-->

MCHEZAJI MPYA WA YANGA ANAYEITWA EMMERSON AANZA MAZOEZI

Kiungo mpya wa Yanga kutoka nchini Brazil, Emerson de Oliveira (wa pili kutoka kulia) akiwa mazoezini na wachezaji wenzake jana asubuhi katika uwnaja wa shule ya sekondari Loyola, wengine kutoka (kushoto) ni Hussein Javu, Hamis Kiiza, na (kulia) ni Andrey Coutinho.
****************************************************
Baada ya Kiungo huyo kabaji kuwasili nchini juzi kutoka nchini Brazil, Emerson de Oliveira Neves Roque jana asubuhi ameanza rasmi mazoezi mepesi katika Uwanja wa shule ya Sekondari Loyola kufuatia kusafiri kwa zaidi ya masaa 11 kutoka jijini Rio de Janeiro.

Emerson ameungana na wachezaji wengine wa Young Africans katika mazoezi hayo jana asubuhi ikiwa ni siku yake ya kwanza katika ardhi ya Tanzania na kufanya mazoezi mepesi mepesi chini ya kocha msaidizi Leonardo Neiva kuijiweka fiti na kutoa uchovu safari.
Kiungo huyo mwenye umbo lililonyumbulika alikuwa akikipiga katika timu ya Bonsucesso FC iliyopo ligi daraja la pili nchini Brazi katika jiji la Rio de Janeiro pia msimu uliopita alikua akicheza soka la kulipwa katika nchi ya Poland latika klabu ya Piotrkow Trybunalski FC.
Kocha mkuu wa Yanga, Marcio Maximo, alisema kuwa mchezaji huyo alikua na programu ya mazoezi mepesi tu kutokana na uchovu wa safari na leo anatarajiwa kuendelea na mazoezi na wenzake kulingana na ratiba iliyopo.
Endapo Emerson atafanikiwa kulishawishi benchi la Ufundi kumsajili basi moja kwa moja ataingia makubaliano na klabu ya Yanga kwa ajili ya kuitumikia kwenye michuano ya kimataifa na Ligi Kuu ya Vodacom Tanznaia bara. Picha kwa hisani ya Mtandao wa Yanga
BOFYA HAPA KUSOMA HABRI NYINGINE ZA MICHEZO
                                        BUSTANI YA MICHEZO
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment