-->

TANZANIA YAPOROMOKA KWENYE VIWANGO VYA SOKA KIDUNIA HUKU KENYA NA UGANDA KUPANDA






Tanzania imeporoka nafasi tano kwenye msimamo wa ubora wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).

Tanzania sasa imeporomoka hadi nafasi ya 122 ikiwa na pointi 226 nyuma ya Malawi iliyo katika nafasi ya 121 ikiwa na pointi227.

Baada ya Tanzania inayoshika nafasi ya 122, inayofuatia katika nafasi ya 123 ni Afghanistan ambayo inatawaliwa na vita na si timu yenye umaarufu hata chembe katika mchezo wa soka.

Nchi zilizo chini ya Tanzania ambazo zinatokea Afrika Mashariki na Kati ni Burundi iliyo katika nafasi ya 125 baada ya kupanda nafasi nne, wakati Rwanda iko namba 129 baada ya kukwea nafasi tano juu.

Kenya iko katika nafasi ya 106 baada ya kupanda nafasi tatu, Sudan nafasi ya 117, Ethiopia wanashika 101 wakati Waganda ndiyo wanaonekana vinara katika ukanda huu kwa kuwa wako 86 huku wakiwa wameporomoka nafasi moja tu.
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment