Rais
uhuru Kenyata ameendelea kujizolea umaarufu mkubwa nchini Kenya
kutokana na matukio mengi anayoyafanya, mengi yakiwa yale ambay ni mara
chache sana kumuona rais akifanya. Mfano ni kama lile tukio la kutoka
ikulu akiwa hana bila ya walinzi, kucheza mziki katika matamasha
mbalimbali na lile la kusimamisha msafara wake kisa tu anunue karanga.
Jipya alilolifanya
siku ya jana ni pale alipoamua kutumia usafiri wa Matatu au kwetu
tunaita Daladala kwenda mjini. Inasemekana Rais Kenyata ndio rais wa
kwanza ktumia usafiri huo akiwa madarakani, marais wote waliopita
hawajawahi kuutumia wakiwa madarakani. Kikubwa kingine alichosema na
kimeungwa mkono na vijana wengi ni kuruhusu Daladala kuchorwa Graffit
jambo ambalo limekua likizuiliwa na uongozi nchini humo kwa mda sasa.
Rais Kenyata alisema ” To be frank why are we interfering with graffiti
on Matatu? Let us promote our young people – Uhuru Kenyatta ”
SOURCE:AFRICAN MISHE
0 comments :
Post a Comment