-->

HABARI MPASUKO:KUTOKA KWENYE KIKAO CHA KAMATI YA MAADILI DDOMA LEO HII

WAJUMBE wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutoka Kanda ya Kaskazini, Kati na Ziwa wamesema iwapo Kamati Kuu (CC) na wale wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) watawaletea majina ya watia nia ambao ni wachafu, mafisadi na wenye kashfa mbalimbali watagoma kupiga kura.

Aidha, wamesema pamoja na mchakato huo kufuata taratibu na kanuni za chama wameitaka Nec na CC kuhakikisha majina ya Profesa Mark Mwandosya, January Makamba na Makongora Nyerere yanapita hadi hatua ya tano bora.
Wakizungumza kwa sharti la kutotajwa majina wajumbe hao walisema wameajipanga vilivyo kuhakikisha kuwa chama kinakuwa na mgombea mzuri ila hawatakuwa tayari kupiga kura kwa mgombea ambaye hana sifa.
Mmoja wa wajumbe hao ambaye anatoka Kanda ya Kaskazini alisema harakati zote za watu kununua urais zimeonekana wazi tangu mwanzo hivyo hawako tayari kuona nguvu hiyo ikitumika katika hatua yao.
Wamesema kutokana na uzalendo wao na hakuna msukumo wa mtu yoyote na iwapo hawatasikilizwa maoni yao Wanzania na CCM watarajie maamuzi magumu.
Mjumbe huyo amesema wanaheshimu vikao halali ambavyo vinafanyika ila wanataarifa kuwa wajumbe wa NEC wamesharubuniwa hivyo ni rahisi kuwaletea majina machafu.
“Napenda kuwa wazi sisi hapa tunatoka mikoa mbalimbali tunasisitiza kuwa iwapo majina ya watu wachafu yakipitushwa nia afadhili chama kipasuke kuliko kuruhusu hali hiyo ambayo haikubaliki,” amesema
Kwa upande wake Mjumbe kutoka Kanda ya Kati amesema wajumbe wa NEC ni 340 lakini wao wapo 1,900 hivyo wakiwapuuza wao wengi lazima kieleweke.
Amesema CCM inatakiwa kupitisha mtu ambaye anasifa sahihi zinazokubalika kuanzia ngazi ya chini hadi juu na sio kutumia nguvu ya fedha kama ilivyojitokeza katika hatua za awali.
“Unajua kuna watu wametumia kadi za wadhamini ambao wamekufa halafu wanasema wanakubalika hilo sio kweli ushahidi upo hivyo wingi wawatu usitumike kama kigezo cha kupitishwa yeye,” amesema
Akizungumzia uamuzi huo mjumbe kutoka Kanda ya Ziwa amesema kanuni za CCM zipo 13 hivyo zikitumikaa ipasavyo ni dhahiri kuwa watu wachafu hawaweze kupita katika hatua hiyo ya tano bora.
Mjumbe huyo amesema Mwandosya, Makamba na Makongoro ni watu ambao wanasifa zinazohitajika ndani ya CCM, hivyo kinachohitajika ni CC kuongeza wengine wawili ambao sio kati ya mafisadi.
Amesema wagombea hao watatu ni wasafi, waadilifu na ni watu makini hivyo chama hakitafanya kosa kuwapitisha na mmoja wao kugombea nafasi hiyo ya urais.
“Kanuni zitatumika lakini pia kwa sisi kutoka kanda hizo tatu watu sahihi kwetu hadi sasa ni Mwandosya, Makamba na Makongoro ila wakituletea wezi, mafisadi hatupigi kura huo ndio msimamo wetu,” amesema .
Akizungumza na vyombo vya habari Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye amesema mgombea wa CCM atapatikana kwa kuzingatia kanuni na taratibu za chama na sio kwa nguvu ya presha ya nje kama inavyosemwa
SOURCE:KENGETE
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment