-->

KAMATI YA BUNGE LA OIC KUANZA KIKAO CHA TEHRAN

OU_a5ec5.jpg
Dk Ali Larijani, Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran), upande wa kushoto.
Kikao cha 31 cha kamati ya utendaji ya mabunge ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Nchi za Kiislamu OIC kimeanza shughuli zake leo Ijumaa hapa mjini Tehran. Kikao hicho kimefunguliwa kwa hotuba ya Dakta Ali Larijani, Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu yaani Bunge la Iran. Kikao cha 31 cha kamati hiyo ya Umoja baina ya Mabunge ya Nchi za Kiislamu, kitakuwa na jukumu la kupanga na kuandaa ajenda ya mkutano mkuu wa umoja huo utakaofanyika katika siku za Jumanne na Jumatano za tarehe 18 na 19 Februari hapa mjini Tehran. Nchi 47 zimethibitisha kushiriki kwenye mkutano huo huku nchi 15 zikitangaza kuwa zitashiriki kama watazamaji.

Dk Ali Larijani amesema kuwa, mabunge ya nchi za Kiislamu na mabunge mengineyo yanaweza; kupitia uanachama wao katika Umoja wa Mabunge ya nchi wanachama wa OIC kuwa na mawasiliano ya karibu na watu wa mataifa mbalimbali na kuweza kufuatilia kwa karibu mahitaji ya wananchi.
Chanzo, kiswahili.irib.ir/habari
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment