-->

TANGAZO MAALUMU KWA VYOMBO VYA HABARI

Uongozi wa Swahili Media Group unapenda kuufahamisha umma kuwa Alex Kassuwi sio mtendaji wala mkurugenzi katika kampuni hii na tunapenda kuwatahadharisha wadau wote  kuacha kuwasiliana  au kufanya mikataba  ya aina yeyote kwa jina la Swahili Media Group na  kampuni zake tanzu na Kassuwi kwani haitatambuliwa.Kuhusu taarifa potofu ambazo zimekuwa zikitolewa na aliyekuwa hisa  mwenza katika kampuni hii Bwana Alex Kassuwi.

Kwa mujibu wa kumbukumbu zetu, Alex Kassuwi sio mmiliki na hahusiki na uendeshaji wa Swahili Media Group kuanzia mwezi Januari 21, 2014 baada ya wanahisa na menejimenti  kumuondoa kwa maslahi ya kampuni hii ni baada ya  kumsimamisha tangu mwezi Octoba 2013 kutokana na ubadhilifu wa mali za kampuni ambao aliufanya akiwa mmoja wa wakurugenzi wa  Swahili Media Group.

Katika kikao hicho Bwana Alex alikiri kuiba mali za kampuni zenye thamani ya zaidi ya dola $15,000 na kuzipeleka kuweka rehani (Pawn Shop) bila ya idhini ya uongozi, alikubaliana na hukumu ya kusimamishwa katika nafasi ya menejimenti na kubakia mwana hisa tu.ushahidi wa nyaraka za wizi kutoka Pawn Shops na mazungumzo ya mkutano yalirekodiwa.

Januari 8,2014 Bwana Alex aliomba  arudishwe kwenye  menejimenti na uendeshaji wa siku kwa siku wa kampuni, kwa njia ya email baada ya jitihada zake za kuomba kwa njia ya simu na text kushindikana, menejimenti ilikataa ombi lake la kumrudisha kazini hasa ikizingatiwa kwamba  nafasi hiyo itaweza kumuweka karibu na vyombo vya ofisi ikiwemo vile  ambavyo aliviiba awali lakini alifahamishwa kuwa hisa zake zitaendelea kuwepo.

Januari 19,2014 Bwana  Alex aliomba kujiondoa rasmi kwenye kampuni kama mmoja wa wanahisa ombi ambalo lilikubaliwa rasmi Januari 21 baada ya kikao cha wanahisa na menejimenti kumkubalia.

Kwa taarifa hii, tunawaomba wadau wote kutambua  kuwa Alex Kassuwi sio mfanyakazi wala mkurugenzi na hivyo haruhusiwi kuisemea  wala kufanya  mikataba yeyote ya Swahili Media Group ikiwemo maidhinisho kwa niaba ya Swahili Media Group.

Uongozi wa Swahili Media Group unamtakia Mafanikio mema bwana Kassuwi popote aendako.
Uongozi Swahili
Media Group / Swahili Media International.
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment