Taarifa zinasema kuwa, vikosi vya kimataifa vya kulinda amani vimejizatiti katika uwanja wa ndege wa Bangui. Duru za habari zinaeleza kuwa, hali ya usalama mjini Bangui ni ya kutisha hasa baada ya kuuawa mbunge mmoja, ambaye alimkosoa waziwazi Waziri Mkuu wa nchi hiyo kwa kushindwa kunusuru maisha ya Waislamu wanaoshambuliwa mara kwa mara na wanamgambo wa Kikristo wa Anti Balaka.
Siku mbili zilizopita, kijana mmoja wa Kiislamu aliteketezwa kwa moto mbele ya jengo la Halmashauri ya Jiji, na kisha nyumba ya kijana huyo iliyokuwa karibu na ofisi hiyo ya serikali ikachomwa moto na wanamgambo wa Kikristo wa Anti Balaka. Wanajeshi wa Rwanda ambao wako nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati nao pia wanakabiliwa na hali ngumu, baada ya wanamgambo hao wa Kikristo kuamua kulishambulia jeshi la Rwanda kwa tuhuma za kuwasaidia Waislamu. Hali hiyo imejitokeza baada ya wanajeshi wa Rwanda kuwazuia wanamgambo wa Anti Balaka kumchoma moto kijana wa Kiislamu mjini Bangui.
CHANZO:IRANI SWAHILI RADIO
0 comments :
Post a Comment