-->

DONDOO ZA AFYA:MAKALA MAALUMU KWA WAGONJWA WA KISUKARI


 Wagonjwa wengi wamekuwa wakishauriwa na watumishi wa afya kuwa pindi tu anapogundulika kuwa ana ugonjwa wa kisukari au shinikizo la damu basi yeye anakuwa ni muhangwa wa dawa hadi pale atakapo kufa na anashauriwa kuwa dawa hizi ndio mkombozi na moyo unaolinda maisha yake. Je leo ningependa nizungumze kuhusu hiki kitu na kujaribu kuangalia nini hasa tunatakiwa kuwa shauri wagonjwa wetu na sio kuwa karirisha fikra potofu zinazojengeka kwenye ubongo na hatimaye kuendelea kudhoofika miili yao na hatimaye kifo. Inasemekana kuwa hadi sasa dakatri pia ni chanzo cha aina ya tatu ya kisukari ambacho hujulikana kama "DOCTOR INDUCED EXACERBATION DIABETES," aka DIE hii ni kutokana na kutojua nini hasa chanzo au mzizi wa ugonjwa wa kisukari na kuwa na fikra finyu kuwa dawa pekee ndio suluhisho na kudharau upande wa pili kuwa hauna manufaa bila kufanya utafiti. Ugonjwa wa kisukari ni moja wapo wa magonjwa yanayo sababishwa na maisha tunayo ishi kila siku hivyo ijulikane kuwa asilimia kubwa ya tiba yake ni kwa kutumia lishe na sio dawa za kisukari. Wengi wetu watumishi wa afya hatuwezi kuwa elekeza wagonjwa wetu namna ya kutubu ugonjwa huu kwa kutumia vyakula vyetu vya majumbani bali wengi tuna egemea upande wa kutoa dawa tu tukiwa na fikra kuwa dawa ndo suluhisho la ugonjwa huu ukisahau kuwa huu ni ugonjwa tabia. Leo napenda niwa eleze kidogo kuhusu ugonjwa huu wa kisukari na nini kisababishi cha kuongezeka kwa ugonjwa huu kwani kulingana na TANZANIA WHO WEBSITE takwimu zinaonesha kuwa mwaka 2008 watu 757000 wanaume na wanawake 588000 walikuwa na magonjwa ya kisukari na magonjwa ya moyo. Idadi ya vifo kwa wanaume wenye kisukari inakadiliwa kuwa ni asilimia 42.8 kwa wanaume na asilimia 28.5 kwa wana wake. Swali la kujiuliza ni karibia nusu ya wagonjwa wenye kisukari wanakufa kutokana na huu ugonjwa. Je ni kweli wagonjwa wengi wanapuuzia kunywa hizi dawa au wagonjwa hawa hawahudhurii clinic za kisukari? Jibu ni hapana!! Hii inatokana na mfumo mbaya kuwa wagonjwa wetu hatuwafundishi namna gani ya kutumia lishe ya mimea na matunda kama tiba kwani watumishi tumekuwa tukiwapotosha watu kuwa dawa pekee ndo suluhisho na kusahau kuwa dawa hizi za kitaalamu zinasababisha mgonjwa kupatwa na maudhi mbali mbali ambayo mara nyingi ndio kisababishi kikubwa cha vifo. Ningependa mimi na wewe tuweke juhudi na namna nzuri ya kuhakikisha jamii inapata elimu ya kutosha ya magonjwa haya na kujua namna gani anaweza kuacha kabisa kutumia hizi dawa na kuanza kurekebisha mlo wake tu. Mie siku zingine nawaza sana kuhusu magonjwa haya na hakuna kitu kinachomaliza nishati ya mwili wangi kama kuwaza magonjwa tabia. Mimi binafsi ningependa kukushauri kuwa watu wengi tunaangamia kwa kukosa maarifa na wale wenye maarifa wanao atamia ndio mungu atawaangamiza kwa mara ya kwanza. Kwani najua hukumu ya kwanza itakuwa ya shetani na hukumu zingine ni kwa wachungaji na wanaofahamu neno na wanapuuzia. Hivyo tusikose maarifa tukae chini tuelezane nini kazi ya idara hizi mbili TIBA ASILI NA TIBA MBADALA nina imani ubora wa huduma wa hawa watumishi ndio inafanya waendelee kuwa na mafanikio. Kwani kuna usemi unasema PHYSICIAN KNOWS A LOT BUT HAS NOTHING TO DO TO THE PATIENT.


Ndg msomaji ungana nami katika makala yangu ya leo kwani nimeongea mengi kuhusu fikra potofu ya wanajamii kuhusu magonjwa haya Kwa kifupi kuna aina kuu mbili za ugonjwa wa kisukari ambazo nitazichambua kwa kifupi hapa ndugu msomaji wangu. Kisukari aina ya kwanza ambayo husababishwa na kichocheo cha insulin kutotolewa ipasavyo ili kuja kuhifadhi sukari iliyozidi kwa matumizi ya baadae. Hii inatokana na seli ambazo zinatengeneza insulin kutoka kwenye kongosho ambazo huitwa beta seli za islets of langer hans kushambuliwa na chemikali za mwili yani antibodies ambazo hutengenezwa na mwili wenyewe na hatimaye huanza kushambulia seli za mwili wenyewe tunaita AUTO IMMUNE DISORDER. Magonjwa haya hadi sasa chanzo chake hakijajulikana nini kinachosababisha seli hizi kushambuliwa. Ingawaje tafiti mbali mbali hufanywa na kutoa matokoe mengi. Tafiti iliyo fanywa kwa kutumia miaka mingi sana na profesa COLIN CAMPBELL ilijaribu kuangalia madhara ya mama kutumia maziwa ya ngombe kumnyonyesha mtoto anapokuwa bado yuko mchanga. Utafiti huu ulionesha kuwa ndani ya maziwa kuna protein iitwayo casein ambayo ni protini ngumu haiwezi kufanyiwa kazi kiurahisi na mwili na hivyo mfumo wa chakula huanza kubambana na hiyo protein na hatimaye kusababisha kuvimba kwa kuta za mfumo wa chakula yani INFLAMATION kisha kusababisha kuvia kwa hiyo protini kwenye mzunguko wa damu hatimaye kusababisha SYSTEMIC IMFALAMATION. Mwili hutengeneza chemikali ziitwazo antibodies kwa madhumuni ya kuiondoa hiyo casein kwenye damu lakini aina hii ya protein inafanana sana na B cells nina maanisha genomic structure yake. Hivyo basi badala ya hiki kilinda mwili kutengenezwa huanza kushambulia seli za kutengeneza insulin B cells badala ya kuindoa aina hiyo ya protein. Hivyo basi watoto wengi waliokuwa wakitumia maziwa tangu alipozaliwa walionekana na ugonjwa huu wa kisukari aina ya kwanza ndani ya miezi 7. Hivyo hizi ni tafiti za watu hata wewe unaweza kufanya hivyo basi sikushauri kuwa maziwa ni mabaya bali chukua hatua. Pia tafiti nyingi zimefanywa kuwa chakula kinacho athiri mfumo wa chakula kinaweza sababisha mpambano na hatimaye kusababisha kisukari aina hii bila kusahau tafiti nyingi kuwa upungufu wa vitamin D huweza kusababisha kuharibiwa kwa B seli. Aina hii ya kisukari hutokea utotoni kuanzia miezi 7 hadi miaka 20. Hivyo ni jukumu letu kuendana na tafiti na kujua tuan enda wapi katika taasisi ya afya. Nina imani jamii haijaeleimishwa ila serikali na wizara ina fahamu umuhimu wa tiba hizi zinazotibu chanzo cha tatizo na sio dalili ndio maana hadi sasa ninavyo andika hii makala Tanzania kuna taasisi ya tiba asili TANZANIA INSTITUTE OF HERBAL MEDICINE kipo muhimbili chuo kikuu kinatoa masters degree na kozi mbali mbali za muda mfupi. Nashukuru kwa juhudi za serikali kwa kutambua dunia hii inaelekea wapi kwani Tunachotaka ni kuikomaza hii idara ili tufikie kiwango walichofikia nchi zilizo endelea. Tiba ya kisukari aina ya kwanza hadi sasa bado ni changamoto kwani utafiti unasema ni kujaribu kuepuka vitu vyote ambavyo husababisha kushambuliwa kwa B seli za kongosho. Kisukari aina ya pili huu ni ugonjwa sugu wa lishe. Unaitwa ugonjwa sugu wa lishe ni kwa sababu huanza kutoa polepole mwilini na hatimaye kushamiri na kuanza kuonesha dalili. Ugonjwa huu husababishwa na kichocheo cha insulin kutofanya kazi yake ipasavyo. Unachotakiwa ujue kuwa kisukari aina hii ni kuwa beta seli za kongosho zina uwezo wa kutoa insulin vizuri kabisa hivyo insulin sio tatizo; tatizo linatokea pale insulin iliyo tolewa haiwezi kufanya kazi kwani kuna kizuizi ambacho kinasababisha mwili kutotambua kuwa kuna insulin ya kutosha kwenye damu.


Swali la kujiuliza je insulin inafanya kazi gani? Na je nini kinasababisha insulin isifanye kazi? Na nini tunachokifanya watumishi wa afya kuhusu kisukari na tunacho amini na kuwaambia wagonjwa wetu!



JIBU Tumekuwa tukifundishwa darasani kila siku kuwa kichocheo cha insulin kazi yake kubwa ni kushusha sukari yani kupunguza sukari kwenye damu. Nadhani wengi mnafahamu hili kuwa husawazisha sukari kwenye damu na tiba zetu zinalenga kuishusha sukari hii ipungue. Ni dhahiri kuwa dhana hii inafanya jitihada ya kisukari kupona ni kazi na itakugharimu kutumia dawa hizi miaka na miaka. Ukweli ni kwamba insulin inafanya kazi ya kuhifadhi nishati ya mwili iliyo zidi yani glucose kwa matumizi yake ya ziada pale itakapo hitajika. Hivyo mungu aliona hili kwamba kama wewe umekula chakula na sukari ikazalishwa nyingi kwenye damu hivyo atengeneze kichocheo ambacho kazi yake kubwa ni kuhifadhi nishati kwa matumizi ya baadae. Hivyo basi kwa kusema hivyo napenda kukuambia kuwa kisukari ni ugonjwa wa insulini na leptin kushindwa kufanya kazi na sio ugonjwa wa sukari kuwa nyingi kwenye damu. Kwa maana hiyo utaaona dawa nyingi hizi za kitaalamu zinalenga kushusha sukari na kuacha tatizo likiwa halija shughurikiwa! Hii ni kutokana na dhana na fikra potofu kuwa sukari ni ugonjwa wa sukari nyingi kwenye damu. Pia inafikia hatua mbaya kabisa kwa miongoni mwa watumishi mgonjwa anapewa sindano za insulin huku akiwa na kisukari aina ya pili! Inasikitisha kuona kitu kama hiki kinafanyika. Kisukari aina ya pili inasababishwa na insulin kushindwa kufanya kazi yake ipasavyo kushindwa huku kunafanya insuli kiwango chake kwenye damu kuongezeka. Je nini sababu tena ya kumpa mgonjwa wako insulin wakati imo imezidi kiwango na haiwezi kufanya kazi? Kabla zijaongea mengi kuhusu kitendo cha kutoa sindano za insulin kwa wagonjwa wa kisukari aina ya pili napenda tuongelee kwanza visababishi vya insulin kushindwa kufanya kazi. 1. Ulaji wa vyakula vya viwandani vyenye sukari nyingi hasa vyakula vyenye sukari aina ya fructose. Kwani aina hii ya wanga husharabiwa haraka sana na seli za mwili na hatimaye kutengeneza sukari nyingi mwilini yani GLUCOSE. Sukari inapokua nyingi insulin hutolewa kwa wingi kuja kuhifadhi sukari iliyozidi yani nishati hii kwa matumizi ya ziada. Hivyo basi insulin huhifadhi nishati ya ziada katika mfumo wa mafuta na wanga aina ya glycogen kwa matumizi yake ya baadae. Mwili unafanya hivi ni kama katika kipindi cha njaa watu huhifadhi vyakula kwa matumizi ya baadae ili wasije kufa na njaa kali kwani akiba itakuwepo. Hivyo ulaji ovyo wa vyakula hivi unasabaisha insulin kuwa juu wakati woote kwenye damu na hatimaye kusababisha insulin kutofanya kazi. Ni sawa na wewe ukiingia kwenye chumba chenye harufu kali sana utasumbuka kwa muda baada ya muda unazoea yani unaona ni harufu ya kawaida tu. Ndivyo na insulin utolewaji wake ukizidi kinachofanyika kwamba inafikia hatua insulin haiwezi kufanya kazi tena. Baada ya insulin kuhifadhi nishati ya ziada kwa matumizi ya baadae katika mfumo wa mafuta hizi seli za mafuta hutengeneza kichocheo kiitwacho LEPTIN ambacho hutolewa na seli zinazohifadhi mafuta yani kwa FAT CELLS. Kazi kubwa ya leptin ni kutoa taarifa ni kiasi gani ya chakula unatakiwa ule, upate chakula muda gani na kukupa hamu ya kula chakula yani appetite. Unatakiwa kufahamu kuwa kadri insulin inavyo hifadhi mafuta haya ndivyo na leptin hutengenezwa kwa wingi na utengenezwaji wa kiasi kingi wa leptin unasababisha leptin kushindwa kufanya kazi yake ipasavyo. Ni sawa na mfano wewe ukikaa katika chumba chenye harufu mbaya baada ya muda mfupi unazoea hiyo harufu mbaya. Hivyo basi kushindwa kufanya kazi kwa hiki kichocheo kinafanya mtu huyu muda wote anakuwa na njaa kali,hamu ya chakula kali, kula sana na kula mara kwa mara. Hivyo basi kisukari ni ugonjwa wa insulin na leptin kutofanya kazi ipasavyo na sio ugonjwa wa sukari nyingi kwenye damu. Kwani ni dhahiri kuwa maelezo yangu hapo juu utashangaa kuwa kama insulin haifanyi kazi yako kutokana na kizuizi ni kwa nini mtu huyu anaongezewa tena insulin kwenye damu? Ni hatari kwa afya yako na ni dhahiri kuwa chakula ni tiba hujafundishwa nini kifanyike ili ukitumie kama tiba. Endelea kutumia kama unatumia lakini angalia njia mbadala ambayo inaweza kukusaidia na hatimaye tatizo lako liishe kabisa inawezekana kabisa weka imani.

Watu wengi sana vyakula hivi vime waathiri kwani asilimia kubwa ya watu hadi sasa wana dalili mbaya zenye kuhatarisha mwili zinatokana na kutumia sukari nyingi mwilini tunaita METABOLIC SYNDROME. Hii ni kikundi cha dalili zifuatazo,sukari kuwa nyingi kwenye damu,nyama uzembe yani belly fat,uzito kupita kiasi, na insulin kutofanya kazi. Hizi ni moja wapo ya dalili zinazo sababishwa na kiwango cha insulin kuwa juu. Hivyo kitendo cha kupewa sindano za insulin ni dhahiri kuwa tatizo linaongezeka kwani insulin na glucose sio tatizo kwani tatizo ni insulin kutofanya kazi kutokana na kizuizi 2. Pia vyakula vya mafuta mabaya vyenye wingi wa cholesterol mbaya. Ifahamike kuwa cholesteral sio mbaya kabisa kwani inafanya kazi kubwa ya kutengeneza seli za mwili. Lakini unatakiwa kujua kuwa mwili wetu una uwezo wa kutengeneza cholesterol kutoka kwenye ini kwa silimia tisini hivyo unatakiwa kutambua kuwa unahitaji kiwango kidogo sana cha cholesterol kupitia kula. Hivyo punguza vyakula vya nyama kwani vina cholesterol mbaya nyingi,vyakula vilivyo kaangwa kwa kutumia mafuta na hivyo kula sana mafuta mazuri yanayo patikana katika mimea kama karanga,parachichi,nazi,na sio bidhaa za wanyama. Mafuta mabaya ni chanzo kikubwa sana katika kusababisha kizuizi cha insulin kutofanya kazi kwenye vipokea insulin. Na hivyo huwezi kutibu kisukari hadi haya mafuta mabaya yaondoke hivyo dawa zote hizi za kitaalamu hushughurika na kushusha sukari kwenye damu ambayo ni dalili na sio mzizi wa tatizo. ASANTENI SANA WOTE MLIOSOMA MAKALA YANGU HII TIBA PEKEE YA KISUKARI NI KUBADILI MITAZAMO POTOFU KUHUSU UGONJWA HUU NA KUANZA KUPAMBANA NA HUU UGONJWA KWA KUTUMIA LISHE ILIYO TENGENEZWA KWA KURUDISHA AFYA YAKO UNGANA NAMI DR MKUMBO K BOAZ FACEBOOK; KB MKUMBO SKYPE: YOUNGKINGBOAZ BLOG: www.doctorboaz.blogspot.com FACEBOOK PAGE : MKUMBO NEPTUNUS COMPANY LTD NUTRITIONAL HEALTH COACH   FOOD IS MEDICINE https://m.facebook.com/HELIETH4GYNAECOLOGIST4CLINIC?ref=bookmark
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment