Aliyekuwa mhadhiri wa chuo kikuu cha waislam Morogoro Ustadh Othaman Mjinga amefaiki dunia usiku wa tarehe 5 na kuzikwa tarehe 6 baada ya swala ya adhuhuri.
Ustadh Othaman Mjinga alikuwa mhadhiri wa somo la Kiarabu katika chuo kikuu cha waislam Morogoro ambaye alifanikiwa kupata elimu yake ya shahada nchini Sudani.Hata hivyo Othamani Mjinga alikuwa yupo kwenye hatua za mwisho za kupata shada yake ya uzamivu(PHD) yaani alikuwa anakaribia kuitwa Dr kutokana na elimu aliyokuwa nayo.
Ustadh Othamani Mjinga atakumbukwa kwa daawah yake iliyojaa falsafa katika kipindi cha uhai wake.
Pia Ustadh Othmani Mjinga alikuwa akisikika mara kadhaa kwenye vipindi vya dini ya kiislam vya radio na tv abood pia kuna wakati aliwahi kuitwa kuzungumza tv Imaan.
Miaka yote amekuwa akihimiza umoja wa waislam na kupinga utengeano.
Kuhusu kifo chake:Ustadh Othmani Mjinga alizidiwa ghafla nyumbani kwake kiasi cha mkewe kuomba msaada kwa ndugu na jamaan kumpleka hospitali.Repota wetu anahadithia kwamba wakati anachukuliwa kupelekwa hospitali alionyesha kuwa ni mtu mwenye kupata nafuu ingawaje hali ilibadilika walipofika mapokezi na baadae kufariki akiwa hapo hospitali ya mkoa wa Morogoro.
Mazishi yake:Mazishi ya ustadh Othamani Mjinga yamefanyika mkoani Morogoro ambako alisaliwa katika msikiti wa MUSLIM UNIVERSITY OF MOROGORO na kisha kwenda kuzikwa katika makaburi Kola baada ya swala ya adhuhur.Ustadh Othamani Mjinga zama za uhai wakeMarehem Ustadh Othamani Mjinga akiwa pamoja na Shekh Filambi na mhadhiri msaidizi wa kwenye kitengo cha mawasiliano ya umma Salim Said
0 comments :
Post a Comment