-->

MASHEKH KENYA WAOMBA USALAMA,NI BAADA YA KUUAWA IMAMU MWARANGI

Polisi wameanzisha uchunguzi juu ya mauaji ya Ustaadh Khalid Mwarangi, Imam wa Masjid Bilal, Likoni, yaliofanyika majuz usiku, huku wakaazi wa eneo hilo wakishinikiza idara ya polisi kuwahakikishia usalama.

Watu wawili waliokuwa kwenye pikipiki walimlenga risasi marehemu alipokuwa akielekea msikitini wakati wa Ishai. 

Itakumbukwa kwamba mbinu ya wahalifu kutumia pikipiki kutekeleza mauji imekithiri sana katika kaunti ya Mombasa katika siku za hivi karibuni.
Aidha usalama wa viongozi wa mpango wa nyumba kumi huenda ukawa matatani ikizingatiwa kwamba huenda ikawa wanalengwa na wahalifu hao.

Idara ya usalama imekuwa ikiahidi kuwakabili wahalifu wanaotumia pikipiki na kukomesha tabia hiyo lakini hadi kufikia sasa hilo linaonekana kutotekelezwa.HIFADHI

Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment