Huenda umekuwa ukitumia intaneti na
hasa mitandao ya kijamii ya Facebook, Twitter, Google+,LinkedIn na
mingine mingi na umeona unataka kujiondoa kabisa ama kuondoa kabisa
taarifa zako zisiendelee kuonekana katika mitandao hiyo kuna njia chache
za kuweza kufuata.
Hii ni njia ya kufuta taarifa zako kwenye facebook |
Facebook
imeweka njia ambayo iko wazi kuonekana kwa kila mtumiaji ambaye anataka
kujiondoa kwenye mtandao huo nayo ni kusitisha yaani kudeactivate
ambayo unaweza kuipata kwenye Account Settings > Security > Deactivate your account.
Usidanganyike
siyo kwamba inaondoa taarifa zako bali inazitunza taarifa zako ili
unapobadilisha uamuzi wa kurudi tena uzipate taarifa hizo.
Kama unataka kweli kuondoa taarifa zako basi unahitaji kulogin kwenye wasifu wako kisha bofya Delete My Account
na baada ya hapo bofya kibox cha bluu hapo utakuwa umeondoa kila kitu
kwenye mtandao wa kijamii wa facebook na huwezi kuzirudisha tena japo
itabidi usubiri baada ya siku 40 zitakuwa zimeondolewa kabisa .
Japo kabla ya kufanya inakupasa uhamishe taarifa zako na mambo yote kwenye tarakirishi yako kwa kufanya hatua zifuatazo Account Settings > General > Download a copy of your Facebook Data > Start My Archive.
Kama ilivyo kwenye facebook ,katika mtandao wa Twitter deactivate ina maanisha ondoa ama futa,ni rahisi sana nenda Account Settings > Deactivate my account > Okay, fine, deactivate account. na hapo weka neno lako la siri imemalizika.
Twitter nayo hutunza kumbukumbu zako
kwa siku 30 ikiwa utabadilisha uamuzi utazikuta taarifa zako,usipofanya
hivyo baada ya muda huo zitakuwa zimeondolewa
Hiyo ni baadhi ya mifano ya kuondoa taarifa zako katika tovuti ya accountkiller.com inatoa maelezo ya mbinu mbalimbali za kufuta taarifa zako katika mitandao mbalimbali ya kijamii
CHANZO:MAISHANATEKNOHAMA
0 comments :
Post a Comment