Dodoma, Tanzania. Wabunge watatu shujaa; Peter Serukamba (CCM), Tundu Lissu (Chadema) na Jenister Mhagama (CCM) waliokua mstari wa mbele, wamewaokoa waandishi wa habari na wamiliki wa vyombo vya habari baada ya kukataa mapendekezo ya serikali ya kubadili vipengele vya Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976 ya kuongeza adhabu kwa waandishi hao endapo watapatikana na hatia ya makosa ya uchochezi.
Pia Spika wa Bunge Anne Makinda naye hakuwa nyuma kwani aliungana na wabunge wengine wakiwamo hao watatu kukataa mapendekezo hayo na kusema kwamba wakati sasa umefika kwa serikali kupeleka bungeni muswada wa sheria wa vyombo vya habari badala ya kuendelea kutoa ahadi zizizokuwa na majibu kila wakati.
Wakati akitoa mapendekezo hayo kwa wabunge, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema alisema: Sitegemei magazeti kuwa mbunge nafanya kazi ya taifa. Walio wangu watanikataa na wasiokuwa wangu watanikataa.Nipo kwa ajili ya Taifa, sitamwangukia mtu yeyote miguuni," amesema Jaji Werema.
Kauli hiyo ilionekana kuwachafua wabunge na wengine kuudhika.
ku
Baada ya muda mfupi kupita, Spika Makinda aliwahoji wabunge na kukataa na kukataa mapendekezo ya serikali. Kutokana na wabunge kukataa, Jaji Werema alisimama na kutaka Spika aruhusu kura zihesabiwe katika kifungu hicho.
"Mheshimiwa Spika, nimesimama kuona hata wa upande wangu wamenisaliti, duh basi naomba kura zihesabiwe kwa kuita majina mmoja mmoja ili tujiridhishe," alisema Jaji Werema.
Wabunge waliokuwa shujaa ni Mbunge wa Kigoma Mjini, Peter Serukamba (CCM), ambaye alipendekeza sehemu ya nane ya muswada iliyokuwa na vipengele vya 39, 40 na 41 iondolewe ili kushinikiza serikali
kupeleka bungeni Sheria nzima inayohusu vyombo vya habari.
"Tukatae vipengele hivi, nawaomba wabunge wenzangu mniunge mkono katika hili na ikiwa tutavikataa vipengele hivi Serikali italeta sheria nzima hapa, mimi sina tatizo na adhabi hata ingekuwa mara tatu, lakini tuleteeni sheria nzima, mnaogopa nini?"
Mbunge wa Peramiho,Jenista Mhagama alisema: "Kwa nini Serikali inachelewesha kuwasilisha muswada wa sheria bungeni? Hebu sasa tukae na wadau tukubaliane mambo ya msingi, tuwe na sheria ili kuinusuru tasnia ya habari, sheria itasaidia kuwadhibiti makanjanja, wapo watu wanaoidhalilisha tasnia ya habari bila sababu za msingi."
Mbunge wa Chadema, Tundu Lissu naye hakuwa nyuma kwani alisema: "Tangu sheria hiyo ilipotungwa miaka zaidi ya 37 iliyopita, hakuna mwandishi wa habari au mchapishaji wa gazeti lolote ambaye amewahi kufikishwa mahakamani na kupatikana na hatia ya makosa hayo badala ya kuwapeleka wakosaji mahakamani, Setikali inafunga magazeti."
CHANZO:HABARIMASAI
0 comments :
Post a Comment