TANZANIA TUNAHITAJI WAPINZANI WA KWELI
Kwanza napenda kumshukuru Mola wangu kwa kuweza kunipa siha njema ambayo ndio silaha yangu katika kupambana na madhira ya ulimwengu huu. Napenda kutumia nafasi hii kwanza kutoa yale yangu ya moyoni bila ya kujali au kuogopa chochote na kuafnya hivi ni haki yangu kwa mujibu wa Ibara ya 18(a) kupitia katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977.
Kabla ya kwenda katika kile kilichonifanya niandike makala hii napenda kuchukua nafasi hii kuwakumbusha watanzania wenzangu kuhusu Tanzania historia fupi mpaka tukafika katika mfumo wa vyama vingi.
Tanganyika ambayo kwa sasa inatambulika Tanzania baada ya kutoka katika utawala wa kikoloni na kuwa Uhuru wa taifa. Katiba ya mwaka 1961 ilitolewa kwa utawala ambao umechanguliwa, Mkuu wa bunge, ushindani wa vyama vingi, siasa na utawala wa kidemokrasia ya kisiasa na kisheria baada ya uhuru. Katiba ya Jamhuri ya 1962 ilipitishwa ikitumia mfumo wa rais ndio mtendaji na kupewa nguvu ya kuwa mkuu wan chi na mkuu wa serikali, rais alikuwa anaendesha nchi na hana wajibu hiari yake mwenyewe wala hakuwa na wajibu wa kufuata zabuni na mtu mwingine. Kusafisha njia kwa ajili ya kupata nguvu ya rais moja. Kipande cha sheria kandamizi kilipitishwa . hii ilikuwa sheria ya kutiwa kizuizini ya mwaka 1962, kwamba rais alitoa amri ya kukamatwa mtu yeyote ambaye alionekana ni hatari na kufungwa kwa ajili ya usalama wa serikali.
Tarehe 14 januari, 1963 karibu mwezi mmoja baada ya rais Julius K. Nyerere alitangaza kuwa Halmashauri kuu ya chama tawala cha Tanganyika African National Unity (TANU) chama kiliamua kwamba Tanganyika lazima kuwa na katiba ya chama kimoja kwa umoja na maslahi ya umoja wa kitaifa na maendeleo ya haraka ya kiuchumi. Kusisitiza kile alichokiita ni kitambulisho cha pekee katika jamii ya kiafrika alisema kwamba katika siasa za kiafrika kama vile jamii, usawa hakukuwa na mgogoro halisi wa tabaka tawala na kwahiyo hakuwa na mfumo wa vyama vingi, hivyo hakuna sababu ya kuwa na mfumo wa vyama vingi.
“ katika jamii ya kiafrika njia ya jadi ya kufanya mambo ni kwa majadiliano huru. Wazee kukaa chini ya mti mkubwa na kuzungumza hadi wao kukubaliana ’’ ( Nyerere 1966: 105). Inaweza kuonesha mti mkubwa ni chama tawala alisema.
Ilikuepeka kutoelewana na yeyote nadhani si lazima kusisitiza kwamba kazi ya tume ya kufikiria kama Tanganyika lazima kuwe na hali ya chama kimoja . uhamuzi huu tayari ulishachukuliwa na tume kuwa Tanganyika ni ya chama kimoja ila kazi ya tume ni kusema ni aina gain ya hali ya chama kimoja kimoja tunapaswa kuwa nacho kwa kuzingatia maadili ya taifa letu na kwa mujibu wa kanuni ambayo mimi na maelekezo na wewe chunguza (Nyerere 1966:252).
Tarehe 26 April 1964. Tanganyika na Zanzibar zinaungana na kuunda umoja wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kusaini mkataba iliyoitwa makala ya umoja wa wakuu husika ya hali ya Jamhuri Julius Nyerere na Abeid Karume. Kipengele muhimu cha maendeleo ya kisiasa ilikuwa kuimarishwa kwa mfumo wa serikali mbili na pande mbili za kiasasa baina ya Tanganyika African National Union(TANU) Tanzania bara na Afro Shiraz Party (ASP) kwa Tanganyika visiwani (Zanzibar).
Mabadiliko mengine alisema katika matendo ya umoja yalichukuliwa kwa kubadilisha katiba ya mpito ya Jamhuri ya Tanganyika na Zanzibar, 1965 (Shivji, 1990)
Katiba ya Jamhuri ya mwaka 1962 ilijulikana kama katiba ya “urais wa kifalme’’ basi katiba ya mpito ya mwaka 1965 kuundwa chini ya chama kimoja , wazo ambalo Nyerere aliliunga mkono mapema mwka 1962. katika mwanga huu ibara ya 3(1) ya katiba ya mpito tangu asili kwamba kutakuwa na chama kimoja cha siasa katika Tanzania. Hii ilikuwa mwanzo wa moja ya vyama vya kiasasa katika Tanzania.
Mwaka 1975 zaidi uwezo wa kisheria iliongezwa sheria namba 18 ya 1975 marekebisho ya makala ya 3 ya katiba ya mpito 1965 hadi kutoa kwamba “ shughuli zote za kisiasa katika Tanzania utaendeshwa na au nchini ya mwavuli wa chama ’’ vyombo vyote vya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itatekelezwa chini ya mwavuli wa chama . mwka 1977 serikali ilipitisha katiba ya kudumu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 1977 kuimarisha mabadiliko ambayo yamekuwa yanafanyika ila muhimu ni kuzaliwa kwa chama cha kimoja – Chama Cha Mapinduzi , matokeo ya muungano wa vyama viwili TANU na ASP ambacho kiliendelea kufanya kazi ya Tanzania bara na Zanzibar. Hatima ya kusudio la katiba ya kudumu ilikuwa ni kuimarisha chama tawala ( Makaramba, 1997). Ibara ya 3 ilivyoanisha CCM kama chama pekee cha siasa katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati ibara ya 3(2) inaipa CCM mamlaka ya mwisho juu ya mambo yote katika Jamhuti ya Muungano wa Tanzania . hii ni mtindo wa siasa wa chama kimoja inaongozwa na mazoezi ya siasa baada ya kujitegemea hadi julai 1992.
Hivyo mjadala wa mfumo wa vyama vingi kwa Tanzania sio kitu kigeni au kipya katika kipindi cha uhuru, baada ya majaribio ya mambo mabalimbali ya kidemokrasia, serikali na jamii wamekuwa wakishuhudia , inagwa kwa wakati hali ilikuwa kimya maneno kwa maneno hayo ya kisiasa. Hivyo mahitaji ya kubadili mfumo wa vyama vingi ulianzamwaka 1983 baada ya kutolewa mapendekezo ya umma kuanza mijadiliano ili kuweza kabadili au kurekebisha katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977..
Hadi kufikia mwaka 1989 , Nyerere alikuwa bado muumini imara wa chama kimoja . 5 marchi 1989 wakati bado mwenyekiti wa chama tawala ni Ali Hassani Mwinyi, aliuambia mkutano wa siasa katika Zanzibari kuwa ni wakati kwa nchi kutumia mamlaka yake. Kama vile kuwekwa kizuizini wanaharakati wa kisiasa kinyume na matakwa ya chama tawala . Nyerere alitangaza kwamba nguvu ingetumika kurejesha imani ya umma katika chama cha waanzilishi wake. Mwezi febuari 1990. nyerere mbunifu wa utawala wa chama kimoja aliatangaza kwamba sasa ni wakati wa kujadili kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa ( Daily Nation , 23 Febuari, 1990 ).
Miaka miwili baadae Nyerere alisukuma chama chakke tawala kuchukua umiliki wa mpango na kuongoza taifa katika zama mpya za demokrasia ya vyama vingi.
CCM inaweza na inapaswa kuwa karibishia nafasi ya kutoka kuongoza na kuwa na amani na mabadiliko katika nchi yetu. Tuna nafasi ya kuhakikisha kwamba mabadiliko haya hutokea kidemkrasia chini ya sheria kutoka kwa ajili ya demokrasia ya kweli. Huu ni wakati Tanzania chini ya CCM wanaweza kuchagua kubadilika na kusimamia mabadiliko ya kwamba baadala ya kufanywa mabadiliko( Daily News, Febuari 29 , 1992)
Matokeo ya mtazamo huu yalibadilisha mtazamo wa Nyerere wa mfumo wa chama kimoja.
Nyerere alifungua mjadala mpana katika nchi. Ndani ya muda mfupi iliundwa kamati iliyojumuisha wasomi, wanasheria, wanafunzi, wanaharakati wa kisiasa, viongozi mbalimbali. Kamati hiyo ilizinduliwa tarehe 28 febuari 1991 na mafaniko kupangwa semina ya vyama vingi katika nchi tarehe 11 juni 1991. ilizinduliwa kamati ya taifa ya katiba (NCCR) Kuongoza mahitaji ya mkutano mkubwa wa katiba , kuanzishwa kwa vyama vingi vya siasa na mkutano wa kujadili mfumo baadaye ya kisiasa ilikuwa ni maendeleo kwamba changamoto za nchi.
Hivyo tarehe 26 marchi 1991, rais Mwinyi alitangaza kwamba tume chini ya mwenyekiti Jaji Francis Nyalali na akachangua wajumbe kutoka chama tawala , serikali na watu binafsi katika Tanzania bara na Zanzibar na alipewa mwaka moja kukamilisha kazi yake. Hata kabla ya mwisho wa mamlaka yake alikuwa ameshawasilisha matokeo yake ya awali na athari hiyo, ingawa asilimia 77.2% ya wale waliohojiwa (36,299) kuendelea kuwa na mfumo wa chama kimoja , akapendekeza mabadiliko ya kisiasa yanaweza kushughulikiwa na mfumo wa vyama vingi.
Baada ya kutazama historia mpaka kufikia katika mfumo wa vyama vingi ambao leo ni tatizo katika nchi hii. Nakirejelea kichwa cha makala yangu kuna maswali ambayo utajiuliza kwa nini niseme TANZANIA TUNAHITAJI WAPINZANI WA KWELI, kwani kuna mambo mengi ambayo yanajitokeza tena yanafanywa na vyama vya upinzani ambayo yamenifanya kuandika makala hii mambo hayo ni kama ifuatavyo:
Mwaka 1995 chama cha NCCR MAGEUZI ndio chama cha upinzania ambacho kilikuwa kinavuta kwa watanzania wa wakati huu kwa kupitia mgombea wake wa Urais Mhe Mlema lakini kwa kuwa bado Tanzania tunahitaji wapenzani wa kweli. Umaharufu ambao aliupata Mlema na Chama chake kuwa na nguvu kubwa sana ndio waliposahau kazi ya upinzani na wakawa wanauchu wa madaraka na walikuwa kwa ajili ya maslahi binafsi na sio kwa ajili ya watanzania. NccR Mageuzi walishindwa kuleta mabadiliko katika siasa.
Mogororo uliibuka katika chama cha NCCR Mageuzi katika ya Mabere Marandu akimshutumu Bwana Mlema kuwa ni usalama wa taifa na Mlema naye akimshutuma Marandu kuwa ni msaliti, NCCR Mageuzi chini ya Marandu walihazimia na kumfukuza Mlema, na Mlema kuhamua kwenda TLP kwa kuwa Mlema alikuwa na wafahasi wengi ndani ya Chama aliondoka nao kitendo ambacho kilipelekea chama kukosa nguvu na yule ambaye alimfukuza mwenzioalishindwa kuendelea chama na hatima yake aliiacha chama na kwenda kujiunga na Chadema. Hapa naona kuwa NCCR mageuzi hawakuwa wapinzani wa kweli bali walikuwa ni wasakatonge ambao watanzania wangewapa ridha ya kuwaongoza wangekuwa wameuza nchi kwa bia nafuu sawa na bure. kama kweli walikuwa wapinzani wa ukweli baada ya kukosa serikali walikuwa wanalumbana wenyewe .
Sio NCCR Mageuzi tu bali CHADEMA ndio cha kinachoitwa cha upinzani kwani kwa mtazamo wangu bado akijakuwa na sifa ya kuwa chama cha upinzani kwani bado aakijakomaa kisiasa wala bado hakuna demokrasia ya ukweli ndani ya chama chao. Kwa nini nasema kuwa chama cha demokrasia bado hakina hadhi ya kuitwa cha upinzania kwa sababu zifuatazo
a. Ni chama cha kisichokuwa na demokrasia ya ukweli ila kimejiegemeza katika itikadi ya kihafidhina , kwani sifa kubwa ya chama cha kihafidhina kutokubali itikadi ya mabadiliko.
b. Kipo chini ya itikadi ya maeneo Fulani na sio kwa ajili ya Tanzania kwa ujumla
c. Kinapanda na wanachama ambao wapo kwa ajili ya watanzania
d. Kutokubali uhalisi na kubaki na tapo la ulimbwende na kushahhau tapo la uhalisia. Ndani ya chadema kama chama cha upinzani kimekuwa na mfumo wa kutokubali uhalisia kwani endapo utataka kutoa maoni yako yawe yale tu ya tapo la urasimi mkongwe kwani huwe unasifia uongozi wa juu na sio kwenda kinyume na na tabaka tawala ( uongozi mkuu).
Napenda kusema kuwa chama cha demokrasia bado akijakuwa chama sahihi cha upinzani . kwani sifa ya chama cha upinzani ni kwa ajili ya kukosoa chama tawala na kutoa suluhisho lakini chenyewe kipo kwa ajili ya kuwashughulikia wale wote ambao kwenye chama watakuwa wanakwenda kinyume kwa mujibu wao ila kwa mujibu wangu ni wale wote ambao wapo kwa ajili ya mabadiliko ya kweli na nia ya kumkomboa mtanzania wa leo ambaye yupo chini ya mwavuli wa ukandamizaji na anaishi kama mkimbizi ndani ya nchi yake.
Kwa upeo wangu nisingweza au kusubutu kumshambilia mtu eti kisa kajiunga na chama tawala hii ni aibu kwa wanachama na chadema na viongozi wao kwa kutumia majukwaa ya siasa katika mitandao ya kijamii kutoa maneno ya kejeli na kuwadharau wenzao( wasanii wa bongo movie) kujiunga na chama tawala. Ngoja niwakumbushe wana chadema kuwa jana wasanii walichukua haki yao kikatiba kwa mujibu wa ibara 20 ( 1) hivyo kuwa chama tawala au chama cha upinzani sio dhambi na kama chama cha upinzani sio kazi yako kuangalia nani yupo chama kipi wewe tangaza sera ya chama chako na sio kujadili vitu ambavyo havina maana.
Kwahiyo narejea kauli yangu kuwa Tanzania hatuna chama cha upinzani japo kuwa tunatambua uwepo wa mfumo wa vyama vingi.
Mungu isaidie Tanzania tupate wapinzani wa Kweli ambao watakuwepo kwa ajili ya kumkomboa Mtanzania ambaye anaishi chini ya dola moja ambaye anapata tabu nyingi kwani mfumo wa elimu bado ni kitandawili ambacho akina ufumbuzi mpaka leo, usuala la maji safi na salama ni fumbo lingine na matatizo mengine mengi. Kwa mtazamo wangu kuwepo kwa mfumo wa vyama vingi vingeweza kuleta haya mabadiliko ambayo chama tawala kimeshindwa kuleta.
MUNGU IBARIKI TANZANIA NA MUNGU WABARIKI WATANZANIA
MUNGU TUPATIE TANZANIA VYAMA VYA UPINZANI VYA UKWELI

Mwandishi wa makala hii

Jina: Mshana Junior
Mwanafunzi:Mwaka tatu(Muslim University of Morogoro)
Simu : 0712 474810
0 comments :
Post a Comment