MCHAKATO wa kukabiliana na foleni katika Jiji la Dar es Salaam, jana ulipata msukumo mpya baada ya Serikali kupokea kivuko kipya kinachokwenda kasi zaidi kuliko vyote nchini, ambacho kitakuwa kikifanya safari zake kati ya Dar es Salaam na Bagamoyo, mkoani Pwani.
Mbali ya serikali kuahidi kuleta kivuko hicho pia imekuwa ikiboresha barabara zake kuwezesha magari yaendayo kasi, lakini pia imekuwa ikipanua kwa kiwango cha hali ya juu barabara katika Manispaa zake tatu za Dar es Salaam ambazo ni Ilala, Temeke na Dar es Salaam.
Kivuko hicho kilipokewa jana na Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli ambaye alisema ujio wake ni juhudi za serikali katika kukabiliana na foleni Dar es Salaam.
Alisema kivuko hicho kimegharimu Sh bilioni 7.9 na kitaanza kutumika hivi karibuni baada ya kukamilika kwa ukaguzi wa mwisho, ambapo pia aliwataka wananchi kushiriki katika kukilinda.
"Kivuko hiki kitasaidia kupunguza tatizo la foleni, sasa hivi hakuna ulazima wa watu wanaotoka Bagamoyo kuja na magari yao mjini kwa sababu tayari kuna urahisi wa kivuko ambacho kinachukua watu wengi zaidi," alisema Magufuli.
Alisema jambo hilo ni la maendeleo, kwani kivuko hicho kitatumiwa na watu wote bila kujali itikadi za vyama vyao, kwani linapokuja suala la maendeleo hakuna suala la vyama kutokana na maendeleo yenyewe kutokuwa na chama.
Naye Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), Marcellin Magesa alisema mipango ya ujenzi wa kivuko hicho ni kwa ajili ya kupunguza msongamano, ambapo kivuko hicho chenye uwezo wa kubeba abiria 300 kimejengwa na mkandarasi M/S Johs Grahm-Hanssen wa Denmark.
Alisema kivuko hicho kabla ya kuingia nchini kilikaguliwa na Mamlaka ya Majini na Nchi Kavu (Sumatra), Ujenzi pamoja na TEMESA ili kuhakikisha kinakidhi mahitaji, lakini kikiwa hapa nchini kabla ya kuanza kutumika kitafanyiwa majaribio tena.
"Wapo wataalamu saba wanaokuja leo (jana) kuwapa mafunzo watumishi wa kivuko hiki namna ya kuwasha vyombo mbalimbali vilivyofungwa kwenye kivuko hiki, kuendesha na kukitunza," alisema.
Alisema kivuko hicho kimefungwa vyombo vya kisasa vya kuongozea ikiwemo GPS, dira na mfumo wa kisasa wa kukifuatilia kwa ajili ya kuongozea pamoja na kamera za usalama na vyombo vya kujiokolea.
Aidha, alisema kivuko hicho kimejengwa kwa mabati maalumu ya Aluminium ambayo hayapati kutu kwa haraka. Urefu wa kivuko hicho ni meta 37.5 na upana wa meta 10.5.
"Kwa niaba ya TEMESA, napenda kukupongeza kwa juhudi ambazo umezifanya na kuwezesha serikali kununua kivuko kipya cha aina yake, katika uongozi wako vivuko vimeongezeka na sasa vimefikia 27," alisema.
SOURCE:HABARI LEO

0 comments :
Post a Comment