Kituo cha Redio cha Al-Noor kilichoadhirika na maafa ya kuungua kwa moto
KITUO
cha kurushia matangazo cha redio Al-Noor kilichopo Mtoni Kidatu wilaya
ya magharibi Unguja kimeungua moto usiku wa kuamkia jana na kusababisha
hasara inayokisiwa kufikia shilingi milioni 80.
Mkurugenzi wa redio hiyo, Mohammed Suleiman, alisema moto huo inawezekana ukawa umesababishwa na hitilafu za umeme.
Alisema
moto huo umeteketeza maeneo yote ya studio zao zote tatu za redio hiyo
na vitu mbalimbali vilivyomo ndani ya studio hizo.
Akivitaja
vitu hivyo Mkurugenzi huyo alifahamisha kuwa ni studio namba moja,
studio namba mbili na studio namba tatu ambayo ni studio kubwa kwa ajili
ya kurushia matangazo na vitu vingine vilivyoungua ni mashine za
kurushia matangazo, kompyuta za kurikodi, mafeni, mazulia na vitu
vingine viliopo ndani ya studio hizo.
Baadhi ya vifaa vilivyounguaa moto uliosababishwa na hitilafu za umeme
“Moto
umetokea usiku wa saa 8 tunasema inawezekana ikawa umesababishwa na
shoti ya umeme japo kuwa hatujathibitishiwa na watu wa umeme lakini
mwanzo ulikuwa umezimwa na ulipowashwa ndipo ilipotokea shoti hiyo na
kuunguza vitu mbalimbali ambavyo vilikuwa vikitumika kwa kuendeleza kazi
zitu za redio”, alisema.
Alifahamisha
kuwa studio namba tatu ni studio kubwa ya kurushia matangazo hivyo
studio hiyo imeungua vitu vyote na kusababisha hasara inayokisiwa ni
zaidi ya milioni 52.
Mkurugenzi
huyo alifahamisha kuwa kutokana na hali hiyo na hasara waliyoipata
kituo hicho hivi sasa kimesimamisha matangazo yake kwa muda hadi pale
watapoweza kukamilisha matengenezo na manunuzi ya vifaa vilivyoungua.
Alisema kituo hicho si mara ya mwanzo kuungua kwani siku za nyuma kimeshawahi kuungua lakini hasara haikuwa kubwa.
Mbali
ya hasara hiyo, alisema mfanyakazi wao Abubakar Fakih, amejeruhiwa kwa
kuvunjika mguu na mkono baada ya kuruka ili kujinusuru.
“Mfanyakazi wetu toka aumie tupo nae pamoja na yupo hospitali kuu ya Mnazimmoja na amefanyiwa upasuaji,” alisema.
Aidha alisema vitabu vitatu vitakatifu (Quran) ambavyo vilikuwa ndani ya studio zilizoungua, havikuguswa na moto huo.
Aidha alisema kituo hicho hakitarusha matangazo yake kwa sasa hadi matengenezo yatakapofanywa.
Alitumia nafasi hiyo kuwataka waumini, wafadhili na watu wenye uwezo kuisaidia redio hiyo.
Posted by Abou Shatry
About Omari Makoo
0 comments :
Post a Comment