Zimebaki pointi tatu tu Azam FC kuwa
mabingwa wa Ligi Kuu Bara kwa mara ya kwanza, hilo halina ubishi.
Azam FC wameshinda mabao 3-0 dhidi ya
Ruvu Shooting katika mechi ya Ligi Kuu Bara iliyochezwa leo kwenye Uwanja wa
Mabatini mjini Mlandizi.
Iwapo Azam FC itaifunga Mbeya City
katika mechi yake itakayofuata, Azam FC ambayo sasa ina pointi 56, maana yake
watatawazwa rasmi kubwa mabingwa.
Katika mechi mabao ya Azam FC yalifungwa
na mshambuliaji mkongwe, Gaudence Mwaikimba, Himid Mao na Kipre Tchetche.
Awali mechi hiyo ilikuwa ichezwe jana lakini kutokana na mvua kubwa, ikaahirishwa na kupangwa kuchezwa leo.
About Omari Makoo
0 comments :
Post a Comment