"Kisheria kuna kitu kinaitwa utawala bora ambao unajengwa kwa misingi ya
Maamuzi ya Sheria (Rule of Law), Mgawanyiko wa Madaraka (Seperation of
Powers), Ukubwa wa Bunge (Parliamentary Supremacy) na Uhuru wa Mahakama
(Independence of Judiciary). Hivi vyote ni kwa ajili ya kuleta
muingiliano sahihi na utendaji bora yaani Checks and Balances. Lakini
kwa mfumo tunaotumia wa Westminster, bunge ndio limepewa madaraka ya
kuwajibisha vyombo vingine pamoja na kutunga sheria (Parliamentary
Supremacy). Hii ndio maana Bunge lina kinga (immunity) ya kufanya
shughuli zake na hizi kinga zimewekwa kwenye Katiba. Hii ni kuepuka
mambo kama haya, wenzetu wazungu yalishawatokea na walitupa huu
utaratibu wakijua. Kwa uamuzi wa leo, haikuwa sahihi mtu kwenda kufungua
kesi mpya na kuomba kuzuia bunge kwani hakuna uhuru ulioingiliwa. Kama
kuna kesi zilizoko mahakamani, ukitoa hii mpya ya leo, basi majaji wake
walitakiwa kutoa mipaka ya nini kinaweza kuamuliwa na sio kusema bunge
haliwezi kujadili. Hii ndio precedent mbaya sana na ukizingatia majaji
pia wanashutumiwa kwenye hiyo report ya CAG. Hatuwezi kusema ni utawala
wa sheria wakati anayezuia mjadala ni muhusika pia."
SOURCE:FACEBOOK
SOURCE:FACEBOOK
0 comments :
Post a Comment