-->

MUHAADHIRI WA CHUO KIKUU CHA KIISLAM MOROGORO AFARIKI DUNIA

Muhadhiri wa chuo kikuu cha kiislam Morogoro aitwae Jaffar Siraj amefariki dunia jana usiku katika hospitali ya Muhimbili.Ustadh Jaffar Siraj aliugua toka 2012 na kupata matibabu ndani ya nchi huku vipimo vya hospitali ya Muhimbili vikionyesha kwamba ana TB akatumia dozi ya Tb pasina mafanikio ndipo wazo la kusafirishwa kupelekwa India lilipokuja mnamo  september 2013 ndipo alipoanza safari ya kuelekea India kwa ajili ya matibabu.Alisindikizwa Nchini India na rafiki yake kipenzi Said Jaff huko iligundulika kwamba mapafu yake yamejaa maji hivyo akafanyiwa upasuaji na kutolewa maji hayo kwenye mapafu.Alirejea nchini na kuendelea kupata matibabu huku akiripoti muhimbili katika kipindi cha miezi sita baada ya upasuaji kutokea India.Hali yake ilianza kutengemaa na kuanza kufanya majukumu yake madogo madogo na baadae kurejea kazini na kuendelea na harakati za daawa ambazo amekuwa akizifanya kipindi chote cha Uhai wake.
Marehem Jaffar Siraji alifariki dunia jana usiku katika hospitali ya Muhimbili baada ya kusumbuliwa na maumivu makali ya kichwa
Jaffar Siraj alisoma hotba na kujumuika na waislam kwenye EID DHUHA katika viwanja vya K/NDEGE.
Jaffar Siraji atakumbukwa kwa wasikilizaji na watazamaji wa Radio Imaan na Tv Imaaan kwenye kipindi cha MWANGAZA WA JAMII
Al akhy Jaffar Sirak katika zama za uhai wake
Historia inaonyesha Jaffar Siraj alisoma elimu ya stashahada katika chuo cha kiislam cha Ubungo Islamic Teacher's College ambako alihitimu mwaka 2004 na kisha akasomesha Msamala Muslim Songea na baadae Matangini Islamic Dar, akajiunga na Chuo cha Waislamu Morogoro wakiwa ndio Batch ya mwanzo 2005. Baada ya kuhitimu alichaguliwa kuwa Mhadhiri Msaidizi na mwaka mmoja baadae alijiunga na Chuo kikuu cha Dar es Salaam kwa ajili ya Shahada ya Uzamili na kurejea MuM ambako amekuwa akifanya kazi mpaka mauti yalipomkuta.
Pia Al akhy Jaffar Siraj alikuwa ndio kiongozi wa  umoja wa wanafunzi waliomaliza chuo kikuu cha waislam morogoro
Watu mbali mbali pamoja na uongozi wa radio imaan na chuo kikuu cha waislam wamemtakia mapumziko mema Al akhy Jaffar Siraji


Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment