Mwenyekiti
Mtendaji wa Kampuni ya Kufua Umeme ya Independent Power Tanzania
Limited (IPTL), Harbinder Sigh Seth (kushoto) akikabidhi mfano wa hundi
yenye thamani ya shilingi Milioni 20 kwa Mwenyekiti wa Chama cha
Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), Juma Pinto (wapili
kulia) ikiwa ni mchango wa IPTL kusaidia maandalizi ya Tuzo za
wanamichezo bora nchini. Wanaoshuhudia kutoka kushoto ni ni Makamu
Mweyekiti wa TASWA, Egbert Mkoko, Katibu Mkuu, Amir Mhando na
Mwanasheria na Mshauri Mkuu wa IPTL,Joseph Makandege na kulia ni Mjumbe
wa TASWA, Rehure Richard Nyaulawa.
Mwenyekiti wa TASWA, Juma Pinto akizungumza na wanahabari baada ya kupokea fedha hizo.
Mwenyekiti Mtendaji wa
Kampuni ya Kufua Umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL),
Harbinder Sigh Seth akiwaeleza wanahabari furaha yake ya kuisaidia TASWA
kitita hicho cha fedha kusaidia wanamichezo ambapo nae alikiri kuwa ni
miongoni mwa wanamichezo na amewahi kuwa Mshindi wa tatu wa Mbio za
Magari Afrika.
Mwenyekiti Mtendaji wa
Kampuni ya Kufua Umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL),
Harbinder Sigh Seth (katikati) akiwaongoza wanahabari kuangalia mitambo
ya Kampuni hiyo ambayo inazalisha umeme. Kulia ni Katibu mkuu wa TASWA,
Amir Mhando na Kushoto ni Mwenyekiti wa TASWA, Juma Pinto.
Waandishi wa habari wakiingia kuangalia uzalishaji wa umeme katika mitambo ya IPTL.
SOURCE:DEWJIBLOG
SOURCE:DEWJIBLOG
0 comments :
Post a Comment