Helkopta
aina ya Chopa iliyoanguka maeneo ya Kipunguni B Ukonga jijini Dar es
Salaam, leo asubuhi na kuua watu wanne waliokuwemo akiwa ni rubani
pamoja na askari watatu.
Miili ya watu waliokuwemo kwenye helkopta hiyo ikiwa imekandamizwa na mabaki ya chopa hiyo.
Sehemu ya mashuhuda wa maeneo hayo wakishuhudia ajali hiyo.
Helkopta
inayosemekana inamilikiwa na TANAPA imeanguka na kuteketea kwa moto
katika eneo la Kipunguni B Ukonga jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
Kwa
mujibu wa mashuhuda, wamesema waliona helkopta hiyo ikipoteza uelekeo
na badaye kuanguka chini hali iliyosababisha kishindo kikubwa baada ya
kulipuka moto.
Inasemekana ndani ya helkopta hiyo kulikuwa na watu wanne ambao wote wameripotiwa kufariki dunia.
Aidha imeelezwa kuwa katika ajali hiyo kulikuwamo na Askari 3 na rubani
0 comments :
Post a Comment