Sixtus Kimaro enzi za uhai wake
MTUHUMIWA wa kesi ya kulawiti mtoto wa kiume, aliyekuwa akitafutwa na Mahakama ya Rufaa, Sixtus Kimaro, ambaye alikutwa na tuhuma hizo wakati akiwa Padri katika Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, amefia nchini Msumbiji na mwili wake umesafirishwa kuja Dar es Salaam.
Taarifa za kifo cha Kimaro zilifikia gazeti hili jana kuwa mwili wa Kimaro, ulikuwa umeshafikishwa katika Hospitali ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Lugalo.
Baadaye taarifa hizo zilithibitishwa na Katibu wa Askofu Mkuu wa Jimbo la Dar es Salaam, Padri Denis Wigila. Akizungumza na gazeti hili, Padri Wigila alisema Kanisa limepata taarifa za kifo hicho kilichotokea nchini Msumbiji.
“Kimaro siyo Padri, kwani aliishaacha kuwa Mlei, hivyo Kanisa halishiriki katika utaratibu wa mazishi kikanisa,” alisema Padri Wigila.
Padri Wigila alisema taratibu za mazishi, zinafanywa na familia ya marehemu kama ilivyo kwa muumini mwingine, na familia hiyo inatarajia kusafirisha mwili wake leo kwenda mkoani Kilimanjaro kwa maziko.
Kwa upande wake, Msemaji wa Baraza Kuu la Maaskofu (TEC), Padri Anatoly Salawa, alipohojiwa kuhusu tukio hilo, alisema walipata taarifa ya kifo hicho na kuelezwa kuwa mwili wa marehemu ulikuwa ukitokea nchini Msumbiji na kupelekwa katika Hospitali ya JWTZ Lugalo.
Kutoroka
Julai mwaka huu, Mahakama ya Rufaa ilishindwa kusikiliza rufaa ya Jamhuri dhidi ya Kimaro, aliyehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela na baadaye kuachiwa na Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam.
Kushindwa kusikilizwa rufaa hiyo, kulitokana na Kimaro kutokujulikana alipo, kwa vile alishaacha kutoa huduma katika kanisa hilo.
Kabla ya hatua hiyo, Wakili wa Serikali, Salum Malick alieleza kuwa wamepata taarifa kwa Msajili wa Mahakama hiyo, kwamba mhusika alipelekewa hati ya wito kwa mwajiri wake, Jimbo Kuu la Kanisa Katoliki Dar es Salaam, lakini waliambiwa kuwa kwa sasa Kimaro siyo mwajiriwa wao tena na hawajui mahali alipo.
Jela
Kimaro alihukumiwa kwenda jela miaka 35 katika kesi ya msingi namba 786 ya mwaka 2005, iliyokuwa ikimkabili, ambapo alikuwa na mashitaka matatu, yakiwamo ya kumlawiti mtoto wa kiume wa miaka 17, shambulio la aibu na kumdhalilisha mtoto huyo.
Padri huyo alikamatwa na askari Polisi wa doria Mei 18, 2005 usiku katika eneo la Changanyikeni jijini Dar es Salaam, ambapo katika kesi yake aliyekuwa Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Pelagia Khaday, Agosti 9, 2006, alimtia hatiani kwa mashitaka yaliyokuwa yakimkabili.
Kimaro baada ya kupatikana na hatia katika makosa yote, alihukumiwa adhabu ya kifungo cha miaka 35 jela. Katika kosa la kwanza alihukumiwa adhabu ya kifungo cha miaka 30 jela, na katika kosa la pili alihukumiwa adhabu ya kifungo cha miaka mitano jela na akaamuriwa kumlipa mtoto huyo fidia ya Sh milioni mbili.
Kuachiwa
Hata hivyo, Kimaro alikata rufaa Mahakama Kuu ambayo ilisikilizwa na Jaji Robert Makaramba, akipinga hukumu ya Mahakama ya Kisutu. Katika hoja zake alidai kuwa Jamhuri haikutoa ushahidi wa kutosha wa kumtia hatiani kwa mashitaka yaliyokuwa yakimkabili.
Jaji Makaramba alikubaliana na rufaa hiyo na Machi 14, 2008, alimwachia huru akisema kuwa ameridhika kwamba hapatakuwa na ushahidi wa kutosha wa kumtia hatiani.
Jaji Makaramba alisema kuwa hitimisho lake katika hukumu yake kulingana na muda na mahali mjibu rufani na mtoto huyo walikokutwa, ni ushahidi wa kimazingira.
Alisisitiza kuwa shahidi wa pili na wa tatu wa mashitaka, ambao ni askari waliodaiwa kumkuta Kimaro akitenda kosa hilo na mtoto huyo, hawakueleza kwa uhakika kile ambacho mjibu rufani alikuwa akikifanya.
Jamhuri katika rufaa yake, iliwasilisha jumla ya hoja saba kupinga hukumu ya Mahakama Kuu ya kumwachia huru Kimaro.
Serikali katika hoja zake, ilidai Jaji aliyesikiliza rufaa hiyo, pia alikosea kisheria na kiukweli kueleza kuwa hapakuwa na ushahidi wa moja kwa moja wa nini mjibu rufani alikuwa akifanya eneo la Changanyikeni Dampo.
Jaji huyo aliyesikiliza rufaa, alidaiwa kuwa alikosea kisheria na kiukweli kwa kutotambua ushahidi wa shahidi wa nne katika mashitaka hayo, bila kutoa sababu zenye nguvu na kwamba alikosea kisheria kwa uamuzi wake kuegemea kwenye ushahidi wa mazingira.
Aidha, upande wa Serikali ulieleza kuwa Jaji huyo alikosea kisheria kueleza kuwa shahidi wa nne wa mashitaka na mjibu rufani, walilazimishwa na uchunguzi wa kitabibu na kwamba Fomu ya Polisi Namba 3 (PF3) iliyowasilishwa mahakamani, ilikuwa ni kusudi la utambuzi tu.
Katika hoja hizo za Serikali, Jaji huyo alidaiwa kupotosha kwa kuhusisha sheria inayohusu ushahidi wa kimazingira na kwamba alikosea kisheria na kiukweli kusema kuwa hapakuwa na ushahidi wa kuunga mkono ushahidi wa shahidi wa nne.
Pia, Serikali ilidai kuwa Jaji aliyesikiliza rufaa, alikosea kisheria na kiukweli kueleza kuwa hapakuwa na ushahidi wa kutosha kuthibitisha
0 comments :
Post a Comment