Godfrey Zambi(Mb) |
Leo katika kikao cha jioni cha Bunge la Tanzania Mh.Godfrey Zambi(Mb)
aliomba kutoa hoja binafsi muda mfupi kabla ya bunge kuahirishwa mpaka
kikao cha jumamosi.
Hoja hiyo ililenga Electronics Fiscal Devise (EFD)
zinazotumiwa sasa na wafanyabiashara baada ya maagizo kutoka Tanzania
Revenue Authority (TRA). Hoja yake ililenga pia kuzungumzia kero
wanayopata baadhi ya wafanyabiashara waliokaidi agizo hilo kuanzia
mkoani Mbeya na kwingeneko nchini. Utakumbuka mwanzoni mwa mwaka huu
kulikuwa na mgogoro jijini Mbeya kutokana pia na mashine hizo.
Mashine hizo zinauzwa kati ya Tsh laki 8 mpaka Million 1 za Tanzania. kinyume kabisa cha bei zake sokoni.
Najaribu kumnukuu Mh.Zambi"Nimepata kusafiri nchini Dubai na China pia
katika ziara na waziri mkuu nimeona hizo mashine hazina bei hiyo ambayo
TRA wanawauzia wafanyabiashara"
DONDOO KUHUSU EFD
- Zinauzwa kati ya Tsh laki 8- millioni 1 za Tanzania.
- Mwisho wa Tarehe ya mfanyabiashara kununua ni 14 Novemba 2013.
- Mfanyabiashara akikosea muamala mmoja(Single Transaction) Faini yake ni Tsh million 3.
- Mfanayabiashara anapewa mafuzo ya kati ya siku moja au mbili.
- Mashine ikileta matatizo kutengenezwa kwake ni kati ya Tsh Elfu 25.
KERO ZA EFD KWA WAFANYABIASHARA
- Zinauzwa Bei ghali sana,kulinganisha na Bei yake halisi
- Elimu iliyotolewa kwa wafanyabiashara ni ndogo sana kiasi cha kuelewa mfumo wa mashine hizo
UMUHIMU WA EFD EFD KWA NCHI
- Zinasaidia kutunza kumbukumbu za mauzo ya Mfanyabiashara.
- Zinaleta faida kwa Taifa kwa kukusanya Kodi.
0 comments :
Post a Comment