-->

PAPA AWAOMBEA MSAMAHA MAKASISI WALIOWALAWITI WATOTO

Kiongozi wa kanisa katoliki Papa Francis
Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis, amewaombea radhi makasisi wa kanisa hilo waliowakosea watoto kwa kuwalawiti.
Papa Francis alinukuliwa kupitia redio ya kanisa hilo mjini Vatican, akitaja dhuluma za kingono dhidi ya watoto kama ukosefu wa maadili miongoni mwa viongozi wa kanisa na kusema watakaopatikana na hatia watawekewa vikwazo.
Mwezi jana Papa Francis, alitetea vikali rekodi ya kanisa katoliki katika kukabiliana na tatizo la dhuluma za kingono zinazotendwa na viongozi wa kanisa.
Ilikuwa baada ya umoja wa Mataifa kutuhumu kanisa hilo kwa kukosa kuwachukulia hatua makasisi watovu wa nidhamu.
Mwaka jana Papa aliunda kamati maalum ya kuhakikisha waathiriwa wa dhuluma za kingono wanapata kusaidiwa, lakini amekosolewa na baadhi ya waumini wa kanisa kwa kujikokota katika kutambua athari za tatizo hilo hasa kisaikolojia kwa waathiriwa.
Alisema alihisi umuhimu mkubwa wa kuomba msamaha kwa niaba ya makasisi waliowalawiti watoto ingawa alisisitiza kuwa idadi ya makasisi hao sio kubwa sana ikilinganishwa na idadi kamili ya makasisi wa kanisa hilo.
"Hatutapiga hatua yoyote nyuma kuhusu tatizo hili, vikwazo vinavyohitajika lazima vitawekwa,'' alisema papa. ''Lazima tuchukue hatua kuanzia sasa.''
Katika mahojiano mwezi jana, papa alilalamika kuwa hakuna aliyechukua hatua kukabiliana na visa vya ulawiti wa watoto kanisani ingawa kanisa linashambuliwa na kuambiwa limegea katika kuchukua hatua.
Kanisa katoliki limekuwa likituhumiwa kwa kosa la makasisi kuwadhulumu watoto kingono katika mengi ya makaisa yake duniani kutokana na maaskofu kukosa kuchukua hatua zozote.
SOURCE:BBC SWAHILI
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment