Vijana
wa wanaounda jimbo la Kawe kwa pamoja wameanzisha kampeni ya kupinga
maambukizi ya VVU katika jimbo lao kwa kufanya matamasha ya wazi yenye
lengo la kuwaamasisha vijana faida za kujua afya zao mapema na jinsi ya
kujikinga na maambukizi ya VVU.
Zikiwa zimebaki siku chache kwenda kwenye tukio la kuazimisha siku ya
UKIMWI duniani ambayo kwa kawaida ufanyika kila mwaka inapotimu tarehe
01- 12, hivyo vijana kutoka jimbo la Kawe wameunganisha nguvu zao za
pamoja wakishilikiana na wananchi wa jimbo la Kawe, watafanya hitimisho
ya kampeni yao yenye kauli mbiu "
JIMBO LA KAWE MAAMBUKIZI YA VVU SASA BASI"
TUKIO LITAFANYIKA KATIKA VIWANJA VYA TANGANYIKA PACKERS SIKU YA 01 - 12 -2014
|
Mhe; Ayubu Tesha (SMG) |
|
Mhe: Diwani wa kata ya Kawe, Ndugu Othman Kipeta |
|
Mhe; Ayubu Tesha (SMG) akitoa taarifa mbele ya wwaandishi wa habari |
|
Wana kamati wakisubiri kufanya maojihano na waandishi wa habari |
|
Wanafunzi wa Sekondari Bunju A wakifanya maigizo yanayohusu ugonjwa wa UKIMWI |
|
Mhe: Diwani akitoa ufafanuzi wa kampeni hiyo |
|
Mhe: Lilian Mkotani |
|
wasanii wa Kawe Unit |
|
Picha ya pamoja na mfadhili wa kampeni |
Wanafunzi wa shule ya msingi Bunju A
0 comments :
Post a Comment