GWIJI Sir Bobby Charlton alikabidhiwa
tuzo ya mafanikio ya muda mrefu na Rio Ferdinand katika tuzo za mwaka
2013 za GQ jana usiku.
Gwiji huyo wa Manchester United
aliungana na Carl Froch na Andy Murray kwa kutambuliwa kwa michango yao
katika ulimwengu wa michezo.
Mwandishi wa Sportsmail Jamie Redknapp
alimkabidhi Froch tuzo ya Mwanamichezo Bora wa mwaka katika sherehe
zilizofanyika hoteli ya Royal Opera, wakati Murray, ambaye kwa sasa yupo
kwenye michuano ya Tenisi ya US Open, ameshinda tuzo ya Mafanikio ya
Mwaka.
Wakali wa United: Sir Bobby Charlton
alikabidhiwa tuzo mafanikio ya muda mrefu ya GQ na nyota wa sasa wa Old
Trafford, Rio Ferdinand
Sura maarufu: Elton John alikuwepo kwenye tuzo hizo sambamba na Bobby Charlton na mkewe, Norma
Mshikilia taji: Mwakilishi wa Sportsmail, Jamie Redknapp akimkabidhi Carl Froch tuzo ya
Mwanamichezo wa Mwaka
SOURCE:BIN ZUBERY
0 comments :
Post a Comment