-->

JE VIBOKO MASHULENI NI HALALI???SOMA MAKALA HII KUJUA SHERIA ZINASEMAJE KUHUSU ILO



Tunapolitazama suala zima la adhabu mashuleni nchini Tanzania na nchi nyingine duniani ni kizungumkuti.Kuna mgawanyiko wa kimtazamo na pia kiitikadi katika makundi mawili; kuna wale wanaosema ni vyema na wajibu wanafunzi wakapata adhabu pale wanapokiuka sheria za shule na wale wanapinga vikali kuwepo kwa adhabu ya aina yeyote ile kwa mwanafunzi(wakisisitiza kutoa maelekezo sahihi kwa mwanafunzi).



Picha na voices.yahoo.com
Kuna adhabu mbalimbali zilizozoeleka kwa miaka mingi iliyopita hadi leo.Kila aliyepitia shule kwa ngazi ya awali hadi sekondari anajua mojawapo ya adhabu hizo; kubwa kuliko zote, na iliyozoeleka, pia inayosemekana ni rahisi kuitumia kurekebisha tabia mbaya ni ile ya viboko…najua kila mtu atakuwa anakumbuka siku alipowahi kuchapwa viboko na mwalimu wake.Bila shaka hakikuwa kipindi kizuri kwako.



Nchini Tanzania, adhabu ya viboko inaendelea kwa kusimamiwa na sheria ya adhabu ya  Kitaifa ya mwaka 1979 kama ilivyotolewa katika kipengele cha 60 cha Sheria ya Kitaifa ya Elimu ya mwaka 1978.



Mwaka 2000, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliweka mkazo kwa kutoa tamko la kisheria kupunguza idadi ya viboko kwa wanafunzi kutoka 6 hadi 4 na ilisisitiza kuwa ni Wakuu wa shule pekee wanaotakiwa kutoa adhabu hiyo.Pia ilitoa tamko la kutoa adhabu kali kwa walimu watakao kiuka sheria hiyo.[1]



Kwa upande mwingine, sheria ya kuwalinda watoto ya mwaka 2009 inaeleza kuwa wazazi wana wajibu wa kuwalinda watoto wao dhidi ya uonevu wa aina yeyote ile(kipengele cha 9), ikijumuisha kupigwa kunakopelekea maumivu kwa mtoto (kipengele cha 3).[2]



Kisaikolojia, adhabu ya viboko kwa mwanafunzi inapingwa vikali kutokana na athari za moja kwa moja kwa mwanafunzi kama;
  • Zinatengeneza mahusiano mabaya ya kibinadamu
  • Huchochea hofu na hali ya kutotaka kutenda kwa mwanafunzi husika 
  • Huchochea hali ya kujitengenezea mbinu za kujikinga na adhabu
  • Madhala ya viboko ni ya muda…maumivu ya viboko hudumu muda mfupi
  • Hazichochei tabia njema bali zinaficha uovu na utukutu.Kawaida mwanafunzi au mtoto    anayechapwa sana viboko, huwa na tabia mbaya.

  • Huangalia zaidi makosa/tabia mbaya kuliko tabia njema
  • Adhabu hii haidhibiti chanzo cha kutokea tabia mbaya ya mwanafunzi.



Tuungane pamoja kipindi kingine katika ukurasa huu wa Elimu ili kujifunza mbinu mbadala wa viboko kwa kutumia saikolojia bila kuleta maumivu au madhara kwa mwanafunzi wakati huo huo ikiboresha tabia njema na ufaulu wake.



Imetalarishwa na kutolewa na

Jielimishe Kwanza!
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment