BARAZA KUU LA WAISLAMU TANZANIA (BAKWATA) limekuwa likimtumia messege na
simu za vitisho Mbunge wa Konde Pemba, Mh Khatib Said Hajj, kufuatia
shutma aliyoitoa Mbunge huyo Bungeni 11/10/2014, kwa BAKWATA na serikali
kutokana na ukimya juu ya malalamiko ya udhalilishaji wa vyombo vya
dola kwa masheikh waliotolewa Zanzibar na kupelekwa Tanzania Bara kwa
tuhuma za ugaidi wakiwa mahabusu
Moja ya ujumbe aliyotumiwa Muheshimwa huyo ni hii
↪” Tunaskitishwa Sana kwa kitendo chako ulichokifanya Jana katika bunge la jamhuri ya muungano ya Tanzania
Wewe ukiwa mbunge muislam haikuwa sahihi kukisema Chombo cha waislam Bakwata kuwa ni Chombo cha kinafiki na baya zaidi kuisema jumuiya hii kuwa ni Moja Kati ya taasisi ya za CCM kama ilivyo jumuiya ya vijana ya CCM.
Na baya zaidi wewe ukiwa ni muislam kuliomba baraza kuu la maaskofu kuwatetea masheikh eti wanaodhalilishwa katika magereza ya Tanzania bara.
Jambo ambalo Halina uthibitisho wowote Bali ni maneno ya mitaani uliyokubali kulishwa nawe ukayameza bila kujitambua.
Sisi kama taasisi ya kiislam inayotambuliwa kisheria na serikali yetu tukufu tunakulaani sana kwa kuikashifu Bakwata na tunaandaa Taratibu za kisheria kupitia wanasheria wetu kuona hatua za kuchukua dhidi yako ili iwe fundisho kwako na wale wote wenye tabia za kuidhakilisha jumuiya hii ya waislam Tanzania
Wabillah tawfiq
Sisi vijana wa Bakwata
Kny sheikh wa mkoa wa Dsm shk Alhad Mussa salim,”↩
Kwa upande wake Mh Khatib kwa ujasiri mkubwa akawajibu kwa kuwatumia ujumbe huu
↪”Mukienda mahkamani mutanikuta nimeshafika nawasubiri
Nilisema bungeni kila mtu ameona na nyinyi kama taasisi inayojiamini Semeni au jibuni hadharani waislam watapima wataamua Nani mkweli au muongo
Hii ya kunitumia sms kwangu nahisi ni ishara ya woga mumewatawala! Niwahakikishie tu mimi najiamini na Allah pekee Ndio tegemeo langu
Allah aalam!↩
SOURCE:MUNIRA BLOG

0 comments :
Post a Comment