Emmanuel Okwi mwenye umri wa miaka 25 amepata fursa ya kwenda kufanya majaribio nchini Denmark katika klaabu iitwayo Sonderjsyke.
Sonderjsyke msimu uliopita ilinusurika kushuka daraja baada ya kumaliza ligi ikiwa nafasi ya kumi katika ligi yenye timu 12 ikiwa imeambulia pointi 33 katika mechi 33 ilizocheza.
Timu hiyo imeona huenda akawa mkombozi wao wa kuifanya timu hiyo kung'aa katika msimu utakaoanza na kuiondolea mkosi wa kukaa mstari wa karibu na shimo.
Emmanuel Okwi atakuwepo nchini Denmark kwa siku 14(wiki mbili) kuanzia tarehe 8/7/2015 akifanyiwa majaribio na kama atafudhu basi atasajiliwa na klabu hiyo ya Sunderjsyke iliyopo nchini Denmark.
Emmanue Okwi hii sio mara yake ya kwanza kwenda kufanya majaribio barani ulaya kwani alishawahi kufanya majaribio kwenye klabu ya Red Bull Salzburg iliyopo nchini Austria.
Klabu ya Simba imempa Okwi baraka zote za kwenda katika majaribio hayo na imesema itafurahi endapo mchezaji wao atafudhu na kufanikiwa kuweza kukipiga barani ulaya
0 comments :
Post a Comment