-->

CCM YAVUNA WANACHAMA WAPYA KIBAO KUTOKEA KASULU


  •  Zaidi ya watu 700 wajiunga na CCM akiwemo aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF Kata ya Rungwe mpya.
  • Asema mtaji wa vyama vya Upinzani ni matatizo ya wananchi na hawasaidii katika kuyatatua badala yake wanataka wananchi waendelee kuumia ili wao wajijenge kisiasa .
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Nyenge  kata ya Kurugongo wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma ikiwa sehemu ya ziara yake mkoani humo.
 Mbunge wa Viti Maalum Ndugu Josephine Gezabuke akihutubia wakazi wa kijiji cha Nyenge kata ya Kurugongo wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo na mgeni wa heshima alikuwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa ofisi ya Tawi CCM kata ya Kurugongo wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akila karanga za kuchemsha pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye baada ya kumaliza mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya michezo shule ya Msingi Nyenge kata ya Kurugongo wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma.
 Balozi Ali Abeid Karume akicheza ngoma ya asili ya Kasulu wakati wa mapokezi kwenye viwanja vya Stendi ya taxi Kasulu mjini.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Ndugu Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Kasulu mjini kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kituo cha stendi ya Taxi na kuwaambia wananchi hao CCM imedhihirisha kuwa komavu kwenye demokrasia ya kweli na hali inavyoendelea hivi sasa wapinzani wameanza kupotea kabisa kwenye siasa kwani kwenye uchaguzi wa madiwani kati ya kata 27 walipata tatu, ubunge Kalenga na Chalinze wameanguka vibaya sana .
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wakazi wa Kasulu mjini na kuwaambia kuwa CCM itaendelea kuhakikisha maendeleo yaliopangwa yanazidi kutekelezwa licha ya kuwa na changamoto mbali mbali hasa wapinzani kutaka wananchi wateseke ili wao wajijenge kisiasa alisema sivyema vyama pinzani kutafuta  sifa kwenye matatizo ya wananchi.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwainua juu wanachama wapya waliojiunga leo kutokea vyama vya upinzani kulia ni Ndugu Nahasoni Kigamba alikuwa Mwenyekiti wa CUF kata ya Rungwe mpya na Adolf Yanda aliyekuwa Katibu wa Chadema kwa wanafunzi wa chuo cha SUA,katika mikutano miwili mikubwa ya leo zaidi ya wanachama 700 walijiunga na CCM .
SOURCE:MWIGULU BLOG
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment