Vita ya kusaka urais
nchini Zimbabwe imeingia katika hatua nyingine baada ya ndugu watatu wa
familia ya aliyekua Rais wa nchi hiyo Michael Sata akiwemo mjane wake
Christine Kaseba kuchukua fomu ya kugombea nafasi hiyo katika uchaguzi
mdogo kupitia chama tawala.
Mjane huyo ameungana na
mtoto wa kiume wa Marehemu Sata aitwaye Mulenga Sata mwenye miaka47
ambaye pia ni meya wa jiji la Lusaka na binamu yake Milen Sampa mwenye
miaka44 ambao wote wamethibitisha kuwania nafasi hiyo ya juu katika
uchaguzi utakaofanyika Januari2o mwakani.
Mjane huyo alisema bado
anaomboleza kifo cha mumewe ambaye alizikwa wiki iliyopita na kwamba
kitendo cha kuona kazi alizoanzisha mumewe hazikukamilika,zinaiumiza
nafsi yake hivyo kuamua kuwania urais ili aziendeleze.
“Maumizu ninayoyapata
yatakua ya bure ikiwa sitatimiza ndoto za Rais Sata alizopanga kufanya
akiwa madarakani”Mjane huyo alikaririwa na kituo kimoja cha redio nchini
humo.
0 comments :
Post a Comment