Bloggers wengi wenye malengo ya muda mrefu na blogs zao pamoja bloggers wapya bado wanachanganyikiwa sana kuhusu platform ipi ni muhimu kuitumia kwenye blogging. Tanzania kwa sasa kuna mushrooming ya blogs, yaani kuwepo kwa blogs nyingi SANA! Ni jambo zuri kwamba watu wanajikita zaidi kwenye tech na ni “mzuka” tu wa kuwa na blog ndio unaowashika watu kwa sababu mwisho wa siku blog hizo hufa. Kinachonifurahisha zaidi ni jinsi ambavyo asilimia 70 ya heading ya blogs zetu utakuta “WELCOME TO MY WORLD”! Simlengi mtu yoyote but if the shoe fits feel free to wear it. Kama hiyo na wewe ndio heading yako, be creative, jitofautishe na wengine!
Yote ya yote, kuna platform nyingi za blogging lakini mbili kubwa ni blogger.com na wordpress.org
Blogger.com ina faida nyingi, na baadhi ni hizi:
1. Ni rahisi kutumia kwa bloggers wapya
Kufanya setup ni rahisi. Unafuata hatua tu na kuingiza details chache, basi!
2. No need to install anything.
Hauna haja ya kufanya installation yoyote! Kila kitu muhimu kipo by default.
3. Ni bure kutumia
As a beginner, hii ni platform nzuri ya kuanzia ka sababu utajifunza basics nyingi ambazo zitakuwezesha kuzoea blogging na ni bure.
4. Kuweka posts ni rahisi
Kuandika post ni rahisi. Ni sawa na kuchapa kwenye Ms Word tu.
5. Rahisi kubadilisha Theme
Kama hauna uhakika na jinsi blog yako inavyoonekana, unaweza ukabadilisha ndani ya sekunde moja tu! Hii inaafanya bloggers wapya wajue jinsi unavyoweza kutumia designs tofauti tofauti kwenye blogging.
6. Dashboard moja
Blog zako zote za blogspot utazipata katika sehemu moja tu tofauti na platform nyingine kama wordpress ambapo inabidi kila moja uifungue kivyake.
HASARA ZA KUTUMIA Blogger.com:
1. Limited flexibility
Ka sababu kuna designs na themes chache, most blogs look and feel the same. Blogs nyingi zinafanana na zina feel the same. Hii inamaanisha hauwezi kujitofautisha na bloggers wengine kwa sababu mnafanana kwa ukaribu sana.
2. Domain Name ndefu sana.
Since blog yako iko hosted na blogger.com, domain name yako itakuwa na brand yao kama:
www.jinalablogyako.blogspot.com
badala ya kuwa na domain kama
www.jinalablogyako.com
Visitors na wateja wako watajua kuwa umetengeneza kwa kutumia blogspot. Sio mbaya ingawa binafsi naona haipendezi watu kujua unatumia ninii. hata for security reasons, inakuwa rahisi kwa hacker kukushambulia akishajua unatumia nini. Kuhusu domain, unaweza ukanunua ya kwako ingawa ndio tayari utakuwa umeingia gharama nyingine.
3. Mmiliki HALISI wa blog yako anabaki kuwa Blogger.com!
Kama ulikuwa hujui, ni kwamba wewe hauimiliki blog yako iwapo ni ya blogspot. inamaanisha iwapo siku Blogger ikifungwa au ikiuzwa, inamiliki blog yako na kila kitu kwenye blog yako. Unless ulifanya backup sehemu, basi ndio utakuwa umepoteza kila kitu. Kama Blogger (yaani Blogger.com) wakiamua kwamba hawaipendi blog yako, wanaizima muda wowote.
Kama una maswali au kuna msaada uanhitaji, comment hapa chini.Kama una mpango wa kutengeneza hela online, unaweza kuanzia blogger ili ukue jinsi blogs zinavyofanya kazi. Baadae, unaweza kuhamia platform nyingine wanazotumia bloggers wazoefu.
0 comments :
Post a Comment