Jamii imepandikizwa makosa yafuatayo kuhusu magonjwa haya
1. Baada ya mgonjwa kubainika kuwa ana pressure au kisukari moja ya sentesi ambayo anaambiwa na watumishi wengi wa afya kuwa kisukari hakitibiki hivyo anatakiwa kunywa hizo dawa hadi atakapokufa. Ni kweli magonjwa tabia usipo badili mwenendo wa maisha utatumia dawa hizi miaka na miaka. Hivyo ninachokushauri ndg rafiki dawa ya magonjwa yote sugu unayo nyumbani ni wewe mwenyewe kujitibu. Dawa za hospital zipo hapo kukusaidia pale unaposhindwa kuhakikisha kuwa sukari yako au pressure yako ina kuwa sawa muda wote. Pia inatakiwa tujifunze namna ya kula vyakula kama tiba. Kwani wengi sana hupenda kuuliza iweje chakula tunakula kila siku na hakitutibu!!! Jibu ni kwamba hakitibu ni kwa sababu hatujui kupangilia na kupika kiwango cha vyakula kama tiba. Hivyo rafiki yangu kama leo hii unataka kuepukana na magonjwa sugu ni kujifunza namna nzuri ya kutumia vyakula kama tiba.
2. Kumekuwa na wimbi kubwa la jamii na watu mbalilmbali wanaosema wanatibu kwa kutumia mimea na matunda ni dhahiri kuwa elimu inatakiwa itolewe ili wawe na uwezo mkubwa wa kushauri kuhusu huduma ya tiba lishe na sio kubabaisha. Kwani uchunguzi unaonesha kuwa wengi hawana uwezo wa kutibu kwa kutumia vyakula. Chakula ni tiba hii ni ukweli usiopingika kwani moja ya tatizo na changamoto kubwa ni kuwa watu wengi wanatumia dawa za hospitalini miaka na miaka bila kupata nafuu hii ni kwa sababu tu hawajabadili mwenendo wa maisha yao.
3. Watumishi wa afya kutofundishwa lishe ya nadharia bali tunafundishwa lishe ya kujibia mtihani ambapo unajikuta huna uwezo wa kumshauri mgopnjwa vizuri kuhusu lishe tiba. Asilimia 90 ya magonjwa ya kitabia hutibiwa kwa kutumia tiba lishe ya matunda na mbogamboga.
KISA CHA MAMA WA DR JOSH AXE
Mama yake dr Axe alikuwa ni mkufunzi wa kitengo cha kutoa mazoezi ,kukimbia na kuogelea hivyo muda wote alikua anajihusisha na mazoezi ili kuuujenga mwili wake. Baada ya miaka kadhaa akiwa kazini alienda kuchunguzwa hospitali na kukutwa na kansa ya titi baada ya hapo tiba ya MIONZI NA CHEMICAL DRUGS IKAANZA. Alitibiwa kwa miaka miwili kwa mionzi baada ya hapo akaenda kupima akaambiwa uvimbe umeisha. Alikuwa amepona kulingana na vipimo vya madaktari lakini ni mtu aliekuwa anaishi na MAUMIVU MAKALI MWILI MZIMA, HAKUNA USINGIZI,KICHWA KUUMA SANA,MIGUU KUUMA,KUKOSA HAMU YA KULA NA KUJISIKIA KUCHOKA MUDA WOTE. Baada ya hapo aliamua kwenda kupata uchunguzi tena uchunguzi ulibaini kuwa ana uvimbe mwingine tumboni. Ndipo m,ama AXE aliamua kuchukua uamuzi wa kutibiwa kwa kutumia PLANT BASED DIET. Akapangia vyakula ,matunda na mbogamboga vizuri baada ya mwaka mmoja alienda kupima na kukuta uvimbe umepungua kutoka 2.5cm hadi 1.5 na huku yale maumivu na matatizo yote ya mwili hayapo tena na afya yake imerudi upya. Baada ya mwaka mmoja alienda tena kupima akakuta uvimbe umeisha. Mungu abarikiwe. Mungu alimuonesha maisha halisi ni dhahiri kuwa mama huyu
0 comments :
Post a Comment