Harakati hizo za shirikisho la soka la Irani kuendesha uchunguzi huo maalumu wa kutambua jinsia halisi za wachezaji wa timu hiyo ulikuja baada ya kufichuka kwa siri kwamba kuna wanaume wanne katika timu ya taufa ya wanawake wa Irani.Shaka dhidi ya jinsia ya wachezaji wa timu ya wanawake wa Iran imeanza muda mrefu sana toka mwaka 2010 kuhusu golikipa wao.
Kwa mujibu wa mamlaka ya habari ya mashariki ya kati wachezaji watukutu wengi walikuwa ni wanaume ambao walikuwa wakiomyesha tabia mchanganyiko za kiume na kike ambao baadae walifahamika kuwa ni wanaume.
Kwa mujibu wa sheria mpya ya shirikisho la mpira wa miguu la Irani kwa sasa Timu yoyote ile ya wanawake haitoruhusiwa kushiriki mashindano ya mpira wa miguu kwa wanawake mpka wafanyiwe uchunguzi maalumu wa kutambua jinsia zao.
0 comments :
Post a Comment