-->

KATIBU MKUU WA UMOJA WA MATAIA ATOA TAHADHARI AFRIKA MASHARIKI YA KATI

130916202824_ban_ki_moon_304x171_getty_nocredit_a7ee3.jpg
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema nchi ya Jamuhuri ya Kati haipaswi kuruhusiwa kugeuka kuwa Rwanda nyingine.
Akiandika maoni yake kwenye mtandao wa BBC, Bwana Ban amesema kwamba zaidi ya nusu ya raia wa Jamuhuri ya Afrika ya Kati wanahitaji msaada wa kibinadamu.
Akihusisha mambo yalivyo Jamuhuri ya Afrika ya Kati na kumbukumbu ya miaka 20 ya mauaji ya halaiki nchini Rwanda, amesema jamii ya kimataifa inapaswa kuchukua hatua sasa badala ya baadae kuja kuomba msamaha itakapotimia miaka ishirini ijayo.
Siku ya Alhamis Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa liliwapa mamlaka wanajeshi 12,000 wa Umoja wa Mataifa waliopo nchini Jamuhuri ya Afrika ya Kati.(Awadh Ibrahim)
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment