-->

BABA ASKOFU AKUTWA NA MADAWA YA KULEVYA

Askofu Emeka Nwachukwu Mert raia wa Nigeria anayehusishwa na biashara ya madawa ya kulevya. 
Vigogo wa madawa ya kulevya wakiwemo viongozi wa dini sasa wanaanza kupukutika kutoka kwenye mstari wa siri huku baadhi yao wakikimbilia nje ya nchi kufuatia oparesheni kali inayofanywa na Kikosi cha Kupambana na Kudhibiti Madawa ya Kulenya Tanzania kuwanasa kila kukicha, Uwazi lina mchoro kamili.Hivi karibuni kikosi hicho kimemkamata askofu (mwangalizi mkuu wa kanisa) aliyetambulika kwa jina la Emeka Nwachukwu Mert raia wa Nigeria ambaye ana kanisa la kiroho maeneo ya Sinza jijini Dar.
Jina la kanisa hilo limedhibitiwa na vyombo husika kwa sababu ya uchunguzi zaidi na uhalali wake wa kuwepo nchini. 
Vyanzo vyetu makini ndani ya kikosi kazi vinaeleza kwamba, mchungaji huyo alikamatwa Oktoba 31, mwaka huu saa kumi usiku Tegeta wilayani Kinondoni, Dar es Salaam akiwa na madawa ya kulevya ‘unga’ aina ya heroine kilo 35. 
KAMA UNGEINGIA SOKONI
Habari za ndani kutoka kwenye oparesheni hiyo zinasema kuwa, endapo unga huo ungeingia sokoni na kununuliwa, basi mtumishi huyo wa Mungu angevuna kitita cha zaidi ya shilingi bilioni mbili.
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment