Gavana wa mji wa Makkah Mishal bin Abdulllah kwa niaba ya msimamizi wa misikiti miwili mitakatifu Mfalme Abdullah wa Saudi Arabia jana aliongoza shughuli za ufanyaji usafi wa Al Qa'aba.
Katika ufanyaji usafi huo mabalozi wa nchi mbalimbali, mawaziri, wanazuoni wa kiislamu, wanadiplomasia na watu mbalimbali walihudhuria.
Tukio la usafishwaji wa Al Qa'aba hufanyika mara mbili kwa mwaka. Hufanyika mwezi 9 Dhul hijjah kwa kuveshwa
kiswa (covering) kipya na mara ya pili hufanyika mwezi 15 Shabaan.
Balozi
wa Afrika kusini Muhammad Sadiq Jaafar ambaye alihudhuria alisema
aliona ni heshima kubwa kwa kushiriki katika kuosha Al Qa'aba.
"Hii ni mara ya tano Mimi kupata bahati na heshima ya kutosha Al Qa'ba", alisema.
Nae Balozi wa Bangladesh Mohammed Shahidul Islam alisema anashukuru kwa mamlaka kumpa nafasi tena ya kuwepo katika jambo tukufu katika dini. Hii ni mara yake ya tisa mfululizo kushiriki sherehe za Uoshaji wa Al qa'aba.
Abdul
Hameed Mohamed Fowzie ambaye ni Waziri wa mambo ya Miji nchini Sri
Lanka naye alihudhuria baada ya kupata mualiko kutoka kwa Waziri wa
mambo ya Hijjah wa Saudi Arabia Bandar Hajjar.
Kabla
kuosha na kusafisha Al Qa'aba huanza kufanya tawaf kwa kuzunguka Al
Qa'aba mara saba na kisha kusali rakaa mbili za sunna ndani yake.
Waoshaji huingia ndani ya Al Qa'aba kwa kusafisha kuta za ndani kwa maji safi na kutumia vitambaa vyeupe.
Kisha
huchukuliwa maji ya Zamzam yaliyochanganywa na manukato ya waridi
(rose), Udi (oud) na miski hutumika kupangusia sakafu. Hatua hiyo
hutumika mikono na majani ya makuti.
SOURCE:AHBAABUR BLOG
About Omari Makoo
0 comments :
Post a Comment