barabara za mijini umekamilika. Ujenzi wa kilomita 3,873 unaendelea.
Upembuzi yakinifu na usanifu umekamilika kwa barabara za urefu wa
kilometa 4,965 kinachosubiriwa ni kupatikana fedha ujenzi uanze. Baadhi
ya barabara hizo zimo katika bajeti ya mwaka huu wa fedha. Barabara za
urefu wa kilometa 3,336 zinafanyiwa upembuzi yakinifu na usanifu wa
kina.
Mheshimiwa Spika;
Katika
kipindi hiki pia, madaraja madogo 7,200 na makubwa 12 yamejengwa na
mengine 16 yapo katika hatua mbalimbali za ujenzi. Miongoni mwa madaraja
makubwa yaliyokamilika ni daraja la Mto Malagalasi na yanayojengwa ni
daraja la Kigamboni na lile la Mto Kilombero. Madaraja haya yalikuwa
miongoni mwa matano yaliyopangwa kujengwa katika Mpango wa Kwanza wa
Maendeleo wa Miaka Mitano mara baada ya uhuru. Madaraja mawili yaani la
Kirumi lilijengwa mwaka 1985 na la Rufiji mwaka 2003. Kwa upande wa
vivuko, tumeongeza vipya 15 na kufikisha idadi ya 28 kote nchini mwaka
2014.
Mheshimiwa Spika;
Tumeongeza
sana fedha katika mfuko wa barabara kutoka shilingi bilioni 73.08 mwaka
2005/06 hadi shilingi bilioni 866.63 mwaka 2015/16. Hii itasaidia
katika matengenezo ya barabara za lami tulizojenga na kujenga nyingine
mijini. Hali kadhalika itatumika kuimarisha barabara za udongo na
changarawe wilayani na vijijini ziweze kupitika wakati wote. Katika
kipindi hiki barabara za changarawe zimeongezeka kutoka kilometa 9,424
hadi kilometa 22,089.
Mheshimiwa Spika;
Katika
miaka kumi hii idadi ya vyombo vya moto yaani magari, bajaji na pikipiki
imeongezeka kutoka 1,696,088 mwaka 2005 hadi 3,313,254 hivi sasa.
Ongezeko hili linalotokana na hali ya kiuchumi ya watu wengi kuwa nzuri
limezua tatizo la msongamano wa magari katika miji mingi nchini. Katika
jiji la Dar es Salaam ambako tatizo ni kubwa zaidi na Serikali imekuwa
inachukua hatua mbalimbali kupunguza ukali wake. Tunapanua ukubwa wa
baadhi ya barabara, kujenga barabara za mzunguko (ring roads) na sasa
tunaanza ujenzi wa barabara za juu ya nyingine (flyovers). Tulianzisha
matumizi ya treni katika reli za TAZARA na TRC kusafirisha abiria. Hivi
sasa reli hizo zinasafirisha abiria milioni 2,804,269 kwa mwaka ambao
wangehitaji daladala 253 kwa siku. Mpango mkubwa wa kuendeleza matumizi
ya reli, Dar es Salaam umeandaliwa na tumeanza kuutafutia fedha.
Usafiri wa Reli
Mheshimiwa Spika;
Katika
kipindi hiki tumetumia muda mwingi kutafuta ufumbuzi wa matatizo
yanayozikabili reli zetu za TAZARA na TRC. Kimsingi reli hizo zimekuwa
zinakabiliwa na matatizo ya uchakavu wa miundombinu na uongozi na
uendeshaji usioridhisha. Kwa sababu ya matatizo hayo reli hizi ambazo
kila moja inaweza kusafirisha tani milioni 5 kwa mwaka zinasafirisha
kati ya tani 200,000 na 300,000 tu. Hivyo basi, mizigo mingi
husafirishwa kwa barabara na kutishia uhai wa barabara ambazo
tumezijenga kwa gharama kubwa.
Kwa
upande wa reli ya kati, uboreshaji wa reli kati ya Dar es Salaam na
Tabora unakaribia kukamilika na utaendelea mpaka Kigoma na Mwanza.
Wakati huo huo mchakato wa ujenzi wa reli mpya ya upana wa kimataifa
(standard gauge) unaendelea. Ujenzi unaweza kuanza mwaka huu kutegemea
kukamilika kwa majadiliano na mabenki yaliyoonyesha utayari wa
kutukopesha pesa za ujenzi.
Mheshimiwa Spika;
Azma yetu
ya kufufua reli ya TAZARA nayo tumeiwekea mkakati. Sisi na Zambia
tumekubaliana kushirikiana kwa karibu katika kutafuta ufumbuzi wa
matatizo yanayoikabili reli yetu hiyo. Bahati nzuri marafiki zetu wa
China nao wamekubali kutusaidia katika mipango yetu hiyo. Ni matumaini
yangu kuwa safari hii tutapata ufumbuzi wa kudumu kwa matatizo
yanayoathiri ufanisi wa reli hii yenye umuhimu wa aina yake kwa uhai na
ustawi wa uchumi wa nchi zetu na watu wake.
Bandari
Mheshimiwa Spika;
Tumeboresha
na kuimarisha huduma katika bandari ya Dar es Salaam kwa mafanikio
makubwa. Mwaka 2014 bandari yetu ilihudumia tani milioni 14.4
ukilinganisha na tani milioni 6.7 mwaka 2005. Mwaka huu inaweza kufikia
tani milioni 18. Siku hizi huduma hutolewa kwa saa 24 na kasi ya
kupakua, kupakia na kutoa mizigo imeongezeka sana na wizi umepungua
sana. Hata wale walioacha kuitumia bandari yetu wameanza kurudi.
Mheshimiwa Spika;
Kuanza
kutumika kwa mfumo wa Single Custom’s Territory unaorahisisha upakuaji
na upakiaji mizigo ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kumeongeza
zaidi ufanisi. Tuko katika majadiliano na DRC na Zambia ambao nao
wameonyesha nia ya kuingia katika mfumo huu.
Kuongezeka
kwa usafirishaji wa mizigo inayopita nchini kuna faida kwani sekta ya
usafirishaji inachangia zaidi ya asilimia 15 ya pato la taifa. Hali
kadhalika, ujenzi wa gati za 13 na 14 katika bandari ya Dar es Salaam
unaotegemewa kuanza mwezi huu utawezesha huduma ya makasha kuongezeka
kutoka makasha 600,000 hadi makasha 1,200,000. Mipango ya kuboresha
bandari za Mtwara, Tanga na zile zilizo kwenye Maziwa yetu makuu na
ujenzi wa bandari ya Bagamoyo zitaiwezesha Tanzania kunufaika na fursa
ya jiografia yake.
Usafiri wa Anga
Mheshimiwa Spika;
Katika
kipindi hiki tumefanya jitihada kubwa ya kuwekeza kwenye ukarabati,
upanuzi na ujenzi wa viwanja vya ndege nchini. Tumekarabati Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere ambao umeongeza uwezo wa kuhudumia
kutoka ndege 7 hadi 30 hivi sasa. Aidha tunajenga jengo la tatu la
abiria kwenye uwanja huo lenye uwezo wa kuhudumia abiria milioni 3.5.
Ujenzi huo unategemewa kukamilika mwezi Oktoba mwaka huu. Kukamilika
kwake kutauwezesha uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere kuhudumia
abiria milioni 6 na ndege nyingi zikiwemo ndege kubwa za kisasa za
Airbus 380.
Mheshimiwa Spika;
Vile
vile, tumeufanyia ukarabati na upanuzi Uwanja wa Kimataifa wa
Kilimanjaro ambao ni muhimu sana kwa sekta ya utalii ya ukanda wa
kaskazini. Uwanja mpya wa ndege wa Songwe kule Mbeya umekamilika na hivi
sasa unatumika. Hali kadhalika, tumeviboresha upya viwanja vya ndege
vya Arusha, Mafia, Mpanda, Kigoma, Tabora, Mwanza na Bukoba.
Ujenzi,
upanuzi na ukarabati huu tulioufanya, umechangia sana katika ongezeko
kubwa la safari za ndege na abiria nchini. Safari za ndege kuja nchini
zimeongezeka toka safari 78 mwaka 2005 zilizokuwa zinatolewa na kampuni
29 za usafiri wa ndege hadi safari 175 zinazotolewa na kampuni 55 mwaka
2014. Aidha, abiria wanaoondoka na kuwasili katika viwanja vya ndege
wameongezeka kutoka 2,172,519 mwaka 2005 hadi abiria 4,670,380 mwaka
2013. Siku hizi Watanzania wanaopanda ndege wanaongezeka kwa kasi kubwa.
Mheshimiwa Spika;
Jambo
ambalo hatukuweza kufanikiwa ni lile la kufufua Shirika letu la Ndege.
Tumefanikiwa kulifanya lisife lakini hatukuweza kulihuisha lirejee hata
kwenye ile hali yake ya zamani. Hata hivyo, fikra na mawazo kuhusu
mkakati wa kulijenga upya shirika hilo yapo. Kwa sasa Menejimenti
imepewa jukumu la kuandaa mpango wa biashara unaoeleweka na
unaokopesheka, kisha Serikali itaona namna ya kulisaidia shirika.
Utabiri wa Hali ya Hewa
Mheshimiwa Spika;
Sambamba
na hayo, tumeboresha huduma za utabiri wa hali ya hewa. Mamlaka ya Hali
ya Hewa imepatiwa vifaa vipya ambavyo vimeongeza ufanisi na usahihi wa
utabiri unaotolewa. Mwezi Februari 2014 Mamlaka hiyo ilipata cheti cha
utoaji wa huduma bora cha ISO na hivyo kuufanya taarifa zake kutambuliwa
kimataifa.
Mawasiliano
Mheshimiwa Spika;
Tumepiga
hatua kubwa katika sekta ya teknolojia ya habari na mawasiliano.
Tumejenga Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano wenye urefu wa kilometa 7,560
unaounganisha miji mikuu ya mikoa yote ya Tanzania Bara isipokuwa mkoa
mpya wa Simiyu. Kwa Mikoa ya Unguja na Pemba, ujenzi wake utakamilika
mwezi ujao. Katika Awamu ya Pili, Mkoa wa Simiyu na wilaya zote nchini
zitaunganishwa.
Ujenzi wa
mkongo huu umechangia katika kuongeza ubora na kasi ya mawasiliano, na
kushusha gharama za mawasiliano. Kwa mfano, gharama za kupiga simu
zimeshuka kutoka shilingi 115 kwa dakika mwaka 2005 hadi shilingi 34.92
mwaka 2014 na gharama za intaneti zimeshuka kutoka wastani wa shilingi
36,000 kwa Gigabyte moja mwaka 2005 hadi wastani wa shilingi 9,000 kwa
Gigabyte moja (GB 1) mwaka 2014. Hii imeshusha pia gharama za biashara
kwa kurahisisha mawasiliano na malipo kati ya mabenki na kwa njia ya
mtandao na simu.
Kwa
upande wa laini za simu, zimeongezeka kutoka laini milioni 2.96 mwaka
2005 hadi milioni 28 mwaka 2014. Watu wanaotumia intaneti wameongezeka
toka milioni 1.6 hadi milioni 9.3 mwaka 2014. Kukua kwa mawasilino ya
simu kumewezesha watumiaji milioni 12.3 kupata huduma ya fedha kupitia
simu za mkononi. Kati ya Julai 2013 na Aprili 2014 jumla ya miamala
milioni 972.6 ilifanyika yenye thamani ya shilingi trilioni 28. Huu ni
wastani wa zaidi ya shilingi trilioni 2 kwa mwezi na kufanya Tanzania
kuongoza duniani kwa huduma hii.
Mheshimiwa Spika;
Tulitambua
kuwa makampuni binafsi ya simu hayapendi kuwekeza vijijini ambako
biashara si kubwa kama mijini. Kwa kutambua umuhimu wa huduma ya
mawasiliano kwa maendeleo, Serikali iliamua ibebe mzigo huo. Kwa sababu
hiyo tumeanzisha Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) ambao utawezesha
kata na vijiji vyote nchini kufikiwa na huduma za mawasiliano. Mfuko huo
umekwisha wezesha jumla ya kata 52 na vijiji 314 kufikiwa na huduma
hizo. Upelekaji wa huduma za mawasiliano kupitia Mfuko huo zinaendelea
kwa kata nyingine 163 zenye vijiji 922, ambapo wananchi milioni 1.2
watanufaika.
Mheshimiwa Spika;
Tumechukua
hatua ya kuhakikisha kuwa mianya ya kodi inazibwa na kwamba makampuni
yanalipa kodi stahiki kwa kununua na kufunga mtambo wa Kusimamia
Mawasiliano ya simu nchini. Mtambo huo unaowezesha Mamlaka ya
Mawasiliano (TCRA) kukusanya takwimu halisi za mawasiliano yanayofanywa.
Tangu kuanza kutumika kwa mtambo huo, mwaka jana Serikali imeweza
kukusanya shilingi bilioni 24.6 ambazo vinginevyo zisingepatikana.
Aidha, tumekuwa nchi ya kwanza Afrika ya Mashariki kuhama kutoka mfumo
wa analojia kwenda digitali. Karibu tutakamilisha kwa mikoa yote.
Tunazipokea nchi kadhaa zinazokuja kujifunza kwetu juu ya uendeshaji wa
zoezi hili.
Ardhi na Makazi
Mheshimiwa Spika;
Maisha
bora kwa kila Mtanzania ni pamoja na kuboresha makazi ya watu. Sote
tunafahamu kuwa makazi ni hitajio la msingi la binadamu. Lengo letu la
kuboresha huduma za ardhi, nyumba na makazi limepata mafanikio makubwa.
Tumepeleka huduma za utawala wa ardhi karibu zaidi na wananchi kwa
kuanzisha Kanda nane za kusimamia upangaji, upimaji na utoaji
hatimiliki. Uamuzi huu umepunguza lile tatizo la watu kuchelewa kupata
hati miliki. Toka 2006 hadi sasa jumla ya hati 164,275 zimetolewa,
vijiji 10,500 vimepimwa na kati yake vijiji 10,341 vimepatiwa
hatimiliki.
Mheshimiwa Spika;
Tumetunga
Sheria kwa ajili ya kuwezesha upatatikanaji wa mikopo ya ujenzi na
ununuzi wa nyumba. Sheria hizo ni pamoja na Sheria ya Mikopo ya Nyumba
(Mortage Finance) na Sheria ya Kutambua Milki ya Sehemu ya jengo haswa
kwenye maghorofa (Unit Tittles Act) ya mwaka 2008. Sheria hizi kwa
ujumla wake zimewezesha watu wengi zaidi kupata mikopo ya kujenga au
kukarabati nyumba zao na kuwawezesha watu kupata umiliki wa sehemu ya
jengo.
Mabadiliko
hayo pia yamewezesha sekta ya nyumba kukua kwa kasi kubwa na majengo na
nyumba za kisasa kujengwa katika kipindi cha miaka 10 hii. Dar es
Salaam ya leo na ile ya 2005 ni tofauti kabisa. Shirika la Nyumba la
Taifa, Wakala wa Nyumba za Serikali, Mifuko ya Hifadhi ya Jamii nayo
imefanya uwekezaji mkubwa sana katika ujenzi wa nyumba katika kipindi
hiki.
Mheshimiwa Spika;
Kwa
upande wa watumishi wa serikali kuwa na nyumba mwaka 2008 tulianzisha
Mfuko wa Mkopo kwa watumishi wa umma ambao hadi sasa umetoa mikopo ya
shilingi bilioni 5.4 kwa watumishi 1,169. Pia, tumeanzisha Kampuni ya
Mikopo ya Nyumba kwa ajili ya watumishi wa umma ambayo tayari imeanza
kazi.
Mheshimiwa Spika;
Ninayo
furaha kueleza kuwa makazi ya wananchi pia yameendelea kuwa bora.
Takwimu za Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2012, inaonyesha kuwa idadi
ya nyumba zilizoezekwa kwa bati zimeongezeka kutoka asilimia 46 mwaka
2002 hadi asilimia 65 mwaka 2012. Kwa lugha nyingine nyumba zilizoezekwa
makuti na nyasi zimezidi kupungua. Haya ni mafanikio makubwa ya kutia
moyo na hatua muhimu katika kuboresha maisha ya Watanzania.
Utafiti
Mheshimiwa Spika;
Jambo
lingine ambalo tumeliwekea msingi mzuri ni eneo la utafiti. Hili ndilo
eneo ambalo ilitalivusha taifa letu kwenda katika maendeleo makubwa
zaidi. Niliamua Serikali ichukue hatua za makusudi za kufufua shughuli
za utafiti ambazo zilikuwa zinapita katika kipindi kigumu. Niliamua kuwa
Serikali ianze safari ya kutenga fedha za kutosha kwa ajili ya utafiti.
Tulianza na shilingi bilioni 10 na kuendelea kuongeza mwaka hadi mwaka
na kufika shilingi bilioni 60 mwaka 2014, katika kipindi cha kujitahidi
kufikia asilimia 1 ya bajeti ya Serikali na hatimaye asilimia 1 ya pato
la Taifa kwa ajili ya shughuli za utafiti.
Mheshimiwa Spika;
Kwa
kutumia kiasi hiki kidogo kilichopo wanasayansi wetu 344 wamepata
ufadhili wa masomo ya shahada ya Uzamili na 173 wa shahada ya Uzamivu.
Miradi 70 ya utafiti imefadhiliwa, kati ya hiyo 22 ni ya kilimo. Fedha
hizi pia zimewezesha Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia kuanzisha
viatamizi vya teknohama ambavyo vimewezesha vijana wetu kubuni na
kuvumbua teknolojia zenye manufaa kwa maendeleo ya jamii na taifa.
Wamezalisha ajira na kunufaisha watu wengi. Kampuni ya Max Malipo ni
mfano mmojawapo mzuri wa matokeo mazuri ya viatamizi hivi.
Huduma za Jamii
Elimu
Mheshimiwa Spika;
Katika
hotuba yangu ya kuzindua Bunge la Tisa mwaka 2005 nilisema kuwa, “Hakuna
Taifa lililopata maendeleo bila kuendeleza elimu. Hivyo kuendeleza
elimu nchini itakuwa agenda muhimu ya Serikali ya Awamu ya Nne”.
Tumetimiza ahadi. Katika kipindi chote cha miaka kumi bajeti ya sekta ya
elimu ndiyo iliyokuwa kubwa kuliko za sekta nyingine zote. Mwaka huu
2015 bajeti ya elimu imefikia shilingi trilioni 3.4 ikilinganishwa na
shilingi bilioni 669.5 za mwaka 2005.
Mafanikio
yaliyopatikana katika sekta ya elimu ndani ya miaka 10 hii ni ya kutia
moyo. Tumeongeza shule za msingi kutoka 14,257 mwaka 2005 hadi 16,538
mwaka 2015 na wanafunzi wameongezeka kutoka 7,541,208 hadi 8,202,892.
Upanuzi huu umewezesha asilimia 98 ya watoto wanostahili kupata elimu ya
msingi sasa kuandikishwa.
Kwa
kushirikiana na wananchi na sekta binafsi tumeongeza Shule za Sekondari
kutoka Shule 1,745 mwaka 2005 hadi Shule 4,753 mwaka 2015. Idadi ya
wanafunzi imeongezeka kutoka 524,325 mwaka 2005 hadi 1,804,056 mwaka
2015. Katika kipindi hiki pia vyuo vya Ufundi vimeongezeka kutoka 184
mwaka 2005 hadi 744 mwaka 2015 na wanafunzi katika vyuo hivyo
wameongezeka kutoka 40,059 hadi 145,511 mwaka 2015. Haya ni mafanikio
makubwa sana.
Kwa nia
ya kuongeza ubora wa elimu, tumechukua hatua thabiti za kukabiliana na
tatizo la uhaba wa walimu, vitabu, maabara za sayansi na vifaa vya
kujifunzia na kufundishia. Tumepanua mafunzo ya ualimu wa Cheti,
Stashahada na Shahada. Hii imetuwezesha kuongeza idadi ya walimu wa
Shule za Msingi kutoka 135,013 mwaka 2005 hadi 202,752 mwaka 2015, na
walimu wa Shule za Sekondari kutoka 18,754 mwaka 2005 hadi 88,908 mwaka
2015. Uhaba wa walimu wa masomo ya sanaa si tatizo tena, tunao wa
kutosha. Tuna upungufu wa walimu 20,141 wa masomo wa sayansi na
hisabati. Ninaamini, hata hivyo, kwa programu za kusomesha walimu wa
sayansi vyuoni zilizopo, katika miaka michache ijayo tatizo hili nalo
tutalipatia ufumbuzi. Kwa mfano, Chuo Kikuu cha Dodoma, mwaka 2014
kimeanza kudahili wanafunzi 5,000 wa ualimu wa masomo ya sayansi.
Mheshimiwa Spika;
Kwa
upande wa maabara za sayansi, katika shule za sekondari za kata tayari
maabara 5,979 zimejengwa na nyingine 4,410 ziko katika hatua mbalimbali
za ukamilishaji. Hivi sasa tunashughulikia upatikanaji na usambazaji wa
vifaa kwa matumizi ya maabara hizo. Kwa upande wa vitabu tumeweza
kuboresha upatikanaji wake kwa mwanafunzi wa Shule za Msingi kutoka
uwiano wa 1:5 mwaka 2005 hadi 1:3 mwaka 2015. Katika shule za sekondari
uwiano ni 1:2 ukilinganisha na 1:8 mwaka 2005.
Mheshimiwa Spika;
Katika
kipindi hiki pia tumeshuhudia upanuzi mkubwa wa elimu ya juu nchini.
Idadi ya vyuo vikuu imeongezeka kutoka vyuo 26 mwaka 2005 hadi 52 mwaka
2015. Miongoni mwa vyuo hivyo ni Chuo Kikuu cha Dodoma na cha Nelson
Mandela cha Arusha ambavyo vimejengwa na Serikali ya Awamu ya Nne. Vyuo
hivi ni fahari ya nchi yetu kwani tumevijenga kwa fedha zetu wenyewe
bila msaada kutoka kwa wafadhili. Ongezeko la vyuo vikuu limefanya idadi
ya wanafunzi kuongezeka kutoka wanafunzi 40,719 mwaka 2005 hadi 218,959
mwaka 2014. Idadi ya wanafunzi wanaonufaika na mikopo nayo imeongezeka
kutoka wanafunzi 16,345 mwaka 2005 hadi wanafunzi 99,590 mwaka huu.
Afya
Mheshimiwa Spika;
Tumepata
mafanikio ya kutia moyo kwa upande wa kuboresha na kupanua huduma ya
afya nchini. Tuliazimia kusogeza huduma ya afya karibu na wanapoishi
watu kwa kujenga vituo vya kutoa huduma ya afya vipya na kuimarisha
vilivyopo. Kati ya mwaka 2005 na 2014 vituo vya kutolea huduma za afya
2,175 vimejengwa. Kati yake hospitali 19, vituo vya afya 168 na zahanati
1,883 zimejengwa.
Tumeimarisha
hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Hospitali za Rufaa za Kanda, Mikoa na
Wilaya kwa kuzipatia vifaa vya tiba na uchunguzi (MRI, CT Scan, X ray,
Ultra Sounds, Maabara n.k). Tumejenga maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii
ambayo inatumika kama maabara ya Kimataifa ya Rufaa kwa nchi za SADC.
Tumeimarisha maabara za mikoa kwa majengo na vifaa vya kisasa vya
uchunguzi wa magonjwa. Maabara yetu ya Mbeya sasa ina uwezo wa kubaini
virusi vya Ebola jambo ambalo miezi michache iliyopita tulikuwa
tunapeleka sampuli Nairobi. Hivi sasa hospitali za wilaya zinaweza
kufanya uchunguzi wa mwenendo wa figo na ini.
Mheshimiwa Spika;
Tumeboresha
huduma ya Afya ya Kinywa katika Hospitali ya Muhimbili kwa kufunga
mashine 26 za kisasa za tiba ya meno na maabara ya kisasa ya kutengeneza
meno bandia. Pia tumeimarisha huduma ya afya ya kinywa kwa kuweka vifaa
vya tiba ya meno kwenye Halmashuri 91. Hivi sasa hospitali 136, vituo
vya afya 63 na zahanati 3 zinatoa huduma hiyo nchini.
Tumeanza
kupata mafanikio katika dhamira yetu ya kujenga uwezo wetu wa ndani wa
kuchunguza na kutibu maradhi ya figo, moyo, saratani na mishipa ya
fahamu ambayo tumekuwa tunapeleka wagonjwa wengi nje. Kwa mfano, tangu
Taasisi ya Moyo ianze kutoa huduma pale Muhimbili wagonjwa 71,963
wamepatiwa matibabu wakiwemo 692 waliofanyiwa upasuaji. Watu hao
wangepelekwa nje taifa lingelipa pesa nyingi. Uwezo wetu utaongezeka
sana hospitali ya Mloganzila itakapokamilika.
Mheshimiwa Spika;
Tumebadilisha
utaratibu wa kusambaza dawa kutoka Bohari ya Dawa. Tumeongeza bajeti ya
dawa na vifaa tiba kutoka shilingi bilioni 40.6 mwaka 2005 hadi
shilingi bilioni 147 mwaka 2014. Idadi ya watu wanaonufaika na Mfuko wa
Afya ya Jamii na Mfuko wa Bima ya Afya wameongezeka kutoka asilimia 3
mwaka 2005 hadi asilimia 19 mwaka 2014.
Katika
kipindi hiki tumetoa msukumo mkubwa katika kupambana na maradhi makubwa
ya kuambukiza yanayosababisha vifo vya watu wengi. Tumeendesha kampeni
ya kupambana na malaria nchi nzima kwa kubadilisha dawa ya kutibu
malaria na kugawa vyandarua 26,371329 kwa watoto chini ya miaka mitano,
kwa akina mama wajawazito na katika kila kaya. Aidha, tumepulizia dawa
ya kuua mbu ndani ya nyumba katika mikoa ya kanda ya ziwa. Matokeo ya
jitihada hizo ni kupungua kwa maambukizi ya malaria kwa asilimia 51 na
vifo kwa asilimia 71. Baada ya kiwanda cha kuzalisha dawa ya kuua
viluwiluwi vya mbu pale Kibaha kuanza uzalishaji, safari ya kutokomeza
malaria hapa nchini ni ya uhakika.
Mheshimiwa Spika;
Juhudi
zetu katika kupambana na ukimwi zimewezesha kushuka kwa maambukizi ya
ukimwi kutoka asilimia 7.7 mwaka 2005 hadi asilimia 5.1 mwaka 2012.
Idadi ya watu waliopima virusi vya ukimwi imeongezeka kutoka 365,189
mwaka 2005 hadi 25,468,564 mwaka 2014. Aidha, tumewezesha vituo 5,244 na
asilimia 97 ya vituo vyote vinavyotoa huduma ya uzazi kutoa huduma ya
kuzia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.
Mheshimiwa Spika;
Kati ya
mwaka 2005 na 2014 tumeongeza udahili wa wanafunzi katika vyuo vya afya
kutoka 3,025 mwaka 2005 hadi 11,807 mwaka 2014. Katika kipindi hicho
wataalamu wa afya 55,608 wameajiriwa. Aidha, tumeongeza ajira ya kada
mbalimbali za afya. Kwa sababu hiyo idadi ya madaktari imeongezeka
kutoka madaktari 1,048 mwaka 2006 hadi madaktari 2,325 mwaka 2014.
Halikadhalika, madaktari wasaidizi wameongezeka kutoka 1,223 hadi 1,914,
wauguzi kutoka 15,961 hadi 22,942 wataalamu wa Maabara kutoka 1,277
hadi 2,378 mwaka 2014. Hivi sasa uwiano wa Daktari kwa wagonjwa ni
1:6,666 ikilinganishwa na 1:35,714 mwaka 2005. Na, uwiano wa Muuguzi kwa
wagonjwa umeshuka kutoka 1:2,347 mwaka 2005 hadi 1:2,008 mwaka huu.
Mheshimiwa Spika;
Tumeendesha
kampeni ya kuboresha lishe nchini na kutekeleza Mkakati wa Taifa wa
Lishe (2011-2016). Kwa ajili hiyo mwaka 2013 tulizindua Programu ya
Uongezaji wa Virutubishi. Matokeo ya jitihada zetu hizo yameanza
kuonekana. Udumavu umepungua toka asilimia 44 mwaka 2005 hadi asilimia
35 mwaka 2014 na uzito pungufu toka asilimia 17 hadi asilimia 13.
Kwa jumla
juhudi zetu za kuboresha huduma ya afya zimezaa matunda ya kuridhisha.
Wastani wa umri wa kuishi wa Mtanzania umeongezeka toka miaka 49 mwaka
2005 hadi miaka 62 hivi sasa. Vifo vya watoto wachanga vimepungua toka
vifo 68 kwa kila vizazi hai 1000 hadi vifo 21 kwa kila vizazi hai 1,000
mwaka 2014. Vifo vya watoto chini ya miaka mitano vimepungua kutoka vifo
112 kwa kila vizazi hai 1000 mwaka 2005 hadi vifo 54 kwa kila vizazi
hai 1000 mwaka 2014, na vifo vya akinamama wajawazito vimepungua toka
vifo 578 kwa vizazi hai 100,000 hadi vifo 432 kwa vizazi hai 100,000
mwaka 2012. Haya ni mafanikio ya kutia moyo ingawaje bado tunatakiwa
kuendeleza juhudi zaidi mara dufu ili vifo vipungue zaidi na zaidi.
Maji
Mheshimiwa Spika;
Serikali
ya Awamu ya Nne imefanya juhudi kubwa katika kuboresha huduma ya
upatikanaji wa maji safi na salama na usafi wa mazingira katika kipindi
hiki. Tumekamilisha miradi ya maji katika miji mikuu ya mikoa 8, Wilaya 6
na Miji midogo 2. Aidha, miradi katika miji mingine 13 ya mikoa, 27 ya
Wilaya na Miji midogo inaendelea kutekelezwa. Utekelezaji wa miradi hii
umewezesha kiwango cha upatikanaji maji mijini kufikia wastani wa
asilimia 86 kwa mwaka 2014 kutoka asilimia 73 mwaka 2005. Na kwa
Vijijini imefikia asilimia 67.6 Mwaka 2014 ukilinganisha na asilimia 53
mwaka 2005. Tumevuka lengo letu la kuwapatia maji asilimia 65 ya wakazi
wa vijijini.
Aidha,
miradi inayoendelea kutekelezwa hivi sasa itakapokamilika katika mwaka
huu wa fedha upatikanaji wa maji mijini utafikia asilimia 90 ambalo
ndilo lengo la Ilani ya uchaguzi ya CCM. Vijijini inaweza kufikia
asilimia 70 ambayo ni juu ya lengo la asilimia 65.
Aidha,
tumeboresha huduma za uondoaji wa maji taka katika miji ya Tanga,
Dodoma, Mwanza, Mbeya, Iringa, Songea, Tabora na Morogoro. Uboreshaji
huu wa huduma za utoaji wa maji taka ni mwanzo mzuri katika kuhakikisha
kwamba tunakuwa na mipango mizuri ya maji taka mijini.
Uwezeshaji wa Wananchi
Mheshimiwa Spika;
Uwezeshaji
wa wananchi kiuchumi ilikuwa ni moja ya dhima kuu ya Ilani ya Uchaguzi
ya CCM ya mwaka 2005. Katika kutekeleza dhamira hii, Serikali
imeendeleza kwa mafanikio makubwa mifuko ya kutoa mikopo kwa vijana,
wanawake, wajasiriamali wadogo na kuanzisha fursa nyingine mpya. Watu
wengi wamenufaika na wao wenyewe kuwa chachu ya kuzalisha ajira,
kupunguza umasikini na kuinua hali za maisha ya watu walioguswa na fursa
zilizopatikana.
Tumeiwezesha
Benki ya Wanawake kuanza na kuendelea kutoa huduma. Kama mjuavyo
niliamua Serikali ichangie mtaji wa mwanzo na inaendelea kuchangia mtaji
huo. Tayari Benki hiyo imeshakopesha watu 125,000 na kati yao wanawake
ni asilimia 82. Hali kadhalika, nilifanya uamuzi wa makusudi wa kuifufua
Benki ya Rasilimali (TIB). Dhamira yangu ni kutaka iwepo Benki ya
maendeleo itakayotoa mikopo ya muda mrefu na wa kati kwa wawekezaji
wazawa. Hii itawezesha kuanzisha na kuendesha shughuli za viwanda,
madini, utalii na biashara kwa urahisi.
Tumeiwezesha
Benki ya Rasilimali kwa mtaji, rasilimali watu na vitendea kazi na
kuifanya iwe moja ya benki ya kutumainiwa nchini. TIB imeshatoa mikopo
kwa makampuni 365 yenye thamani ya shilingi bilioni 512. Aidha, imetoa
mikopo kwa miradi 201 yenye thamani ya shilingi bilioni 156 kupitia
dirisha dogo la kilimo. Natoa pongezi maalum kwa viongozi na watumishi
wa Benki ya Rasilimali kwa kazi kubwa na nzuri waliyofanya katika
kipindi hiki kifupi. Naomba waendelee na moyo huo kwa maslahi ya nchi
yetu.
Mheshimiwa Spika;
Tumetimiza
ahadi yetu ya kuimarisha ushirika nchini kama nguzo kuu ya kuunganisha
nguvu za wanyonge kujiletea maendeleo. Katika kipindi hiki, idadi ya
Vyama vya Ushirika vya aina mbalimbali nchini imeongezeka kutoka 5,832
mwaka 2005 hadi 9,604 mwaka 2015.
Kwa
upande mwingine, Vyama vya Akiba na Mikopo (SACCOS), vimeongezeka zaidi
ya mara tatu kutoka vyama 1,875 mwaka 2005 hadi 5,559 mwaka 2014. Akiba,
hisa na amana za wanachama zimeongezeka kwa zaidi ya mara tano kutoka
Shilingi bilioni 85.6 mwaka 2005/2016 hadi Shilingi 463 bilioni mwaka
2014 na mikopo kwa wanachama imekua mara 13 toka shilingi bilioni 65.7
hadi shilingi bilioni 893 mwaka huu. Kwa hakika haya ni mafanikio
makubwa ya kujivunia. Watu wengi wamewezeshwa kupunguza umasikini wao na
wengine kuondoka katika lindi la umasikini.
Sanaa na Michezo
Mheshimiwa Spika;
Niliahidi
kusaidia kukuza michezo na sanaa nchini. Kwa upande wa michezo
niliahidi kuwa Serikali italipia makocha. Nilitimiza ahadi yangu kwa
michezo ya soka, netiboli na ngumi. Kwa upande wa riadha tuliwapeleka
wanariadha wetu China, Ethiopia na New Zealand kwa maandalizi ya
mashindano ya kimataifa. Timu yetu ya taifa ya soka haijafanya vizuri
sana. Kwa upande wa soka tulianza kupata matumaini lakini baadae
yakafifia. Timu yetu ya taifa ya soka haijafanya vizuri sana pamoja na
kubadili makocha. Hata vilabu vyetu pia havifanyi vizuri. Kwa kweli
lazima Watanzania tukae chini na kujiuliza kwa nini hatufanyi vizuri na
tufanye nini tufanikiwe.
Mheshimiwa Spika;
Nilifanya
uamuzi wa kurejesha michezo mashuleni pamoja na mashindano ya michezo
kwa shule za msingi na sekondari (UMISHUMTA na UMISETA). Nia yetu ni
kutaka vipaji vya michezo vya vijana viibuliwe wakiwa bado wadogo na
kuendelezwa. Uamuzi huu umerejesha uhai na matumaini kwamba siku za
usoni tutaona matunda yake.
Kwa
dhamira hiyo hiyo, kwa kushirikiana na Kampuni ya Symbion Power na Klabu
ya Soka ya Sunderland kituo cha kuandaa wanamichezo wadogo kinajengwa
pale Kidongo Chekundu, Dar es Salaam. Kituo hiki kinatarajiwa kuwa
tayari ifikapo mwezi Septemba, 2015. Kikitumiwa vizuri huenda ikawa
ndiyo mwanzo wa safari ya uhakika ya kuendeleza soka hapa nchini.
Tukifanikiwa Kidongo Chekundu, vituo vingine kama hivyo vinaweza
kuanzishwa sehemu nyingine nchini na wadau mbalimbali.
Mheshimiwa Spika;
Tumepata
mafanikio ya kuridhisha kwa upande wa sanaa za filamu na muziki. Vijana
wetu wa tasnia hizi wamekuwa wanafanya vizuri kiasi kwamba leo hii Bongo
Flavor na Bongo Movie zimevuka mipaka ya Tanzania. Zinaitangaza sanaa
ya Tanzania, lugha ya Kiswahili pamoja na nchi yetu. Vijana hawa
wameitoa kimasomaso Tanzania na kutufutia unyonge tunaopata kwenye
michezo. Tasnia hizi zimeajiri vijana wengi, wanalipa kodi na wanasaidia
sana katika kuhamasisha na kufikisha ujumbe kwa mambo muhimu katika
jamii.
Mheshimiwa Spika;
Kwa nia
ya kutaka kuendeleza ujuzi, mbinu na maarifa kwa wasanii wetu mwaka wa
jana niligharimia timu ya watu wazoefu wa fani za muziki na filamu
kutoka Marekani kuja nchini kutoa mafunzo ya muda mfupi. Ninafanya
mipango waje tena kwani mafunzo ya mara kwa mara yatawaimarisha wasanii
wetu.
Kwa
wasanii wa muziki niliwatimizia maombi yao ya kutaka kuwa na mastering
studio. Kwa wote nimefanya jitihada kubwa ya kutafuta majawabu kwa
tatizo sugu la kupata malipo ya haki kwa kazi wazifanyazo. Tumetunga
Kanuni ambazo zimewezesha kazi za wasanii kutambuliwa na kulindwa.
Halikadhalika, tumeweza kuanza utaratibu mpya wa kusambaza kazi za
wasanii ambapo wao wenyewe wana sauti nazo. Nitajitahidi katika kipindi
kifupi kilichobaki niyasukume kwa kasi masuala yaliyosalia ili niwaache
wasanii wetu mahali pazuri. Nataka wapate malipo ya haki kwa vipaji vyao
na jasho lao ili wainue hali zao za maisha.
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
Mheshimiwa Spika;
Wakati
nalihutubia Bunge la Tisa tarehe 30 Desemba 2005 niliahidi kwamba
Serikali itafanya kila iwezalo kuhakikisha Tanzania inakuwa na uhusiano
mzuri na mataifa mengine duniani, na mashirika ya kimataifa na kikanda.
Leo, miaka 10 baadae napenda kuwahakikishia kuwa ahadi yetu
tumeitekeleza, tena vizuri kuliko tulivyotegemea. Tanzania ni rafiki wa
kila nchi na kila shirika la kanda na kimataifa. Hadhi yetu katika uso
wa kimataifa imepanda sana. Tunaheshimiwa, tunasikilizwa, tunathaminiwa
na kuaminiwa na mataifa makubwa na madogo.
Katika
kipindi hiki tumetembelewa na wageni wengi mashuhuri kutoka mabara yote.
Tumeweka historia kwa kutembelewa mfululizo na Marais wawili wa
Marekani yaani Rais George W. Bush mwaka 2008 na Rais Barack Obama mwaka
2013, na Marais wawili wa China Rais Hu Jintao mwaka 2009 na Rais Xi
Jinping mwaka 2013. Pia tulitembelewa na Wafalme, Marais, Mawaziri Wakuu
na Mawaziri kutoka nchi za Mabara yote duniani. Aidha, tumetembelewa na
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Rais wa Umoja wa Ulaya, Rais wa Benki
ya Dunia n.k.
Tumeshirikishwa
katika shughuli nyingi na mikutano mingi. Nimepata fursa ya kushiriki
katika mikutano mbalimbali ya kimataifa pamoja na miwili ya G8
kuwakilisha Afrika. Nimewahi kushiriki na kupewa dhamana ya uongozi
katika kamati na Tume kadhaa za Afrika na dunia. Nimewahi kuwa
Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (2008), Mwenyekiti wa Kamati ya Wakuu wa
Nchi za Afrika kuhusu Mabadiliko ya Tabia Nchi, Mjumbe wa Danish Africa
Commission, Mwenyekiti wa ALMA. Hivi karibuni nimeteuliwa kuwa
Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Mataifa Kupendekeza Namna Bora kwa Dunia
Kushughulikia Majanga ya Afya.
Mheshimiwa Spika;
Katika
kipindi hiki tumefungua Balozi mpya 5 katika nchi za Oman, Malaysia,
Brazil, Uholanzi na Comoro. Hii inafikisha idadi ya Balozi zetu kuwa 35.
Pamoja na ufinyu wa bajeti jitihada zimekuwa zinafanyika kuboresha
huduma kwa Balozi zetu na wanadiplomasia wetu. Tumejenga jengo la
Ubalozi New Delhi na kununua majengo ya ofisi ya kitega uchumi
Washington DC, New York na Ufaransa. Tumeanzisha Kurugenzi ya Diaspora
katika Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ili
kuwashirikisha Watanzania waishio ughaibuni katika maendeleo ya nchi
yetu.
Ushirikiano wa Kanda
Mheshimiwa Spika;
Tanzania
imeendelea kuwa mwanachama mwaminifu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki,
SADC, Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa. Tumepiga hatua kubwa katika
kuimarisha na kuendeleza utengamano wa Afrika Mashariki. Katika miaka 10
hii tumefanikiwa kukamilisha utekelezaji wa Umoja wa Forodha tarehe 1
Januari, 2010 na tarehe 1 Julai, 2010 tulianza utekelezaji wa Soko la
Pamoja ambao unaendelea hivi sasa. Tumetia saini Itifaki ya Umoja wa
Sarafu Novemba 2013 ambayo utekelezaji wake unaendelea vizuri. Matunda
ya utekelezaji wa utengamano kiuchumi yameanza kuonekana. Kwa mfano,
mauzo yetu katika soko la Afrika Mashariki yameongezeka kutoka bidhaa
zenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 161 mwaka 2005 hadi bidhaa
za Dola za Marekani bilioni 1.2 mwaka 2014. Uwekezaji nchini Tanzania
kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki umeongezeka toka
miradi 35 yenye thamani ya Dola za Marekani milioni 39.5 hadi miradi
244 yenye thamani ya Dola za Marekani milion 676.5. Haya yote ni
mafanikio makubwa.
Mheshimiwa Spika;
Kuhusu
Umoja wa Maendeleo wa Nchi za Kusini Mwa Afrika (SADC). Tumeendelea
kushiriki kwa ukamilifu katika shughuli za umoja huo. Tumeshiriki kwenye
kutafuta suluhisho la Visiwa vya Comoro, Madagascar, Zimbabwe na DRC.
Salamu za Kuaga
Mheshimiwa Spika;
Tulipanga
kufanya mengi na tumefanikiwa mengi, lakini hatukuweza kuyamaliza yote
kwa sababu ya changamoto mbalimbali na kubwa zaidi ni uhaba wa
rasilimali fedha na wakati mwingine rasilimali watu na vitendea kazi.
Hata hivyo tumeweza kutekeleza zaidi ya asilimia 88 ya ahadi zetu
zilizomo kwenye Ilani za Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi na mipango ya
Serikali.
Siku moja
nikiwa Marekani mwandishi mmoja wa habari aliniuliza, je, utakapomaliza
uongozi wako utapenda Watanzania wakukumbuke kwa lipi? Nikamjibu,
nitapenda Watanzania waseme, “Rais Kikwete alitukuta kuleee! na sasa
anatuacha hapa palipo juu”. Mimi na ninyi ni mashahidi kuwa tulipo leo
ni bora zaidi ya kule tulipokuwa jana.
Changamoto
za nchi haziishi kila siku zinaibuka mpya. Kila ukimaliza moja inazaa
changamoto nyingine. Hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa baba wa taifa ambaye
naye hakumaliza changamoto zote, ndivyo ilivyokuwa kwa Mzee Mwinyi na
hivyo ndivyo alivyoniachia Rais Mkapa. Nami namwachia anayekuja, naye
afanye yake na yatakayobakia atamwachia atakayemfuatia. Jambo linalonipa
faraja ni kuwa nami nimetoa mchango wangu kwa maendeleo ya nchi yetu na
watu wake
Shukrani
Mheshimiwa Spika;
Nitakuwa
mchoyo wa fadhila nisipokushukuru Mheshimiwa Makamu wa Rais, Dkt.
Mohamed Ghalib Bilal kwa msaada wako, ushauri wako na ushirikiano wa
karibu ulionipatia katika kipindi hiki cha miaka 5. Nakutakia kila la
heri katika maisha yako baada ya mimi na wewe kumaliza kipindi chetu cha
uongozi. Namshukuru Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein, ambaye pia alikuwa Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano katika kipindi changu cha kwanza.
Nakushukuru kwa ushirikiano wako mkubwa, msaada wako na ushauri wako wa
hekima na busara ambao umewezesha mafanikio tuliyoyapata katika kujenga
nchi yetu na katika kuimarisha muungano wetu.
Kwa namna
ya pekee namshukuru Mheshimiwa Mizengo Kayanza Pinda, Waziri Mkuu na
Kiongozi wa Serikali Bungeni kwa kazi nzuri na ya kutukuka uliyoifanya
katika kipindi cha miaka 8. Umepita katika misukosuko mingi, na wakati
mwingine umebebeshwa lawama isiyokuwa yako. Daima umeonyesha ukomavu,
uimara na kutotetereka. Napenda pia kumtambua Mheshimiwa Edward Lowassa
ambaye katika kipindi kifupi alichokuwa Waziri Mkuu alifanya kazi kubwa
na nzuri.
Nawashukuru
pia Mawaziri, Katibu Mkuu Kiongozi, Makatibu Wakuu, Wakuu wa Mikoa,
Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi, Watendaji na watumishi wote wa Serikali
Kuu na Serikali za Mitaa kwa mchango wao katika kufanikisha majukumu ya
Awamu ya Nne. Mmenisaidia sana. Kwa kweli mafanikio haya tunayozungumza
leo yameletwa na juhudi zenu.
Nawashukuru
viongozi wa dini, asasi za kiraia na vyombo vya habari kwa kuniunga
mkono mimi na Serikali yangu na kwa mchango wenu muhimu. Nawaomba
muendelee kuilea amani ya nchi yetu na watu wake.
Nakishukuru
Chama changu, Chama cha Mapinduzi kwa kuniamini, kuniunga mkono na
kunisaidia kwa karibu, katika miaka yote hii kumi. Wakati wote CCM
imekuwa pamoja nami na Serikali. Kimetoa uongozi wa nchi na kuisimamia
Serikali kutekeleza Ilani.
Mwisho
lakini sio mwisho wa umuhimu, naishukuru sana familia yangu. Namshukuru
mke wangu Bi. Salma Kikwete kwa mchango wake mkubwa ulionipa utulivu wa
kutekeleza majukumu yangu. Upo msemo kwamba, “kwa kila mwanaume mwenye
mafanikio, yuko mwanamke”, nawaambia ni kweli. Shukrani zangu, pia, kwa
wanangu na wajukuu zangu kwa kunivumilia pale walipomkosa baba yao na
babu yao. Karibuni mambo yatakuwa tofauti mtaniona mara kwa mara kiasi
kuwa huenda mkanichoka.
Hitimisho
Mheshimiwa Spika;
Ninapoagana
na Bunge letu natambua kuwa baadhi ya Wabunge mnarudi kutetea viti
vyenu nawatakia kila la kheri. Nimewahi kuwa Mbunge, hivyo naelewa hofu
na mashaka mliyonayo. Mwenyezi Mungu awape utulivu na subira. Nawatakia
mapumziko mema kwa wale ambao mmeamua kustaafu. Wale wanaogombea Urais
waliomo humu nawatakia kila la kheri, na nawashukuru kwa kuonyesha nia
ya kunipokea mzigo huu mzito. Nawatakiwa heri katika matamanio yenu.
Kwa ndugu
zangu Watanzania wenzangu, nawashukuruni kwa kuniamini na kunichagua
mara mbili kuwa kiongozi wa nchi yetu. Nawashukuru kwa kuniunga mkono
wakati wote wa uongozi wangu. Mmenipa heshima kubwa ambayo sitakaa
nishau maishani mwangu. Ninamaliza kipindi changu cha uongozi nikiwa
nawapenda sana na nitaendelea kuwapenda mpaka siku Mwenyezi Mungu
atakaponiita. Nitawa-miss kama mtumishi na kiongozi wenu mkuu lakini
tutakutana kwa urahisi zaidi nikiwa raia. Baada ya hotuba yangu ndefu,
sasa natangaza kuwa Bunge la 10 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
limevunjwa rasmi, lakini litabakia kuwa hai mpaka tarehe itakayotangazwa
rasmi kwenye Gazeti la Serikali kwa mujibu wa Katiba.
Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania.
Asanteni kwa kunisikiliza!
0 comments :
Post a Comment