-->

LOWASA AIKANA AKAUNTI YA TWITTER INAYOTUMIA JINA LAKE

Dar es Salaam. Waziri mstaafu, Edward Lowassa amekanusha taarifa mbalimbali zinazoenezwa na mitandao ya kijamii kuhusiana na mjadala wa wizi wa fedha za Akaunti ya Tegeta Escrow Sh306 bilioni.
Taarifa kwa umma kutoka ofisi ya Lowassa ilisema tangu Bunge lilipoanza mjadala wa wizi huo wa fedha Novemba 26 mwaka huu kuna mtu au kikundi la watu wameanzisha akaunti ya mtandao wa ‘Twitter’.
Ilisema akaunti hiyo imepewa jina la Edward Ngoyai Lowassa,@edwardlowasa ambayo hana uhusiano nayo.
“Tunawaomba wananchi kupuuza yote yanayoandikwa katika ukurasa huo. Watanzania tuachane na tabia ya matumizi ya mitandao ya kijamii kupotosha umma, ” ilisema taarifa hiyo.
Ilisema kwa kutumia ukurasa huo, mtu huyo amekuwa akiandika masuala kadhaa kuhusiana na suala hilo la Akaunti ya Escrow na kile kinachoendelea bungeni, ikionekana kama ni kauli ya Lowassa.
Akaunti hiyo ilisomeka “Richmond hadi natimuliwa hakuna senti iliyokuwa imeibiwa, lakini hakuna aliyesimama kunitetea, leo watu wanatetea wizi wa waziwazi.
BOFY HAPA KUSOMA HABARI NYINGINE ZA SIASA
                                         UWANJA WA SIASA
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment