Mahafali ya sita ya chuo kikuu cha Kiislam Morogoro ambayo yamefanyika hapo jana tarehe 9/11/2013 yalikuwa ni mahafali ya kipekee baada ya kuhudhuliwa na maelfu ya watu huku magari mbali mbali ya Abood na costa mbali mbali zingijiingizia siku kwa kupata wateja wa kuwasafirisha kwenda mikoani.Pia wawakilishi mbali kutoka vyuo vingine kama vile dodoma,St Joseph,Jordan na vinginevyo walifika kwenye sherehe hizo za kutunukiwa shahada kwa wahitimu hao.Ujio wa wageni hao kutoka vyuo mbali mbali ulionyesha ishara ya mahusiano mazuri ambayo chuo imekuwa nayo na vyuo vingine vilivyomo ndani ya nchi.
Moja ya mabasi ya Abood likiwa linashusha abiria kuja kwenye mahafali kutokea Dar es salaam katika viwanja vya Muslim university of Morogoro
Gari yenye nembo ya St Joseph likiwa limepaki katika eneo ambalo magari mbali mbali yalipaki
.Mahafali hiyo amabayo mgeni rasmi alikuwa mkuu wa chuo hicho cha kiislam Hajjat Mwantumu Malale aliewatuku shahada mbali mbali wahitimu hao kama vile shahada ya uzamivu,shahada ya ukalimani,na nyinginezo.
meza kuu ikiwa imesheheni wahadhiri mbali wakiweno maprofesa pamoja na madokta ambao ni sehemu ya uongozi wa chuo wakioongozwa na makamu mkuu wa chuo Profesa Hamza Njozi.
Biashara ya mataji,juisi,soda pamoja vitu vingine mbali mbali vilihamia eneo la karibu na chuo kwani maelfu ya watu waliweza kuhuduria sherehe hizo
kamera yetu pia ilimnasa mwandishi wa JICHO LA HABARI akiwa anawasiri kwenye sherehe hizo
0 comments :
Post a Comment