Mkurugenzi
wa Mawasiliano Airtel Tanzania Beatrice Singano akiongea na waandishi
wa Habari wakati wa kutangaza Kliniki ya Kimataifa ya mpira wa soka ya
Manchester United ambayo itafanyika Jijini Dar es Salaam April 23-27
chini ya wakufunzi kutoka Klabu ya Manchester United. Kushoto ni
Mkurugenzi wa Mashindano ya Vijana Ayoub Nyenzi.
.Kliniki ya soka ya Man U kufanyika Dar
· Kuendeshwa na wakufunzi wa Man U
· Kushirikisha nchi 12
· Tanzania kuwakilishwa na wachezaji 19
Kampuni
ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania janaimetangaza kufanyika kwa
kliniki ya soka ya Kimataifa ya Manchester United hapa Dar es Salaam
kuanzania 23 -27 Aprili mwaka huu.
Kliniki
hiyo ambayo itafanyika kwenye uwanja wa Azama FC (Chamazi Complex
Stadium), ina nia ya kuwaendeleza vijana waliofanya vizuri kwenye
michuano ya mwaka jana ya kimataifa ambayo ilifanyika Lagos, Nigeria na
kushirikisha nchi 12 ambapo timu ya Tanzania ya wasichana iliibuka
mabingwa.
Hii ni
mara ya pili kwa kliniki kama hiyo kufanyika hapa nchini kufuatia
kliniki kama hii liyofanyika kwenye Uwanja wa Taifa 2011. Kliniki
nyingine ilifanyika Nairobi 2012 na Tanzania iliwakilishwa na wavulana
watatu na wasichana watatu.
Kama
ilivyokuwa kwenye kliniki zilizopita, kliniki ya mwaka huu itaendeshwa
na makocha kutoka shule za soka za Klabu ya Manchester United na
wanatarajiwa kutoa mafunzo ya awali ya mpira wa miguu kama vile kupiga
pasi, kukimbia na mpira, kupiga mashoot, nidhamu na nyingine nyingi.
Akiongea
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa
Mawasiliano wa Airtel Tanzania Beatrice Singano alisema kliniki hiyo ni
sehemu ya mpango kapambe wa Airtel kusaka na kuendeleza vipaji vya soka
hapa Tanzania na Barani Afrika kwa ujumla.
‘Airtel
inajivunia kuwekeza kwenye soka ambayo ina uwezo wa kuileta jamii pamoja
kupitia hamasa ya mashabiki na yenye uwezo wa kuwafanya wachezaji
kupata elimu pamoja na ajira’, anasema Singano.
Aliongeza
kuwa Airtel inajivunia programu ya Airtel Rising Stars kwa kuleta
furaha na hamasa kubwa miongoni mwa vijana wa Tanzania na pande nyingine
za Bara la Afrika hivyo kuifanya kampuni ya Airtel kuhamasika kuendelea
kuwekeza kwenye soka.
Kwa
upande wake, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Celestine
Mwesigwa ameishukuru kampuni ya Airtel kwa mpango huu makini wenye nia
ya kutafuta na kuendeleza vipaji chipukizi vya soka Tanzania.
‘Ninaamini
ya kwamba Tanzania imebarikiwa kuwa na vipaji vingi vya soka.
Tunachohitaji ni uwezo wa kifungi na raslimali za kutuwezesha kusonga
mbele na ndio maana tunawashukuru Airtel kwa kujitokeza kutuunga mkono
kupitia programu hii ya vijana’, Anasema katibu wa TFF.
Washiriki
wa kliniki hii watatoka nchi za Kenya, Uganda, Malawi, Chad, Burkina
Fasso, Sierra Leon, Sheli sheli, Congo Brazzaville, Nigeria, Zambia na
wenyeji Tanzania ambao watawakilishwa na wachezaji 19.
Airtel
Rising Stars ni programu inayojumuisha Africa nzima ili kutoa nafasi kwa
wanasoka chipukizi chini ya umri wa miaka 17 kuonyesha uwezo wao mbele
ya mawakala wa soka, makocha na kupata fursa ya kujiendeleza zaidi.
Mpango huu unawalenga wavulana na wasichana Barani Afrika.
Mkurugenzi
wa Mawasiliano Airtel Tanzania Beatrice Singano akiongea na waandishi
wa Habari wakati wa kutangaza Kliniki ya Kimataifa ya mpira wa soka ya
Manchester United ambayo itafanyika Jijini Dar es Salaam April 23-27
chini ya wakufunzi kutoka Klabu ya Manchester United. Kulia ni Afisa
Uhusiano Airtel Tanzania Tanzania Public Relations Officer Jane Matinde
0 comments :
Post a Comment